Kwa nini wanaume hamtukubali na watoto

Kwa nini wanaume hamtukubali na watoto

masai dada

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
17,386
Reaction score
19,309
Ni swala la ajabu sana ambalo pengine ukilifukiria unaeza ukasikitika.

Ni kawaida sana wanaume kutuambiwa wana watoto hata watatu na wenyewe kuona kawaida sana bila hata kutushawishi kwamba utaishi na mwanangu.

Yaani wao uchukulia kawaida sana sisi kuishi na watoto wao bila kuuliza chochote na wao huona sinkikwazo chochote na pindi utakapokionesha basi unaonekana Mkatili unaonekana wewe sio mke mwema(JAPO KUNA WANAWAKE HUKATAA ) ila sio wengi.

SASA IJE SISI NDO TUNA WATOTO
Wanaume wengi hukataa kuoa mwanamke mwenye mtoto KWA MSISITIZO na hata kama akikubali husema basi mtoto wako akae kwa bibi au baba ake sijui atawajibika na mambo mengi hapo katikati.

SASA SWALI NI JE KWANINI NYIE MNAONA SISI KUKAA NA WATOTO WENU NI RAHISI LAKINI NYINYI KUKAA NA WETU NI ISSUE tena kubwa sana?
 
hii kweli ni ngumu kwao kukubali ila sio wote masai dada wengine ni wastaarab sana ambao pia ni wachache mnoo ngoja tusubirie majibu
 
Last edited by a moderator:
mimi siwezi kulea bao la mwenzangu

Sasa kwanini wa kwako uliezaa na mamaafacebook namlea (natania) ila mie niliezaa na TANMO hutaki kumlea?

Ila MO11....hiyo kasumba imepitwa na Wakati, kama unanipend mimi, kwanini uchukie mtoto ulienikuta nae?
Kama ukimchukia mwanangu...jua utanikosa.
Huo ni ubaguzi mkubwa
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri hata wanawake wenyewe mnachangia hili suala kwa kiasi kikubwa sana hapa namaanisha Dada zetu na mama zetu.
Nakutolea mfano,shangazi yangu(Dada Wa baba) alipendwa na mjomba na wakaanza kuishi wote kabla ya kufunga ndoa.lakini shangazi yangu alikuwa ameshazaa na mwanamme mwingine.amini husiamini mama mkwe wake na mawifi zake walimchukia sana kisa kwanini kaka yao amemchumbia mwanamke mwenye mtoto.nakumbuka ilibidi yule mtoto Mimi namwita binamu baba yangu amchukue tuishi naye lakini chuki hazikuisha kwa shangazi yangu.
 
Kwa kuwa dada yangu umesema WANAUME,bhasi naomba nijibu swali kwa swali kama mwanaume ambae niko included humo...
Kwann mwanamke anaongezeka thamani na kuonekana wa maana sana endapo atajitunza mpaka wakati wa kuolewa????
 
mimi sikubali kabisa mwanamke aliezaa full stop......sasa mwingine unakubali mwanamke mwenye mtoto halafu huyo mtoto humkubali huko ni kutokujitambua utaweza vipi kumtenganisha mwanamke na mtoto wake?? worse case scenario baba wa mtoto lazima ahusike hapo! ndio maana mimi mwanamke aliezaa....NO NO NO!
 
hii kweli ni ngumu kwao kukubali ila sio wote masai dada wengine ni wastaarab sana ambao pia ni wachache mnoo ngoja tusubirie majibu

wapo wanawake wengi wanakubali watoto
na wanaume ni wachache mnoo kukubali watoto wetu
 
Last edited by a moderator:
Kwa kawaida inafahamika mwanaume ndo bread winner.....inakuwa ngumu mtu anajituma kutafuta pesa ili atunze mtoto wa mwanaume mwenzie lakini yeye akiwa na mtoto anachukulia simple kwa sababu pesa anatafuta yeye we mwanamke huwezi kuwa na sauti sana
 
Sasa kwanini wa kwako uliezaa na mamaafacebook namlea (natania) ila mie niliezaa na TANMO hutaki kumlea?

Ila MO11....hiyo kasumba imepitwa na Wakati, kama unanipend mimi, kwanini uchukie mtoto ulienikuta nae?
Kama ukimchukia mwanangu...jua utanikosa.
Huo ni ubaguzi mkubwa
aahahaha mwenza lea tu mwanangu ntakuja mchukua akikua
 
Hii inawahusu sana wanaume wa kichaga....mbadilike.
Nimeshajionea kwa rafiki zangu kama 3.
Wachaga hawakubali watoto atakaowakuta nao mwanamke.
Ila wazaramo...nawapa hongera

wazaramo kidogo wanakubali eeh

hili sikuliangalia kikabila zaidi....nimeliona in general tu
 
Hii inawahusu sana wanaume wa kichaga....mbadilike.
Nimeshajionea kwa rafiki zangu kama 3.
Wachaga hawakubali watoto atakaowakuta nao mwanamke.
Ila wazaramo...nawapa hongera
ila wao ndiyo wanazaa nje balaa
 
Nafikiri hata wanawake wenyewe mnachangia hili suala kwa kiasi kikubwa sana hapa namaanisha Dada zetu na mama zetu.
Nakutolea mfano,shangazi yangu(Dada Wa baba) alipendwa na mjomba na wakaanza kuishi wote kabla ya kufunga ndoa.lakini shangazi yangu alikuwa ameshazaa na mwanamme mwingine.amini husiamini mama mkwe wake na mawifi zake walimchukia sana kisa kwanini kaka yao amemchumbia mwanamke mwenye mtoto.nakumbuka ilibidi yule mtoto Mimi namwita binamu baba yangu amchukue tuishi naye lakini chuki hazikuisha kwa shangazi yangu.

Ewaaaa....nilikua naendelea wewe umeniwahi......wanaume mara nyingi huwa hawana tatizo kabisa ila sasa wanawake hiyo midomo itasemwa mpaka ndoa itavunjika...
Mfano hata staa wetu kaamua kutoka na mwanamke mwenye watoto watatu na ukitazama most ya watu wanaoponda ni women....
Nilitaka kumuuliza hili swali masai dada kwann
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom