Prof. Mbarawa ni Presidential material! Tuwaspot na kuwagroom Presidential materials au tumwache tu yeyote awe?

Prof. Mbarawa ni Presidential material! Tuwaspot na kuwagroom Presidential materials au tumwache tu yeyote awe?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,027
Reaction score
132,783
Wanabodi,

Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo huwa na swali, na hoja, halafu jibu tulitoa wewe mwenyewe.

Moja ya matatizo makubwa ya nchi yetu ni kutokuwa na kitu kinachoitwa succession plan kwenye urais wa nchini, hivyo mwaka wa uchaguzi ukifika, kila mtu anajitokeza na kujiona anaweza kuwa rais wa Tanzania kama ilivyotokea hapa

Hivyo hili ni bandiko la swali, niliuliza jee Tanzania, tuanze utamaduni wa kuwaspoti Watanzania wenye uwezo wa uraisi, yaani presidential materials, na kuwagroom ili kikifika kipindi cha uchaguzi, we just pick tuu miongoni mwao ili tupate kiongozi bora, kama ni rais, rais bora, au tuendelee na huu mtindo wetu wa kuwaacha tuu Watanzania wowote wanaojiona wanauweza urais na wamekidhi sifa na vigezo, wajitokeze tuu kama lile zogo la 2015 ndani ya CCM?.

Yaani tuache kila anayeutaka urais, ajitokeze tuu kugombea na aje awe rais wetu hata kama sio presidential material?. Hivyo kupelekea Tanzania kuja kuwa na hatari ya uwezekano wa kumpata bora rais badala ya raisi bora?.

Sifa za Urais wa Tanzania.
Nafasi ya urais wa JMT, inashikwa na raia yoyote wa JMT mwenye sifa na vigezo. Tangu JMT imezaliwa mwaka 1964, hadi leo zaidi ya miaka 53, tumekuwa na marais watano, marais 4 kutoka bara na rais mmoja tuu kutoka Zanzibar, Ali Hassan Mwinyi. Hivi ni kweli hakuna Mzanzibari mwingine tena aliyekidhi sifa na vigezo kuweza kuwa rais wa JMT?.

Wazanzibari wengine wote wenye sifa waliojaribu, hawakuweza kupata kutokana na kuzidiwa sifa na vigezo na wagombea kutoka bara, matokeo yake hadi leo sisi bara ni 4 kwa 1 Zanzibar. Hali hii iendelee hadi lini?.

Ni kufuatia hali hii, ilipelekea nikashauri
Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Lakini leo, baada ya kumsikiliza Mtanzania huyu ambaye ni Mzanzibari, Prof. Makame Mbarawa, kiukweli kabisa, nimemkubali sana kuwa ana kidhi sifa na vigezo hadi sifa za ziada za nationalism ya Utanzania kwanza, na ni mzalendo wa kweli, kwa sababu kwa kauli na matendo, amethibitisha pasi shaka kuwa yeye kwanza ni Mtanzania, kisha ni Mzanzibari, wakati kiukweli kabisa, kwa Wanzanzibari walio wengi, wao wanajinasibisha kwanza na Uzanzibari wao na kisha ndio Watanzania!.

Hebu msikilize Prof. Mbarawa.

Presidential Material ni nini?, Jee ni Kama Wife Material?.
Kila mwanamke, anakuwa na uwezo wa kuolewa na kuwa mke wa mtu, lakini sii kila mwanamke, anaweza kuwa mke bora, ili mwanamke kuwa mke bora, anapaswa kuwa na sifa za ziada za kumfanya awe mke bora, zaidi ya ile sifa kuu ya kila mwanamke ni uanamke wake, hivyo kila mwanamke anaweza kuwa mke, lakini sii kila mwanamke anaweza kuwa mke bora!, ili mwanamke aweze kuwa mke bora, mwanamke huyo, anapaswa kuwa na sifa za ziada ambazo ndizo humfanya kuwa wife material!.

Vivyo hivyo, kila raia wa nchi yoyote, anaweza kuwa rais wa nchi kwa kukidhi sifa na vigezo, vilivyoainishwa na katiba, lakini sii kila mtu, anaweza kuwa rais bora, ili kumpata rais, atakayekuwa rais bora, rais huyo ni lazima awe na sifa za ziada za presidential material, na ikiwezekana hata presidential personality, yaani tabia za kipresident, na mwonekano wa personalty ya kipresident, ataona jinsi anavyozungumza, anazungumza with powers na authority ya kimamlaka ya urais, yaani rais anazungumza soft but firm, mtu ukiwa rais, kauli yako tayari ina mamlaka, you don't have to shout kila wakati!, au kutoa kauli za ajabu ajabu!. Kwenye set up ya dunia, Mungu ndio The Almighty, na kwenye set up ya nchi, rais ndio kila kitu!, ni kama mungu fulani!, ndio maana hawezi kukosea, hapaswi kupayuka, hawezi kusema vitu vya hovyo hovyo, zile sifa za ziada za kumfanya mtu kuwa na personality ya urais kwa mawazo, maneno na matendo, ndio presidential material, Prof. Mbarawa, kaonyesha anazo!.

Akitokea Mtu Asiye Presidential Material Kuupata Urais, Nini Kitatokea?.
Kwa vile nafasi ya urais inaongozwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, akitokea mtu asiye presidential material kuupata urais, then katiba, sheria, taratibu na kanuni, zitatumika kumbadilisha kwa kumshape hadi awe na presidential personalities, na kufundishwa kubehave na kuzungumza kama rais, with time, mazoezi na uzoefu, hatimaye mtu huyu atakuwa presidential material, ila ikitokea ni mmoja wa wale watu ambao sio presidential material kabisa, then mtu wa aina hii, kubadilika huwa inakuwa ngumu, hivyo kitakachofuata ni mtu huyu atatawala jinsi anavyojua yeye, ataikanyaga katiba, atazivuruga sheria, taratibu na kanuni, hadi anaweza hata kugeuka dikiteta ambapo mwisho wa siku ni watu kujuta na japo taifa linaweza kupata maendeleo ya vitu na sio maendeleo ya watu!. Mtu huyu atakuwa ni bora rais na sio rais bora!, hvyo inapotokea fursa ya watu wamspoti kiongozi ambaye ni presidential material, mtu wa aina hii sio wa kumuacha hivi hivi, mtu huyu anahitaji kuwa groomed, ili kuliepushia taifa letu, na uwezekano wa kumpata rais ambaye sio presidential material. Prof. Mbarawa ni Presidential Material, awe groomed ili tuje tupate rais bora.

Tanzania Tunamapungufu Makubwa Katika Kupata Wagombea Presidential Material.
Ukifuatilia upatikanaji wa baadhi ya marais wetu, akiwemo rais Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli, mtakubaliana na mimi, hazikufanyika headhunting zozote based on vigezo vya ziada, as a results, marais wetu wote wamepatikana kwa personal initiaves zao wenyewe na sio kwa kuwa spotted na kuwa groomed to be statesmen, matokeo yake tumepata marais wengine ni presidential materials na wengine sio, huo u presidential material watajifunzia huko huko ikulu, wengine walijaribisha tuu na kujikuta wamepata wakati kuna wengine walipania sana, na ikabidi wafanye mambo ndipo wapate. Nafasi ya urais ni nyeti sana, isiachwe kushikwa na yoyote hadi wengine kujaribisha tuu na kujikuta wamepata, mnaonaje tukianza utaratibu wa kuwaspot able people ambao ni presidential material, tukawa groom na kuwachagiza kugombea, ili in future, kila rais wa Tanzania, kabla hajagombea, tujiridhishe kwamba ni lazima kwanza awe presidential material, afanyiwe grooming ndipo agombee?.

Jee ni Kweli Jakaya Kikwete Aliurahisisha Sana Urais, Kila Mtu Alijiona Anaweza Kuwa Rais?
Jakaya Kikwete ni born and breed CCM, ni mtu wa watu, a man of the people, easy, simple and down to earth. Alipogombea kuteuliwa, tatu bora alikuwa yeye Jakaya Kikwete, Prof. Mark Mwandosya na Dr. Salim Ahmed Salim. Kati ya watatu hao, kwenye sifa na vigezo based on the strengths, experience na dominant qualities, Dr. Salim ndio was the most experienced with top presidential qualities, akifuatiwa na Prof. Mwandosya, best brain, na very serious a no nonsense man!, wa mwisho kwa sifa ni Jakaya, lakini katika kuchagua, CCM ikaongeza vigezo, viwili, kimoja ni 'uenzetu' na 'kuchagulika', Jakaya akaibuka mshindi kwa vigezo hivyo vipya kuwa ndani ya CCM, Jakaya ndio mwenzetu zaidi kuliko Dr. Salim ambaye mwanzo hakuwa CCM, na Prof. Mwandosya ni mtu wa kuja!. Kigezo cha kuchagulika, pia Jakaya akawabwaga kwa hoja kuwa ana sura nzuri, na ni mtu wa cheko na bashasha, hivyo akateuliwa na kuchaguliwa kwa ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 80%!. Na kweli, utawala wa JK, ukawa ni utawala wa kiushkaji, always smiling, alikuwa ni mtu wa kujichanganya sana akihudhuria misiba hata ya watu wa kawaida, akitembelea wagojwa, ni mtu wa kujishusha, na alipenda sana kusafiri, hadi watu kumuita jina la utani, Vasco Da Gama. Pia katika kipindi cha Jakaya, rushwa, uzembe na ufisadi vilishamiri sana, hadi JK kuitwa ni rais dhaifu!.

Jee Tuendelee Kujiachia Yoyote Awe Rais Wetu, Hata Kama Sio Presidential Material, au Tuandae Succession Plan na Kuwa Groom Marais Wetu?.
Simplicity, cheko na bashasha za JK, zilipelekea watu kuuona urais ni kitu simple, kiasi kwamba JK alipomaliza, walijitokeza wana CCM Zaidi ya 40 kutaka kumrithi!. Huu ni utitiri wa wagombea ambao pia unathibitisha, ndani ya CCM, hakuna any secession plan, hivyo urais hutolewa kwa mtindo wa sadakalawe, anayepata apate, anayekosa akose!. Hatuwezi kuendelea kuwapata marais wetu kwa mtindo huu, kama Tanzania tunataka maendeleo ya kweli, rais wa Tanzania lazima kwanza awe na qualities za presidential material, kisha atengenezwe, kuwa groomed into a good, fine president. Huyu Prof. Mbarawa, ameishaonyesha kuwa anazo qualities za presidential material, kinachotakiwa ni kum fine tune na kumgroom into good, fine president to be!.

Jee Urais wa Tanzania ni Kupokezana Kati ya Mkristo na Muislamu, au Bara na Zanzibar?
Japo Nyerere alikuwa Mkristo, akapokelewa na Mwinyi ambaye ni Mwislamu, baadaye akaja Mkapa ambaye ni Mkristo, akapokelewa na Mwislamu Jakaya Kikwete, sasa ni Mkristu, John Pombe Magufuli, hii inamaanisha rais ajaye baada ya Magufuli ni lazima awe Muislamu, hivyo Prof. Mbarawa, anafiti sana?. au ni no, hakuna kupokezana kidini, hii imetokea tuu by a coincidence, anaweza kutoka rais Muislamu na kufuatiwa na rais Muislamu, na Muislamu tena na tena, au Mkristo na kufuatiwa na Mkristo na Mkristo tena. je
Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki ...

Rais wa Tanzania Akiwa Mkristu, ni Lazima Awe Mkatoliki?.
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ...
Kama ilivyo hakuna kupokezana kwenye urais, ndivyo ilivyo hakuna udini, au udhehebu kwenye urais, mtu wa dhehebu lolote anaweza kuwa rais wa Tanzania, japo marais wote wa Tanzania ambao ni Wakristu, wote walikuwa ni Wakatoliki, kuanzia Mwalimu Nyerere alikuwa Mkristu Mkatoliki, Benjamini Mkapa Mkristo Mkatoliki, na John Pombe Magufuli, Mkristo Mkatoliki, hii haimaanishi kwamba rais wa Tanzania akiwa ni Mkristo, ni lazima awe Mkatoliki, hawa Wakatoliki, wametokea tuu kufuatana by a mere coincidence tuu, tena mwaka 2014, wakati huo, hakuna aliyejua kuwa kuwa Magufuli ndie angekuja kuwa rais ajaye wa Tanzania, nilikutana na jamaa yangu fulani, akanieleza vitu vya ajabu, na mimi nikaviripoti humu, ila hivyo nilivyoelezwa, vilipokuja kutokea na kuwa kweli, ilibidi tuu niendelee kukanusha for the sake of uzalendo kwa nchi yangu. Jee mtu huyo, alinieleza nini?,
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John ...

Jee Kila Mwenye Sifa za Kutoa Rais Bora, Lazima Autake Urais, Lazima Agombee, Au Achagizwe?.
Sisi binadamu ni kama vidole, hatulingani, kuna vingine virefu, vingine vifupi, vingine vinene vingine vyembamba, vivyo hivyo kwenye watu, hatulingani, vivyo hivyo kwenye kupata rais bora, kati ya wagombea wote zaidi ya 40 wa CCM, rais Magufuli ndio ameibuka mshindi, haina maana rais Magufuli ndio the best kuliko wagombea wengine wote!, au kati ya hao Watanzania wote waliogombea, ndio the best we had, no way, kati hao waliogombea na Magufuli, kuna baadhi yao, would have made a better president than Magufuli, lakini katika mchakato, determinant ya mgombea sio who will make the best president, but who is able kutuletea ushindi katika mazingira yaliyopo, mpaka leo naamini Dr. Salim Ahmed Salim na Prof. Mark Mwandosya, would have made a better president than JK!, lakini kwa kwa mazingira yale, wangeweza kuwaletea ushindi?. Vivyo hivyo kwa Magufuli, kwa kukatwa mtu maarufu kama Lowassa, lazima CCM ijiulize imsimamishe nani mwenye uwezo wa kuwaletea ushindi, not necessarily is the best, or ni presidential material or not, issue ni ushindi!
Tuwachagize Presidential Materials Wagombee?.
Kuna Watanzania wengi wenye sifa za kutuletaa rais bora kabisa, lakini wengine hawana vyama, wengine wala hawauwazi urais, hivyo wanapotokea watu wenye sifa kama Prof. Mbarawa, unaweza kukuta ndio wale type ya watu hawauwazii hata huo urais, lazima wachagizwe, hata katika hao wagombea zaidi ya 40 wa CCM ile 2015, sio wote waliutaka urais, kuna baadhi walifuatwa na kuchagizwa kwenda kuchukua fomu na kugombea, hivyo mnaonaje wale wote wenye presidential personalities, or presidential materials, tuwachagize waanze kufikiria kugombea?.

Hitimisho, Tusisubiri Marais Wajitokee Tuu, Tuanze Kutengeneza Marais.
Kuna kauli isemayo, leaders are born and not made, Mimi ni muumini wa good leaders, besides being born leaders, they are made, hivyo lets start making our leaders by grooming them to be good leaders. Kwa upande wangu kwa 2020, nimeishamspoti mmoja kutoka upinzani,
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha ...

Na kwa 2025, niliishamspoti mmoja.
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa ... - jamiiforums.com
huyu Prof. Mbarawa ni wapili, tuendelee kuwaibua presidential materials ili kufikia 2025, tupate viongozi bora, japo mimi binafsi niko kwenye lile kundi tunaotaka 2025 katiba ibadilishwe Magufuli aendelee kama nilivyouliza hapa.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...

Namalizia kwa lile lile swali la msingi, Jee Tanzania, tuanze utamaduni wa kuwaspoti Watanzania wenye uwezo wa uraisi, sifa na vigezo, yaani presidential materials, na kuwagroom ili tupate rais bora, au tuendelee kuwaacha tuu Mtanzania yoyote
mwenye sifa na vigezo, anayeutaka urais, awe tuu rais wetu hata kama sio presidential material?. Hivyo kuja kuwa na hatari ya uwezekano wa kumpata "Bora Rais" badala ya "Raisi Bora"?.

Mfano mzuri ni huyu Prof. Mbarawa, jee achagizwe akampokee Dr. Shein pale Zanzibar ile 2020, ili 2025, aje kumpokea Magufuli huku bara?.
Jumamosi Njema,

Paskali
 
watu wa bara wameitawala zanzibar mfululizo,mkapa,kikwete,magu

natarajia mpambano mkali na mtoto wa mwinyi ambaye ni waziri wa ulinzi

pia mbarawa ajiepushe na kundi la kipara,maana linapingwa sana

pia nashauri apewe muda awe waziri wa mambo ya nje akapate uzoefu,tunaona wa sasa anavyoyumba katika siasa za kimataifa
 
Unataka tuache huu utamaduni Wa watu kujaribu kisha 'Tunawasukumizia"? Mimi nadhani ungeshauri kuwa kama kuna mtu sio presidential material na Bahati mbaya 'tumemsukumizia' tutafute njia ya kumtoa kikatiba kabla taifa halijaangamia.
Ujue kwa taifa wiki moja tuu kuongozwa na MTU asiyefaa kuna weza kuleta madhara kwa miaka 20 mbele
 
Pole sana.Fulani ataponzwa na bwana fulani maana amepewa kitengo kinachoweza kum-Bazili Mramba huko mbeleni.

Najiuliza tu mpaka leo sijui atakuwa amesaini mambo mangapi maana kitengo chake ndio kinaongoza kwa kutuhumiwa kufanya mambo nje ya utaratibu.
 
Hebu acheni ujuha,

Rais ndo kwanza ana miaka miwili mshaanza kumuota mrithi wake,

Badala ya kumbana aliyepo ajikite kwenye huduma za kijamii, elimu, afya awekeze nguvu huko, mnawaza mrithi,

Hivi tutatoka lini kwenye huu ujinga, Maradhi na umasikini?

Tumbane huyu ili hata atayekuja ajue kuwa naongoza watu si maroboti

Watz mnaboa saba
 
Pascal Njaa ( Mayala) huwa nakuelewa sana. Katuka kila post zako nimetafuta biasness nimekosa kabisa.. Huwa unatuliza kichwa sana. Jamaa (Makame) ni Mtu mwenye Hekima sana, msikivu, msomi mzuri na asie na upendeleo wowote katika awamu Hii japo ni ngumu ila jamaa hajabadilika.
 
Pascal Njaa ( Mayala) huwa nakuelewa sana. Katuka kila post zako nimetafuta biasness nimekosa kabisa.. Huwa unatuliza kichwa sana. Jamaa (Makame) ni Mtu mwenye Hekima sana, msikivu, msomi mzuri na asie na upendeleo wowote katika awamu Hii japo ni ngumu ila jamaa hajabadilika.
Kwa hali halisi ya sasa, ni vigumu sana mzanzibar kuwa rais wa muungano. Anaweza kuwa na sifa zooote, lakini being a zanzibari is a disqualification.
 
Back
Top Bottom