So sina nyumba..., so kuna zenye room mbili.., so kuna huyo dada kaolewa... Yaani nimechoka na hizo so, so kabla sijamaliza hata kusoma. Ila, samahani, mimi nahisi wewe ndio chanzo cha tatizo kama siyo tatizo lenyewe. Msema kweli mpenzi was Mungu.
Kwani shilingi inazama wakati meli inaelea? Kwa nini kisu kikali kinakata na kisu butu hakikati? MImi si mtaalam lakini majibu ya maswali haya yananianbia kuwa inawezakana wewe ni mwembamba kupitia kiasi. Kwa hiyo ukilala unatengeneza mgandamizo mkubwa kwenye godoro kuliko mtu mwenye ujazo...
Ni kweli Ikulu ya Dodoma haivutii sana Kama ile ya Dar es Salaam. Hata hivyo, napenda kukusahihisha kidogo kuhusu ikulu ya Afrika ya Kusini.
Ni hivi, majengo yanayotumika kama ikulu ya South Africa yanaitwa Union Buildings yaani Majengo ya Muungano. Na Muungano wenyewe ulifanyika mwakabe1910...
Basic ya 750? Kima cha chini mpaka Sasa ni sh. 170,000/- kwa mwezi. Sasa wewe unamaana gani na hiyo 750 yako? Unamaana ya 750,000/- au kitu kingine? Unaweza ukapata jibu lisilo sahihi kutokana na ulichokiandika.
Kwa ufupi kabisa ni kwamba serikali inapendekeza kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wake kutoka sh. 2,040,000 kwa mwaka (sawa na sh. 170,000/- kwa mwezi) hadi kufikia sh. 3,240,000/- kwa mwaka (yaani sh. 270,000/- kwa mwezi) kuanzia Julai 2020. Hapo utaona kuwa kima cha chini cha...
Hongera mkuu kwa miyo wa utu. Huyo msaidie kuondoa guilty kwa kumwonyesha kuwa kuna jambo unakwama na yeye ndiye anayeweza kukusaidia.
Kisha mwombe msaada wa jambo la kawaida tu ambalo liko ndani ya uwezo wake. Mfano, unaweza ukamwambia kuwa unatamani sana kula ugali na mrenda au dagaa au...
Msije mkamdanganya kuwa mtoto ni wake. Mtoto anayezaliwa na miezi saba atakuwa hajakomaa (premature au njiti). Kwa maelezo yako ni kwamba mtoto amezaliwa na afya njema. Hii ni kusema mimba ilitungwa kabla ya mwezi Desemba 2018 (kwa vyovyote vile ni mwezi Novemba au hata kabla). Huyo shemeji yenu...
Kukataa kuwa hamna maumbile madogo ya kiume (silipendi neno "vibamia") ni kunitia upofu. Ni sawa na kusema hakuna watu marefu/wafupi, wanene/wembamba, weusi/weupe, wanaume/wanawake.
Hivyo vitu vipo na kwa kiasi kikubwa ni function of genetics. Ni kama tu unavyowaona wanaweke. Wapi wenyewe...
Mkuu Mwanakiji, nimebaini kuwa kila mmoja kati ya wale wazazi anampenda zaidi mtoto wake marehemu aliyemzaa nje ya ndoa na mwanamke/mwanaume mwingine alipokuwa kijana. Japokuwa si rahisi kwa mtu kumsahau mtoto wake aliyefariki, ni ajabu kidogo kufanya hizo kumbukumbu on the expense of the living...
Itakapompendeza Mungu na Rais wa JMT nikateuliwa kuwa mkuu wa mkoa au hata wa wilaya, nitapiga marufuku watu kuvaa sare za chama katika matukio muhimu ya kitaifa kama Haya.
Naamini kuwa hii itasaidia kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa bila kujali itikadi za kisiasa na kulinda hadhi ya Rais...
Yaani mbunge anadai kuwa usafiri wa ndege utasaidia kushusha gharama za usafiri? Usafiri gani anaouzungumzia? Labda angesema usafiri wa ndege utaokoa muda kwa watakaoweza kuutumia.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.