Hili lipoje? Msaada wa mawazo

qarem

JF-Expert Member
Oct 19, 2018
612
785
Hello everyone..!! Nadhani mpo fresh wakubwa!! Naenda moja kwa moja kwenye mada ;

Jamani ndugu yenu sijui nina tatizo gani aiseh, nikilala katika godoro sehemu ninayo lala lazima ijenge shimo, nikiamka asubuhi najikuta nipo kwenye shimo, mgongo na kiuno vinakuwa vinauma!!

Nimeuliza kwasababu kuna kipindi nilikua naishi na demu mmoja hivi sehemu yake anayolala akiamka ipo kawaida na ana mwili sehem ninayolala mimi imejenga shimo!! Nikasema may be ni ubora wa godoro but why ni kwangu tu ukizingatia godoro ni mpya?

Now nipo nimekuja home kusalimu nalala na mdogo wangu wa kiume sehem anayolala ipo kawaida ila mimi kwangu kumejenga shimo na tatizo ni lile lile naumia mgongo na kiuno!!

Sasa ndugu zangu ninaomba ushauri wenu nijue shida ni nn maana kama ni ubora wa godórokwanini kwangu tu ndo hujenga shimo na nina kilo za kawaida tu 65,!!?

Msaada wa kitaalamu tafadhali wakuu!natanguliza shukran!!!
 
Jipige kifuani sema mm ni kidume nna uzito

Nikutoe wasi wasi hauna shida ila inaonekana unalala mahala pamoja kwenye godoro yaani ukilala haugeuki unabaki palepale
Asante sana Mkuu!! Ushauri wako ni mzuri sana
 
Hello everyone..!!nadhani mpo fresh wakubwa!! Naenda moja kwa moja kwenye mada ;

Jamani ndugu yenu sijui nina tatizo gani aiseh,nikilala katika godoro sehemu ninayo lala lazima ijenge shimo,nikiamka

Msaada wa kitaalamu tafadhali wakuu!natanguliza shukran!!!
Kwani shilingi inazama wakati meli inaelea? Kwa nini kisu kikali kinakata na kisu butu hakikati? MImi si mtaalam lakini majibu ya maswali haya yananianbia kuwa inawezakana wewe ni mwembamba kupitia kiasi. Kwa hiyo ukilala unatengeneza mgandamizo mkubwa kwenye godoro kuliko mtu mwenye ujazo mkubwa (nyama nyingi). Kwa hiyo lazima godoro litabonyea sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom