Nimesoma nikaishia kusikitika tu, kwamba kiswahili ni lugha ya kigeni kwa nchi kama Tanzania. Hili siyo kosa lako, huenda usomaji wako wa kiswahili na uelewa kuhusu historia ya kiswahili ikawa ni shida kwako.
Mara nyingi huwa sijibu hoja dhaifu kiasi hiki, lakini kwa kuwa wewe umejinasibu...
Ukituliza akili unaweza kuelewa maana ya kilichotokea. Hata hivyo najua hamuwezi kufikri zaidi ya hisia mlizonazo dhidi ya Uchaguzi. Tathmini ya kina inatakiwa kufanyika na kubaini chanzo cha kuenguliwa kwa hao nguli wa Upinzani ni nini. Ukishindwa kufikri vizuri utaona unyanyasaji na kuonewa...
Mbona unatoa takwimu ambazo mwenyewe binafsi huna uhakika. Umetumia kigezo gani kutoa takwimu zenye utata kiasi hiki, hayo ni mawazo yako na kama ungepata mda wa kutathmini usingeweza kusema hivyo. WaTanzania wengi wanaakili timamu, hizo takwimu zako si za kweli.
Hii nchi inaheshimika sana ndugu hizo ni hisia zako tu. Nchi hii inajulikana kimataifa sasa sababu ya Magufuli, tena inajulikana kwa maendeleo yake ya kasi sana. Hata hivyo una uhuru, unaweza kuhamia kwa marafiki waliokuambia nchi haiheshimiki maana huenda mnafanana na mnaweza kuwaza kwa hisia wote.
Umeeleza mambo mengi sana ambayo binafsi nimeona kiasi fulani cha weredi katika maelezo yako. Uwezo wa kujenga hoja, kukumbuka historia na kuweka wazi mambo kazaa ambayo yanaonekana kwa wazi. Binafsi nimefurahi jinsi ulivyojitanabaisha na kuelezea kinagaubaga mtazamo wako kama mTanzania...
Mara zote huwa tunashindwa kujua Uhuru na Haki humaanisha nini hasa, kwenye taifa huru na linalojitegemea na lenye sheria zake kama taifa.
Huwezi kudai haki kama hujatimiza wajibu binafsi, huo tutaita UZANDIKI. Kusema hivyo haimaanishi kuwa nakubaliana au sikubaliani na mambo yote yanayoendelea...
Nilichoandika hapo ni Ukweli ambao hauegemei upande wowote wala haupingiki. Tatizo kubwa kwako ni umekuwa mtumwa wa Chama chaka kiasi kwamba hadi umekosa uwezo kifikra, kuweza kutafakari vinginevyo. Hata hivyo sikushangai kwa sababu unatumia hisia zaidi kuliko akili na uwezo kujenga hoja zenye...
Mara zote ukitaka mabadiliko lazima uonyeshe uwezo mkubwa na wakuaminika bila kupingwa na zaidi ya asilimia hamsini ya watu unaoishi nao. Binafsi napenda sana kusikia mawazo ya watu hasa kuwapatia uhuru wa kueleza mitazamo wao na malengo yao.
Kitu ambacho WaTanzania tunakosa ili kufanya mambo...
Mara zote ukitaka mabadiliko lazima uonyeshe uwezo mkubwa na wakuaminika bila kupingwa na zaidi ya asilimia hamsini ya watu unaoishi nao. Binafsi napenda sana kusikia mawazo ya watu hasa kuwapatia uhuru wa kueleza mtazamo wao na malengo yao.
Kitu ambacho WaTanzania tunakosa ili kufanya mambo...
Huu ni mtazamo wako ambao siyo lazima kupingwa au kukubaliwa kwani ni haki yako kutoa mawazo yako.
Binafsi siwezi kukubali au kukataa moja kwa moja, isipokuwa kitu tunachotakiwa kujiuliza ni kwa nini Vyombo vingi vya habari vikiwemo vyombo binafsi havitangazi. Siyo kulaumu na kutoa taarifa...
Umeeleza vyema kulingana na msimamo wako kisiasa, japo uliyoyaeleza pia hayana uhalisia kuhusu wafanya biashara wadogowadogo na bodaboda.
Wafanya biashara hapo awali walikuwa wanatoa sh 1000/= kila siku kama Kodi kwa maana hiyo kufikia 30000/=tsh kwa mwezi sawa na 360,000/=tsh kwa mwaka. Baada...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.