Nimechunguza sana mikutano hii nikagundua wanaohudhuria mikutano ya Ccm karibia wote wamevaa sare za chama kuonyesha ni waandaliwa na ni wale wanaccm wenye vimadaraka ila ukawa ni wananchi wa kawaida wenye uchungu na nchi yao.
Ccm wametoa hela nyingi sana kuharibu upinzani lakini upinzani ndio unazidi kuimarika,walianza na wakina lamwai,Ngawaia, kaburu, Zito,sasa wamempata lipumba,kwa kuwapa hela nyingi
Hizo hela wanazotumia kuhonga Heri wangeficha zije kuwasaidia watakapokuwa bench, maana hata wahonge nani mwendo tunaotembelea huwezi simamisha ghafla watu wakawa salama hivyo ni kunyooka tu mpaka magogoni
Huyu Jamaa aliyeleta hii mada hajielewi, hajui kuwa kingereza ni lugha ya walevi? Wewe nenda bar yoyote waone watu wakiwa hawajalewa wanaongea vizuri kiswahili ila wakishalewa wanaanza lugha special ya walevi, kujua kingereza hakuna uhusiano na kuwa kiongozi bora
Nimefurahi kuona video clip ya mama aliyevaa nguo za rangi ya inzi wa chooni akikatiza mbele ya wamachinga na kuzomewa kuwa ni mwizi, duu ina maana wananchi mitaani karibia wote ni ukawa?
Lowasa amejisafisha vizuri maana amesema mwenye ushahidi wowote kwamba yeye Lowasa ni fisadi aende mahakamani, kama hakuna basi kimya kisikike acheni vuvuzela, shut up and keep quite
Nashangaa kuona serikali inayotumia nguvu za silaha kudhoofisha nguvu ya umma na demokrasia.Ukiwa kinyume na mawazo ya serikali ya Tanzania au hukubaliani nayo, tegemea kufa kwa risasi. je, wataweza kuwamaliza watanzania wote?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.