Moto mkali wawaka Julius Nyerere International Airport; wadhibitiwa

Oct 23, 2014
39
10
Wadau kuna mwenye taarifa kuhusiana na moto unaoendea kuwaka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere usiku huu?

Nyongeza shughuli zote zimeamishiwa Terminal one.
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg


====== Habari Zaidi =======

Moto mkubwa umezuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) usiku wa leo na kusababisha taharuki kubwa kwa wasafiri na watumiaji wa uwanja huo, ambapo imelazimu shughuli zote uwanjani hapo kusitishwa kwa muda wakati vikosi vya zimamoto vikiendelea na kazi yao kwenye uwanja huo mkubwa zaidi nchini Tanzania.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Martin Otieno ameuambia mtandao huu kuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo na kwamba uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha moto huo na hasara iliyosababisha, unaendelea kufanyika na kwamba tayari shughuli zote za kawaida zinaendelea kama kawaida.

Taarifa zaidi, zitatolewa baadaye.

Source GPL

Habari zaidi zinasema...

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa ameunda kamati ya watu 12 kuchunguza tukio la moto uliotokea usiku wa kuamkia leo.

Alisema ameunda tume huyo kwa lengo la kupata sababu za kitaalamu.

Tume huyo inayoongozwa na Joseph Nyahende kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imepewa mwezi mmoja kutoa taarifa ya sababu za moto huo.
 
Back
Top Bottom