Enny,
Pole sana kwa muda uliokuwa mbali na familia yako. kwa kuwa umepata kazi tayari wala huna haja ya kujishauri, cha muhimu ni kuondoka bila bosi wako kutoridhika na uamuzi wako, kwa kuwa mnaweza kukutana popote, si unajua maisha? hata hapo unapoenda anaweza akaja akawa tena bosi wako...