Hiyo kazi nzuri unayosifia ilitakiwa ionekane ktk maisha ya kila Siku ya Wananchi. Mtoa mada anachosema ni kwamba pamoja na tumbua tumbua zote lakini hali za maisha ya wakulima wafanyakazi Wafanyabiasha ni mbaya sana. Uchumi nao unachungulia shimoni.sasa hicho cha zaidi unachokiona wewe ni nini!!
Ni sawa sauti ni ya Kachero Membe kabisa, lakini Mbona sioni baya lolote aliloongea? Kwa sasa kila mtu ameshakichoka hiki chama hata JPM mwenyewe na ndiyo maana anawateua wapinzani kuwapa madaraka anawaacha CCM wenzake.
Mkuu shangaa, ati mtu unamchangia Yule mwanamke tapeli Wastara pesa ya Matibabu India na hapo hapo unakataa kutoa pesa za kuokoa maisha ya mbunge aliyepigwa risasi 32 na Mungu akamponya, halafu hapo hapo unapinga magoti kanisani ati unamwomba Mungu,huko ni kumtusi. Unafiki umepita vipimo.
Ati sasa hivi mmenogewa mnataka kututawala milele, hahahaa, labda huyo Mungu ni Mjomba wenu, Shubamit, tunamwomba Mungu huyo huyo awavunje vipande vipande wauaji wakubwa
Nakubaliana na wewe kwa baadhi ya mambo mkuu, lakini ukweli ni kwamba mambo mengi mabaya yanayozungumziwa juu ya Mwalimu ni ya kutunga, na pia lazima ukumbuke wakati wa utawala wa Nyerere dunia nzima ilikuwa ni bado sana, elimu walikuwa nayo wachache sana, mitandao haikuwepo kabisa, so ilikuwa...
Mwalimu Nyerere Angekuwa hai Leo ninaamini pengine kwa huu utawala uliopo angekuwa ama Gerezani au Ameuawa kabisa kwa risasi au sumu. Kwa sababu katika vitu ambavyo huyu baba yetu alivipigania ktk uhai wake kwa nguvu zake bila utani au uoga ni haki za watu. Hakuwahi kuogopa kumkosoa au kumkemea...
Mkuu huyo lusinde si unajua anaongozwa na Tumbo? Yeye yupo kwa ajili ya kutetea Tumbo lake tu, kwa hiyo lazima ajipendekeze sana. Huyu ni mtu wa hovyo sana, sijui inakuwaje watu wenye Akili timamu wanakubali kumchagiua mtu Kama huyu kuwa kiongozi wao!
Ni watu waaminifu sana, na ni watu wema sana, hawajui longo longo, mkishakubaliana mmekubaliana, sio watu wa kugeuka geuka, wengi wao hawajui uongo maana yake ni nini, wao ni zaidi ya walokole japokuwa hawana dini, kazi kwao ndiyo kila kitu. Kwao hakuna jobless.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.