Kwani mtu akiwa mgombea inamzuia vipi kuwashirikisha waumini wenzake kumuombea ili aweze kushinda? Ina maana hata angewaomba watu wa nyumbani kwake mngesema analeta ukabila? Kama angekuwa anapiga kampeni na kuomba kura kanisani ingekuwa mbaya lakini ameomba kuombewa kitu ambacho ni kizuri...
Hayo ya kiroho ni ya kweli kabisa na yanawatesa watu wengi sana. Soi mapadri tu hata wana ndoa ambao waliapa mbele za Mungu kuwa watakuwa pamoja hadi kifo lakini wengine wanaamua kuchepuka na matokeo yake madhara yanakuwa mengi sana ktk familia. Tunapaswa kumheshimu Mungu.
Slaa ni mbogo aliyejeruhiwa. Ana hasira za kuukosa umaarufu. Lakini ukweli ambao ameshindwa kuutambua yeye kama Padri ni kuwa Mungu sio mwanadamu. Akimchagua mtu yeye anaangalia moyo na anamtengeneza kuwa mtu mzuri ijapokuwa sisi wanadamu tunaweza kuwa na kumbukumbu ya maovu yaliyofanywa huko...
Mungu ndiye anayejua kila kitu. Acheni maneno mengi zaidi sana tumuombe MUNGU kwa bidii ili nchi ipate mabadiliko mema yasiyoleta madhara kwa baadhi ya watu.
Ni kweli mzee Slaa aachwe apumzike ili atafakari upya maisha yake ya kisiasa. Akishatafakari nadhani atakuja na majibu sawia. Tuache kumuwekea maneno mdomoni tumsubiri aje mwenyewe kuzungumza.
We tapeli halafu unataka ushauri kwa watu wa Mungu? Kwanza wewe mzinzi na hujaokoka bali unawahadaa watu. Ushuri ni wewe utubu mbele za Mungu na mbele za waumini na kuwaambia ukweli kuwa wewe ulikuwa tapeli ila sasa umeacha na wakuombee. Unaweza pia kumtafuta askofu au mtumishi wa kweli wa Mungu...
Sio rahisi hivyo. Labda kama Mungu kweli kakuonesha kwamba ndivyo atafanya. Mtu mmoja tu hawezi kukisambaratisha chama wakati kuna watu maarufu wengi tu ndani ya CCM. Labda wangekuwa wamegawanyika makundi mawili ningekubaliana nawe.
Acheni kujifariji. CCM ni Taasisi kubwa. Labda hao wakubwa wagawanyike kutokana na tukio la EL kuhama. Sanasana kuna watu watakuwa njia panda wakati wa uchaguzi, hususan wale wapenzi wake ambao pia wanaipenda CCM na wasingependa kuhama.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.