Dr. Slaa hatanyamaza, hataishia hapo!

Dr. Slaa hatanyamaza, hataishia hapo!

Hivi kweli watz wamemuelewa Dr slaa?
Dr slaa kweli ametoa ujumbe aliotaka kutoa?
Km hatujamuelewa nn kifanyike, tumpuuze au atueleze upya?
Wachache mlioelewa mnatusaidiaje kuelelwa hoja zake.

Dr slaa ni mtu pekee aliyeanzisha vita ya ufisadi bungeni 2005 _2010 na alipita kutuaminisha kuwa lowasa ni fisadi papa na tulikuwa tunamsubiri atuambie ufisadi umeishaje hadi wamempokea au ilikuwa ni kutafuta umaarufu na kumchafua ili chadema ipate kuwa juu,ndiye mtu pekee tuliyekuwa tunamsubiri kwn alipokuwa akizunguka alidai ushahidi anao,jana ndo amekuja na maelezo kuwa hawezi kukaa na mgombea huyo kwani bado anaamini ni fisadi papa na ushahidi na makablasha ndo yale anayo swali ni kuwa kweli upinzani Tanzania upo kweli? Kama ni kweli aliyosema dr na majibu ya tundu lisu kuna mashaka na mustakabali wa hii nchi
 
slaa akapumzike. amechoka, amejitenga, ni mpweke kisiasa. pia aliyoyaleta sio mapya alishayasema kabla,
watz watajiamulia wenyewe nini ni nini
 
Ha ha haaa Tabby umenikumbusha,

"CCM ni choo" by Slaa,

kwa hiyo wanachama wake akiwemo mwenyekiti wao ni vinyesi ila Lowassa ameopolewa na kuletwa Chadema, Slaa katika ubora wake.
 
Last edited by a moderator:
Lipi ambalo limekuwa jipya na geni alilolisema Dr. ambalo halikufahamika kama si ndani hadi nje ya nchi?

Sana sana ni Lowasa kujiunga na waendesha boda boda badala ya wakubwa wazuri wa ccm. Is this an offence? Sheria gani inamhukumu Lowasa kwa kujiunga na CHADEMA bila wakuu wa nini kule sijui? Acha utani jamaa wewe.

Dr. Slaa akitamka kitu ndicho leo unakiona kuwa ni tamko la Mungu?

Aliposema orodha ya mafisadi mbona hamkuwafikisha mahakamani kwa hukumu kwa kuwa Dr. Slaa alisema?

Alipotetea umma mbona mlimvunja mkono na kumpa ulemavu wa kudumu kama mnamwamini ki hivyo?

Tanzania ni ya Watanzania na si ya ccm.

Kwa taarifa yako hotuba ya Dr. Slaa imewafanya watu waelewe kwamba ana hasira zake binafsi na si za nchi kwa kuwa tu viongozi wake waliamua kumpa ugombea Lowasa badala ya yeye. Hilo ni kosa gani kwa shiria ipi number ngapi ya mwaka gani chini ya katiba ipi?

Kama ccm mlijua lowasa ni mchafu kwa kuw aDr Slaa alisema, pia aliwasema kinakikwete n.k kwanini hamjawafungulia mafaili ya uchunguzi muwafikishe mahakamani ili wahukumiwe? Kwa mujibu wa katiba ya nchi ni nani kati ya Dr. Slaa, Wewe, Ccm na Mahakama wenye mamlaka ya kisheria ya kumtia mtu hatiani? Kwa nini mnashindwa kuwafikisha kwenye mahakama ili watiwe hatiani kwa mjibu wa sheria?

Hao unaosema wamesikia ni majuha wa wapi hao ambao watashindwa kuchambua suala lililodhahiri namna hii? Bila shaka watakuwa julmuiya na vichaa.

Kama Slaa alijua lowasa ni mchafu, na kwamba ni mgonjwa wa akili aliwezaje kumtongoza ahamie chadema? Kumbuka kwamba Slaa ndiye alilyeanzisha mchakato huu na yeye amekubali. Halfu leo aone Lowasa hafai kwa lolote na sisi tumuamini katika hil.


Na kwa hiyo unakubaliana na kila alichosema dr. Slaa, hata KWAMBA CCM NI CHOO NA LOWASA NI KINYESI KILICHOOPOLEWA KUTOKA CHOONI NA KULETWA SEBULENI.

KWA AKILI YAKO WEWE, UNAKUBALIANA NA HILI KWAMBA CCM NI CHOO CHA KILICHOJAA NA KAZI YAKE NI KUTUNZIA MAVI?

Kwa hiyo kuna mtu timamu anayweza kudiriki kusema ni afadhali akakae ndani ya shimo la choo linalonyewa mavi na kuyatunza akiogopa jivi moja lililoko sebuleni?


Hizo akili ni za ccm peke yake .

WATANZANIA NDIO WENYE NCHI, TUNAMPIGIA KURA LOWASA CHINI YA UKAWA NA KAMWE HATUTAKUBALI KULAZIMISHWA KUINGIA KWENYE SHIMTUO LA CHOO LINALOTUNZA MAVI KWA MASLAHI YA FUNZA WA CHOONI. HLO SAHAU.

IT IS OVER!. Tumechoka na hila za ccm na sasa tunakwenda kulizika rasmi 25 October.
Teh teh teh pole sana kamanda ndiyo siasa zilivyo.
 
Slaa ni mbogo aliyejeruhiwa. Ana hasira za kuukosa umaarufu. Lakini ukweli ambao ameshindwa kuutambua yeye kama Padri ni kuwa Mungu sio mwanadamu. Akimchagua mtu yeye anaangalia moyo na anamtengeneza kuwa mtu mzuri ijapokuwa sisi wanadamu tunaweza kuwa na kumbukumbu ya maovu yaliyofanywa huko nyuma. Lakini pia amesahau maandiko matakatifu yanayosema kuwa sisi sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu na tunapewa Neema bure na Mungu. Lakini pia yeye kama Padri anayejua maandiko kasahau andiko linalosema usihukumu usije ukahukumiwa na lingine linalosema Bwana angetazama maovu yetu je ni nani angesimama? Kwani yeye Slaa hana maovu? Lakini hata kama yeye ni mtakatifu je ni nani kampa mamlaka ya kuhukumu wenzie. Hata kisiasa Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kumhukumu mtu kwanini wanaomtuhumu Edward Lowasa hawakumpeleka mahakamani kama akina Yona na Mramba? kwanza ingerahisisha kumuwekea pingamizi la kutogombea urais. Kama mtu anapendwa na wananchi inakuwaje dhambi kugombea urais?
 
IV LOWASSA NI NANI?? ccm wanamsema RAIS WETU slaa nae kwa RAIS WETU zitto nae KWA RAIS WETU lipumba nae KWA RAIS WETU. IV LOWASSA NI NANI??? - JIWE KUU LA PEMBENI
 
Swali langu kwa Dr. Slaa ni hili. Katika maelezo yake amesema hataki Taifa lipate kiongozi mbovu na ambae sio muadilifu. Sasa kwa wagombea wote walio katika mchakato huu ni Lowasa tu ndio mwenye shutuma za Rushwa na Ufisadi? Vp kuhusu yale mengine yanayosemwa ya uuzaji wa nyumba za serikali na Ripoti za CAG na 10% toka kwa makandarasi? Mbona hakuyaongelea? au haya hayatuhusu kuyafaham kwa undani? kama lengo lilikuwa ni kuwachambua wagombea na shutuma zao basi angekua fair na sio kumshambulia mtu mmoja. Why lowasa?????Tunapata mashaka.
 
Dr amepofushwa macho na fikra bila kujijua.Yatamtokea puani
 
Angalau amekuwa mkweli kuwa mchakato wa kumpata mgombea wa chadema ulikuwa ni wa kidemokrasia. Yeye hakutaka demokrasia....alitaka chama kitekeleze matakwa/masharti yake tu ambayo hata hivyo si matakwa au masharti ya kikatiba (kwa katiba ya sasa ya CDM).

Amefanya vema kutoka CDM, lakini hili la kutumika na CCM kumpiga kampeni against UKAWA, litamgharimu sana kisiasa (kusema kuwa ameacha siasa, hakuwa mkweli!).
 
Swali langu kwa Dr. Slaa ni hili. Katika maelezo yake amesema hataki Taifa lipate kiongozi mbovu na ambae sio muadilifu. Sasa kwa wagombea wote walio katika mchakato huu ni Lowasa tu ndio mwenye shutuma za Rushwa na Ufisadi? Vp kuhusu yale mengine yanayosemwa ya uuzaji wa nyumba za serikali na Ripoti za CAG na 10% toka kwa makandarasi? Mbona hakuyaongelea? au haya hayatuhusu kuyafaham kwa undani? kama lengo lilikuwa ni kuwachambua wagombea na shutuma zao basi angekua fair na sio kumshambulia mtu mmoja. Why lowasa?????Tunapata mashaka.
 
Hapa hakuna cha upande wala kununulika slaa hanunuliki alichokiongea tukae na kutafakari ndio uhalisia bravo slaa
 
dr hakutakiwa kuacha siasa,sijui nani kamshauri,,,,,,anatakiwa aanzisha movement nchi nzima kupinga mafisadi kukabidhiwa ikulu,watu watamsapoti,aweke talkshow kwenye tv kila week,,,,,,
 
Madhara ya Dr Slaa niyaonayo mimi ni haya ya gafla dr slaa kugeuka na kuwa mtu hatari katika kipindi hiki nyeti sana anatonyesha vidonda vya udini. Kusema et Sumaye aliamuru askari kuingia msikiitini na mbwa n.k hii kutaka kuibua maswala ya udini. Sasa Waislamu waanze kujenga dhana kwamba huyo ndo mbaya wao. Akumbuke kulenga udini ni hatari kipindi kama hiki. Hivi swala la kumsema Lowasa Mlutherani anataka aaminishe watu kuwa huyo ni wa walutherani na maaskofu wao. Dr Sl amepotoka. But i hope he is too late. Asikilize hotuba za mwalimu alizuia sana watu kutafuta Legitimacy (uhalali) kweny udini huko ni kuanza kupoteza muelekeo wa anachokitafuta. SS haijulikani kama mpinzani au mwana ccm!
 
Hatuna imani na siasa za ukawa hata mjitetee vipi tumechokeza na sias zetu zakutufaya mazezeata shame on you.
 
Hapa hakuna cha upande wala kununulika slaa hanunuliki alichokiongea tukae na kutafakari ndio uhalisia bravo slaa

Dr.Slaa sijui kachanganyikiwa,mimi ni mkristo mkatoliki,Dr. anasema mambo ya ajabu,mara yeye ni Padre,mara Josephine ni mke wake na Mungu amefunga ndoa!!!!
Naomba ni mkumbushe Dr.Slaa,katika mtiririko wa Sakramenti kuna Sakramenti ya ndoa au Sakramenti ya daraja takatifu.Hakuna kitu kama ndoa na Daraja takatifu.
Mtume Paulo aliliambia kanisa,"sio kwamba nimefika au nimekwisha kamilika,la! Bali ninakaza mwendo ili nilishike lile ambalo kwalo nimeshikwa na Yesu"

Dr.Slaa usitake kutuaminisha wewe ni mkamilifu.
Yesu Kristo alisema,"...hakuna aliye mwema ila Baba wa mbinguni tu"
Wema wako Dr.Slaa ni upiiiii?
 
Aliyo yasema ni kweli nayaamini. Tatizo ni Alipo shiriki mazungumzo ya kumpokea mtu anaye jua fika atachafua chama, huku akijua katiba ya chama chake haibani wana chama wapya kupewa nyadhifa, alitegemea nini?. OK sawa kama Lowasa angebaki kuwa mwana chama wa kawaida aliye kuja CHADEMA na hiyo assets, ina maana ufisadi wa Lowasa ungefutika?????......... Huyo mzee huwa namwamini, ktk hili naona kuna mambo kajichanganya.
 
Ukatae ukubali dr.slaa atabaki shujaa wa mabadiliko na ataandikwa kwa wino wa dhahabu kwa yale aliyoyaamini na kusimamia bila kuyumba. Ndie aliyeijenga chadema na kufikia hapo ilipo na kuporwa.mnyonge mnyongeni haki yake apewe.limewagusa endeleeni kutafakari aliyoyasema dr.slaa kwa wenye medula obligata iliyo kamili wanatafakari usikurupuke kwa mahaba
 
Back
Top Bottom