Recent content by Kitang'wa1

  1. Kitang'wa1

    Kama nyie mnaroga na sie tunaroga vilevile

    Hakika Mabadiliko yatakuja, RAIA washachoka sana na uzuri siku hizi wanaelewa pia. Ahsante kwa teknolojia - mitandao ya kijamii kuhusika.
  2. Kitang'wa1

    Joshua Nassari avuliwa Ubunge wa Arumeru Mashariki kwa “Utoro” Bungeni

    Sio habari nzuri hata kidogo, tusubirie chama kitatoa tamko gani, ama mbunge mwenyewe, maana sio busara kuhukumu bila kusikiliza upande wa pili. Muda umebakia mchache kuelekea uchaguzi mkuu, hivyo gharama hizo sijui zitarudi vipi za uchaguzi mdogo. Maoni yangu though. Ahsante Sent using...
  3. Kitang'wa1

    Ndugu yangu acha kujitanua ofisini kwako rudi haraka nyumbani kwako mkeo analiwa

    Jamaa anaumia sio kwamba huyo mwenye mke haambiwi, ila anaambiwa sana tu sema hataki kuamini wala kujishughulisha kutaka kujua ( nilivyomuelewa). Ndio hapo utasikia waswahili wanasema ' uchawi upo'. Ila ukweli ni inakera sana zaidi kuumiza pia. Wenye wake / waume mnajua. Huyo mke sijui...
  4. Kitang'wa1

    Kamanda wa polisi kanda maalum Ilala hawa watu walioko kila kituo cha polisi wanatunzwa na nani?

    Siku raia wakichoka nao, mtasikia tu matokeo yake. Kuna namna nyingi na za kistaarabu kukagua na kukamata, ila siyo UHUNI huu. Ahsante!
  5. Kitang'wa1

    Kamanda wa polisi kanda maalum Ilala hawa watu walioko kila kituo cha polisi wanatunzwa na nani?

    Safi sana umewapiga picha, yaani tunasubiria majibu ya hao (kama kweli) waliowatuma. Hii ni hatari na itasababisha mabalaa kama majambazi kukuvamia kwa kisingizio hicho, na naifananisha na wale wanaokamata pikipiki wakiwa hawajavaa sare, na wakati mwengine kusababisha ajali zinazopelekea...
  6. Kitang'wa1

    Tahadhari kwa watumiaji wa mitandao

    Mataifa makubwa yenye nguvu, yana njia nyingi sana na tofauti ya ukusanyaji wa pesa; Kwanza kufanya PROPAGANDA, iliyo ya kiakili sana na ngumu kugundua, kwenye jamii yake na mataifa mengine. Pili baada ya hapo ni kufanya UJAMBAZI halali (kwa wao), kama vile vita visivyoeleweka na kusapoti...
  7. Kitang'wa1

    Mojawapo kati ya picha zako

    Hello Mkuu Mshana Jr, habari za siku?! Naona mambo yako yameanza tena, ila binafsi siogopi kufa na tayari picha ya kwenye jeneza langu nishaiandaa, nawaambia wanaonihusu wanahisi natania, ila naamini siku nikifariki wataiweka hiyo, labda nifariki nikiwa mzee sana, ila sina hofu ya kifo. Pole...
  8. Kitang'wa1

    Wizara za ULINZI na KAZI, Vilio vinavyowahusu

    Karibuni weledi wa mambo humu, msaidie. Naamini kila kada huupitia mtandao huu kupata habari na kusaidia pia. Ahsante!
  9. Kitang'wa1

    Wizara za ULINZI na KAZI, Vilio vinavyowahusu

    Habari zenu wadau humu?! Mnamo 20 March 2017 nilileta maada humu ya kulalamikia madai yetu sisi mafundi na vibarua Dodoma, hapa. Ilikuwa na kichwa kisemacho; DODOMA, Ujenzi wa Ofisi za Waziri Mkuu na Makao Makuu ya JWTZ, Dhuuma zinazoendelea. WAHUSIKA JF MKIWEZA MUUNGANISHE NYUZI HIZI ILI...
  10. Kitang'wa1

    DODOMA: Ujenzi wa Ofisi za Waziri Mkuu na Makao Makuu ya JWTZ. Dhuluma zinazoendelea

    Inawezekana kweli wewe halikuhusu, ila kuna litakalowahusu, na ni hatari sana kusema kwa niaba yao. Naamini Media Houses, na wengineo tajwa, wakimaliza na habari hizo mlizozitaja, watashtuliwa na kushtuka kukuta hali siyo hali. Ahsante!
  11. Kitang'wa1

    DODOMA: Ujenzi wa Ofisi za Waziri Mkuu na Makao Makuu ya JWTZ. Dhuluma zinazoendelea

    Nimeeleza vema tu ujenzi wa ofisi na makazi, maana yake bado kuna kazi zinaendelea. Tembeleeni pale mujionee MLIMWA C. Na kule kwa JWTZ, kama ujuavyo, ni makao makuu ya ulinzi, kugawana vitu haiwezekani na siyo utaratibu mzuri. Saidieni jamani hali siyo nzuri (kwa wenye access ya kuweza...
  12. Kitang'wa1

    DODOMA: Ujenzi wa Ofisi za Waziri Mkuu na Makao Makuu ya JWTZ. Dhuluma zinazoendelea

    Huu siyo umbea mkuu ni kweli na maumivu yanaendelea. Wakiachana nao stahiki zao watazipataje? Maana bwana mapesa alishatangaza namnukuu; 'mkiringa nyie, naenda Singida, Dsm, mwanza, na mikoa mingine kuchukua mafundi'. Mwisho wa kunukuu. Yaani yupo verry proud na kama kuna anayemkingia kifua...
  13. Kitang'wa1

    DODOMA: Ujenzi wa Ofisi za Waziri Mkuu na Makao Makuu ya JWTZ. Dhuluma zinazoendelea

    Nawashukuru Jf kwa kuurudisha ama kuuweka Uzi huu kwenye jukwaa hili, naamini msaada na haki u/vitapatikana haraka. Ahsante!
  14. Kitang'wa1

    DODOMA: Ujenzi wa Ofisi za Waziri Mkuu na Makao Makuu ya JWTZ. Dhuluma zinazoendelea

    Waandishi wa habari za uchunguzi, fanyieni haya kazi nawaombeni, maana naamini katika nguvu ya habari, ila tu mniwie radhi kwa kutowajumuisha kwenye maelezo ya ndani juu hapo. Haki za raia zinakandamizwa, msaada wenu tafadhali kwa wote niliowataja hapo. Wahusika JF kitengo sijui muhusika...
Back
Top Bottom