Kitang'wa1
JF-Expert Member
- Dec 4, 2014
- 460
- 285
Habari zenu wadau humu?!
Mnamo 20 March 2017 nilileta maada humu ya kulalamikia madai yetu sisi mafundi na vibarua Dodoma, hapa. Ilikuwa na kichwa kisemacho; DODOMA, Ujenzi wa Ofisi za Waziri Mkuu na Makao Makuu ya JWTZ, Dhuuma zinazoendelea. WAHUSIKA JF MKIWEZA MUUNGANISHE NYUZI HIZI ILI WASOMAJI WAPYA WAPATE PICHA PANA.
Bahati mbaya sana sikupata/hatukupata msaada humu kwa kuwa kilikuwa ni kipindi kile cha skendo na stori nchi nzima za baadhi ya viongozi.
Leo tunarudi tena, tukizililia wizara tajwa hapo juu, maumivu na uonevu unaofanywa na watendaji wenu wa chini na wale mnaowapa tenda halafu hamuwafuatilii kwa ukaribu, siyo jambo jema na siyo lazima yatokee ya kutokea ndiyo muanze kuunda tume.
Familia zetu zinalia, kuanzia watoto hadi wake zetu wametununia na hawatuelewi, sikukuu imepita kavu kavu, madukani tena hatukopesheki, na njia tunazibadilisha, ni kurudi tu usiku kukimbia madeni, wakati tunadai pesa nyingi tu.
Kwa sasa (Pale Msalato, Makao Makuu ya JWTZ), walioshika tenda ile wameleta mafundi na vibarua WATANZANIA wasiojua udhaifu uliopo tokea mikoani (kama walivyojigamba tangu awali), wanakula nini wanalala wapi hatujui, na wameongeza WA-SOUTH AFRICA -Blacks- wenzao. Mafundi wenyeji wa mkoa huu wote (idadi kubwa), tumeacha na kuugulia tu maumivu makwetu.
Waandishi wa Habari, Waziri wa Kazi, Waziri wa Ulinzi, Mbunge wa eneo hilo, RPC wa Mkoa huo, Waziri Mkuu, Rais wa Nchi, Mkuu wa Majeshi, tafadhali kila mmoja kwa nafasi yenu mliangalie hili tupate stahiki zetu. Mlituaminisha tufanye kazi, kazi tumefanya hamtulipi.
ANGALIZO: Mkitembelea pale JWTZ Msalato, mtaona mafundi na vibarua, wamevalishwa overroll na mabuti, mkadhani wana furaha, muongee nao kidogo muwasikie, halafu shtukizeni ziara zenu, msitaarifu wahusika. Mtarudi humu ama popote pale kutushukuru.
Imani yetu ni Tutasaidiwa.
Ahsante!