DODOMA: Ujenzi wa Ofisi za Waziri Mkuu na Makao Makuu ya JWTZ. Dhuluma zinazoendelea

Kitang'wa1

JF-Expert Member
Dec 4, 2014
460
285
Habari zenu wadau wa Jf.

Naamini mtandao huu unasomwa na watu wengi wa kada mbali mbali hapa nchini na hata nje ya nchi hii.

Utafiti mdogo nilioufanya mkoani Dodoma (Utafiti binafsi na siyo wa kiofisi), ni kuwa pamoja na nia nzuri na njema ya Serikali ya awamu hii ya tano, kutaka kuhamia Mkoani Dodoma, bado kuna watendaji wachache wanataka kuharibu taswira hiyo.

Mathalani, kuna ujenzi unaendelea wa ofisi mbali mbali na makazi ya watendaji wa ofisi hizo za Serikali iliyopo (wote tunafahamu hilo naamini), ila ujenzi ama jenzi hizo zinachafuliwa na walioshika tenda ama na watendaji husika, KUTOWALIPA WAFANYAKAZI NA VIBARUA KWA WAKATI AMA KUTOWALIPA KABISA AMA KUWALIPA NUSU YA MALIMBIKIZO YAO. Utakuta wananchi wanajitolea kufanya kazi kwa moyo wote (wakiwa na ile dhana ya msemo wa Serikali hii ya, Hapa Kazi tu), ila malipo yao kuzungushwa.

Yanayoendelea kwenye ujenzi wa ofisi / makazi ya Waziri Mkuu, eneo la MLIMWA C, maumivu na vilio hivyo ni ya muda mrefu kama nilivyoeleza hapo juu, na aliyeshika / kuongoza mradi / ujenzi huo ni Mchina. Watu wanalia sana, watu wanadaiwa sana mtaani, pesa wanazisikia tu hewani.

Yanayoendelea kwenye ujenzi wa Makao Makuu Ya Jeshi (JWTZ), eneo la MSALATO, wananchi wanajitoa sana kutafuta ridhiki zao pale, ila malipo wanazungushwa, na wapo wanaodai zaidi ya wiki nne, maana utaratibu wa pale wa awali ulikuwa kulipwa kila siku, wakabadili kulipwa kila baada ya siku tatu, wakabadili tena kulipwa kila baada ya wiki, ila malipo ni hakuna wanaishia kulipwa ahadi nzuri tu. Kuna wakati wafanyakazi waligoma, wakafukuzwa bila kulipwa, ikatokea tena wiki mbili zilizopita 11/03/2017 mafundi na vibarua baada ya kufanya kazi kwa takribani zaidi ya wiki, wakiwa na madeni uraiani, waliahidiwa pesa kutoka wiki hiyo ya tarehe tajwa hapo juu, ila ilipofika jioni mabosi wote walipotea eneo la ujenzi, na pale ni eneo la Jeshi, askari waliopo pale wakawataka mafundi na vibarua watoke nje, maana muda wa kuwa pale uliisha, wakati watu wapo nje wanajadiliana misimamo yao, mara huyo bwana fedha (akijitambulisha kama mwana ccm, mnene, mweusi, anaongea sana na majivuno mengi), akiwa na gari lake aina ya Ford Ranger, nyeupe, akatokea (maana aliambiwa wananchi wanamsubiria awape pesa zao), ila cha ajabu kwa dharau zake, akawapita mafundi na vibarua wale kwa kasi huku akiwatimulia vumbi kwa kutembelea 4WD mchangani. Na watu wakaondoka bila kulipwa.

Hadi leo, watu wanafanya kazi kwa kusononeka bila kulipwa, japo wanatoa chakula cha mchana pale, ila ni kama danganya toto, maana hakitoshi ukizingatia na aina ya kazi zinazofanyika. Cha ajabu bwana mapesa huyo tajwa juu, anajivunia kupata tenda nyengine ya kujenga makao makuu ya Polisi, eneo la Kisasa (kwa mujibu wa maelezo yake, maana ni mropokaji sana na majivuno mengi).

Siku moja kabla ya mgomo huo tajwa juu, walikuja Mkuu wa Wilaya kama siyo wa Mkoa na RPC wa mkoa, na wakitembezwa na huyo bwana mapesa.

Tenda ya pale (Msalato JWTZ), inashikiliwa na Mzungu tokea Afrika ya Kusini, ambaye amekuja na wa-south wenzie ila ni Black's, nao pia cha kushangaza wanazungushwa malipo yao, na siku ya mgomo tajwa juu hapo waligoma.

Serikali kuu, kupitia Mkuu wa Mkoa Dodoma, Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini, RPC wa Dodoma, Mkuu wa Kikosi Jeshi Cha Msalato cha Dodoma, wabunge na Madiwani wa Dodoma, tafadhali chukueni hatua stahiki pesa zitoke na watu wafanye kazi kwa furaha na siyo manung'uniko.

ANGALIZO:

Wakienda Viongozi pale, hawapewi nafasi ya kuongea na mafundi na vibarua, ni mwanzo mwisho kuambatana na bwana mapesa, na huyo mzungu, laiti mkija na kutaka kuongea na raia wanaofanya kazi pale, mtayasikia mengi zaidi ambayo sikuyataja humu. Jwtz pale wana utaratibu mzuri wa kupiga picha mafundi na vibarua, ila hawawasainishi mikataba, jambo ambalo ni hatari kwa kuwa rahisi kudhulumiwa.

Majina ya kampuni husika, wahusika wakuu, na mengineyo, yamehifadhiwa, ila wakibisha yatatolewa. Viongozi tajwa juu hapo, mkishindwa nyie naamini Raisi, atarudi tena Dodoma, kutetea wanyonge hao.

Ahsante!
 
Waandishi wa habari za uchunguzi, fanyieni haya kazi nawaombeni, maana naamini katika nguvu ya habari, ila tu mniwie radhi kwa kutowajumuisha kwenye maelezo ya ndani juu hapo.

Haki za raia zinakandamizwa, msaada wenu tafadhali kwa wote niliowataja hapo.

Wahusika JF kitengo sijui muhusika kwa jina ama title la/ya Mods, nirudishieni maada hii jukwaa la Habari Na Hoja Mchanganyiko. Hii different forum kwa kweli sijawaelewa na siijui.

Ahsante!
 
Nawashukuru Jf kwa kuurudisha ama kuuweka Uzi huu kwenye jukwaa hili, naamini msaada na haki u/vitapatikana haraka.

Ahsante!
 
Potelea mbali acha nao wale!
Si huyo unayetaka awasaidie amesema yeye hashurutishwi wala kupangiwa na mtu!

Mkiona mnaumia acheni!

Alienda kuchukua fomu ya urais peke yake na hasikilizi umbea wa mitandaoni
 
Huu siyo umbea mkuu ni kweli na maumivu yanaendelea. Wakiachana nao stahiki zao watazipataje? Maana bwana mapesa alishatangaza namnukuu; 'mkiringa nyie, naenda Singida, Dsm, mwanza, na mikoa mingine kuchukua mafundi'. Mwisho wa kunukuu.

Yaani yupo verry proud na kama kuna anayemkingia kifua vile.

Ahsante!
 
Mkuu tafuteni njia mbadala tu huko muone mtafanyaje manake bwana yule kasema afanyi maamuzi eti kisa mnasema nini. Ushauri tu mnaweza kugawana nondo, mabati, cement......au hata kulipua lipua tu sio mbaya......nchi ya kiduanzi sana hii mamaaeee.......kweli UN hawajakosea kusema wa mwisho kati ya nchi zenye furaha. Hata Somalia wanatushinda
 
Huu siyo umbea mkuu ni kweli na maumivu yanaendelea. Wakiachana nao stahiki zao watazipataje? Maana bwana mapesa alishatangaza namnukuu; 'mkiringa nyie, naenda Singida, Dsm, mwanza, na mikoa mingine kuchukua mafundi'. Mwisho wa kunukuu.

Yaani yupo verry proud na kama kuna anayemkingia kifua vile.

Ahsante!
Kamateni mgongeni ngumi ndo kilichobaki.....na pesa yenu atalipa vile vile.....
 
Waandishi wa habari za uchunguzi, fanyieni haya kazi nawaombeni, maana naamini katika nguvu ya habari, ila tu mniwie radhi kwa kutowajumuisha kwenye maelezo ya ndani juu hapo.

Haki za raia zinakandamizwa, msaada wenu tafadhali kwa wote niliowataja hapo.

Wahusika JF kitengo sijui muhusika kwa jina ama title la/ya Mods, nirudishieni maada hii jukwaa la Habari Na Hoja Mchanganyiko. Hii different forum kwa kweli sijawaelewa na siijui.

Ahsante!
Wapo bize wanachunguza vyeti vya Makonda badala ya kuchunguza mambo ya maendeleo
 
Nimeeleza vema tu ujenzi wa ofisi na makazi, maana yake bado kuna kazi zinaendelea. Tembeleeni pale mujionee MLIMWA C. Na kule kwa JWTZ, kama ujuavyo, ni makao makuu ya ulinzi, kugawana vitu haiwezekani na siyo utaratibu mzuri.

Saidieni jamani hali siyo nzuri (kwa wenye access ya kuweza saidia). Hata kusema tu ni msaada tosha.

Ahsante!
 
Nimeeleza vema tu ujenzi wa ofisi na makazi, maana yake bado kuna kazi zinaendelea. Tembeleeni pale mujionee MLIMWA C. Na kule kwa JWTZ, kama ujuavyo, ni makao makuu ya ulinzi, kugawana vitu haiwezekani na siyo utaratibu mzuri.

Saidieni jamani hali siyo nzuri (kwa wenye access ya kuweza saidia). Hata kusema tu ni msaada tosha.

Ahsante!
Waandishi na media houses wako biZe na bashite vs clouds
 
Inawezekana kweli wewe halikuhusu, ila kuna litakalowahusu, na ni hatari sana kusema kwa niaba yao.

Naamini Media Houses, na wengineo tajwa, wakimaliza na habari hizo mlizozitaja, watashtuliwa na kushtuka kukuta hali siyo hali.

Ahsante!
 
Back
Top Bottom