mdogo wangu hata mimi hiyo story nikiisikia ila hakugoma kushuka inasemekana siku anatimba MJ kuna sehemu ya jiji walikuwa wamechoma taka sasa ule moshi ukawa unaelekea maeneo ya airport ukichanganya na ule moshi wa pale feri wa kukaanga samaki ikawa hewa mchanganyiko kama anajua zaidi aongezee...
mkuu unetisha sana professor janabi oyeeee kuna nchi tajiri za ulaya usafiri wao mkubwa ni baisikeli na kutembea kwa miguu kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza
mkuu bora huyu kajiweka hadhalani kuepuka aibu mbeleni jimbo liko wazi mbona tz tunao watoto wa vigogo wazeekea nyumbani kina fatuma aka shangazi, halima mdee kina esther bulaya na wengine wengi ila wanaona aibu kujitangaza ndo inakura kwao
mkuu uko sahihi yeye angesema watu wa maofisini tungemuelewa kirahisi mtu uko machimboni unapiga nyundo mwanzo mwisho, uko bandarini unapakia cement ,uko shamba unavuja shasho mwanzo mwisho, ule mara moja kwa cku haiingii akilini afafanue vizuri mie ningemuelewa kama angekuja na ushauri wa...
2025 mkuu sio mbali andaa kichinjio ukipiga kura usiondoke mpaka mshindi atangazwe kaa umbali wa hizo mita 100 zao mwaka huu tunaanza na hao wenyeviti wao walipita bila kupingwa
mkuu wangu mshana Jr acha dawa ituingie mwendazake tulimsema sana kwa kila baya umeme ukatike kutwa nzima chakula kipande mafuta bei juu nauri bei juu wa tz hatuna jema haatunui tunataka nn mie niko shamba huku nasubiri kuvuna mpunga
sasa mkuu ulitaka atuite matajiri wenzie kutuita wanyonge alimaanisha wewe unaweza dhurumiwa haki yako na tajiri na huna pakumpeleka sasa yeye akachukua jukumu lakutusemea wanyonge au wewe kwenu umeme hua haukatiki au una chuki na magu wa vyeti feki nn
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.