Recent content by KAYGREKO

  1. KAYGREKO

    Maandamano ya amani+viongozi wa dini+diaspora

    MAANDAMANO YA AMANI + VIONGOZI WA DINI + DIASPORA Nianze na ukweli ambao wengi tutakubaliana. Afrika hatuna mazowea ya kuwa na maandamano ya amani. Na hata zile nchi zenye uzoefu wa maandamano ya amani, huanza kwa amani na mwishowe huzuka fujo. Kwa nchi yetu ya TZ, na hasa baada ya yaliyotokea...
  2. KAYGREKO

    Tatizo lipo kwetu Waafrika, si kwa Mataifa ya Magharibi

    Nakubaliana nawe kuwa binadamu siku hizi ni wabishi, lakini ktk huu ubishi walionao, je unashauri nini kifanyike ili tuondokane na hali hii mbaya tunayoendelea kuishi nayo?
  3. KAYGREKO

    Tatizo lipo kwetu Waafrika, si kwa Mataifa ya Magharibi

    Umefafanua vyema tatizo ambalo sote tunakubaliana kuwa lipo. Lakini bado hujatusaidia ushauri wako wa nini kifanyike ili tuondokane na tatizo. Unajua moja ya matatizo ambayo wengi tunayo, ni hii hali ya kuendelea kulichambua tatizo bila ya kujaribu kushauri hatua za kulitatua.
  4. KAYGREKO

    Tatizo lipo kwetu Waafrika, si kwa Mataifa ya Magharibi

    TATIZO LIPO KWETU SI KWAO Madhara na unyonge unaotukumba Waafrika, sababu kuu ni sisi wenyewe. Ni kweli wazungu wanaendelea kutubana kwa kutumia mbinu tofauti lakini uhusika wetu katika kufika hapa tulipo bado unabaki kwetu. Huwa najiuliza na kukosa jibu nikiangalia mifano michache ifuatayo...
  5. KAYGREKO

    Diaspora na deni la Taifa

    Usichokijua usikiongelee utawapoteza wanaotaka kujua. Na kama ulikuwa umeongea kiutani basi naona kadhia hii si ya utani.Try to be serious. Je wewe ushawahi kuja nje? Kama bado waulize rafiki zako watakujulisha kuwa hiyo idadi ya laki tatu unayoitaja ni ndogo mno
  6. KAYGREKO

    Diaspora na deni la Taifa

    DIASPORA NA DENI LA TAIFA Hakuna takwimu kamili, lakini inaaminika watanzania tuliopo ughaibuni tunafika milioni mbili. Aidha wengi tunaoishi ughaibuni, tunajua nchi yetu ina deni la nje na la ndani japo wengi hawajui kiuhakika ni kiasi gani. Leo ningependa kuja na ushauri ambao kwa wale...
  7. KAYGREKO

    Tusikwame kwenye udaku pekee

    SI UDAKU PEKEE… Mbali ya sifa ya kupenda habari za udaku ambazo huwafanya wabongo wengi kukesha mitandaoni, kuna upande wa pili wa wabongo ambao wanayoyajadili mtandaoni hayana kabisa uhusiano na wale wa kundi la udaku. UTASUUZIKA NA MOYO YAKO UKIWASIKILIZA. Na hasa kama huna ile hulka hasi ya...
  8. KAYGREKO

    Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?

    TUTAKE TUSITAKE TUTA(.…….) Miezi minane iliyopita, nilipata bahati- mbaya/nzuri- ya kulazwa hospitali ya Red Cross Athens kwa COVID- 19. Kulazwa kwangu hospitali si hoja kinaishi kwa wale watu wangu wa karibu ambao hawaamini uwepo wa ugonjwa huu. Kumekuwa na mjadala mrefu mno khs covid 19 na...
  9. KAYGREKO

    Samantha azuiliwa Hotelini Zanzibar, Hotel inahudumia Wateja Wa Italia pekee

    JE HADI LEO - 2019 - TUUKUBALI UBAGUZI HUU? Jana 18/8 nilipoangalia vdeo aliyotuma MILLARD AYO khs mwanadada mweusi aliyekataliwa kuingia hoteli kule Zanzibar kwa sababu ya rangi yake nilikumbuka zile enzi ambazo kule...
  10. KAYGREKO

    Algeria na Argentina watokomeza ugonjwa wa Malaria

    Cha kujiuliza hapa ni nini walichofanya, tusichoweza sisi kuwaiga?
  11. KAYGREKO

    Viwango vya furaha duniani: Tanzania yashika nafasi ya 153 kati ya 156

    Vigezo vyovyote watavyodai wamevitumia, haviwezi kutupatia ukweli wa hali halisi ilivyo.
  12. KAYGREKO

    Kinondoni, Dar: Ghorofa linalodaiwa kumilikiwa na Balozi Ramadhani Dau lapigwa mnada ili kufidia deni Bank M

    Huu uhakikà wako wa 100% unaweza kuwathibitishia wanaosoma maelezo yako? Maana humu kila mmoja anasema lake kulingana na vile anavyojiona anajua. Hivi mnadhani mnajua sana kuliko vyombo vya uchunguzi vya serikali? Magufuli angemwamini vipi kumpa ubalozi kama Dr.Dau angekuwa na kasoro au mwizi...
Back
Top Bottom