Algeria na Argentina watokomeza ugonjwa wa Malaria

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Algeria na Argentina zimethibitishwa na kutambulika rasmi na Shirika la afya ulimwengu WHO kuwa zimetokomeza ugonjwa wa malaria.

Hatua hii inamaanisha katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, hakujaripotiwa hata kisa kimoja cha mgonjwa wa malaria katika nchi hizo.

Malaria ugonjwa unatokana na kuumwa na mbu umesalia kuwa ni moja ya magonjwa yanayoongoza kwa vifo duniani.

Inakadiriwa kuwa mwaka 2017 pekee kulikuwa na visa Milioni 219 na vifo zaidi ya Laki Nne vya malaria, huku aslimia karibu 60 ya vifo hivyo vikiwa vya watoto wa umri wa chini ya miaka 5.

Algeria ni nchi ya pili katika ukanda wa Afrika wa WHO kutambuliwa rasmi kama imetokomeza malaria baada ya Mauritius ambayo ilithibitishwa rasmi mwaka 1973.
 
Wenzetu waliamua kupambana na malaria kupitia vector control method..kuangamiza mazalia yote ya mmbu na kuhakikisha uruliziaji wa ndani ya nyumba (indoor residual spray).

Sisi tunahangaika na kunywesha watu madawa kila siku na kugawa vyandarua ambayo matumizi yake jayajweza kupunguza maambukizi ya malaria kwa kiwango kikubwa.
 
Back
Top Bottom