KAYGREKO
Member
- Jan 18, 2013
- 37
- 32
TATIZO LIPO KWETU SI KWAO
Madhara na unyonge unaotukumba Waafrika, sababu kuu ni sisi wenyewe. Ni kweli wazungu wanaendelea kutubana kwa kutumia mbinu tofauti lakini uhusika wetu katika kufika hapa tulipo bado unabaki kwetu.
Huwa najiuliza na kukosa jibu nikiangalia mifano michache ifuatayo:
1. Kagame amekubali nchi yake kufanywa dampo ya wakimbizi hata wa Syria, Bangladesh, nk. Amefadhilisha vijimilioni toka UK. Je, madhara ya baadae ameyazingatia?
2. Nchi kadhaa za Kiafrika zimeuza wanyama wengi Uarabuni kiasi cha kwamba Dubai imeanzisha Safari park yenye mvuto wa hali ya juu hadi wengi washaanza kufadhilisha kwenda huko badala ya kuja Afrika. Je, watalii watapopungua kuja kuangalia wanyama Afrika tutawalaumu wazungu/Waarabu?
3. Eti sisi wa kukosa ngano kwa sababu ya vita vya Ukraine na Urusi? Tunategemea kuagiza wakati tuna ardhi yenye rutuba kuliko ya huko tunakotegemea kuagiza. Je, na hapa tutawalaumu Wazungu?
4. Kuna mifano mingi mno ya kila pande ambayo kwa ujumla wake inaonesha wazi kuwa tatizo kuu lipo kwetu si kwa wenzetu .
Je, tunaanzaje kujinasua kwenye tope hili?