Atakua sahihi kwa alichofanya ili liwe funzo kwa wengine, kwa maneno yake huyo alikua mwanamke wa kwanza na hakujua kwamba SIO KILA MWENYE UKE ANASTAHILI KUWA MKE.
nilichomaanisha ni kwamba matokeo ya DNA test hayako 100% perfect. ingekua bora kama amepima sehemu kama tatu halafu afikie maamuzi hayo, ni maamuzi mazito mno
Mke ni zaidi ya tendo la ndoa, jiulize mipango yako katika maisha ni ipi, angalia kama huyo ni mtu sahihi kuwa mwenzi wako katika maisha yako na familia utayojaaliwa na Mungu, kama ana vigezo vinavyokufaa fanya utaratibu wa kumuoa kama na yeye ana nia ya dhati na pia hujaeleza mmefahamiana na...
nadhani gesti zinazozungumziwa hapa ni zile za bei rahisi, ambazo pembeni au kwenye hizo gest utapata pia na pombe za kienyeji na umeme ukikatika kunawashwa taa za chemli ,popote utakapo lala gesti za aina hiyo utakua mtu wa ajabu sana ukiwashangaa kunguni
kumuacha huyo mke ni bora kwake, huwezi kuvumilia tabia mbovu za mke kwa kisingizio cha watoto, hakuna jema watoto wanalojifunza hapo, aache utegemezi wa kuamini hawezi pata mke bora kuliko huyo, ataishia kwenye presha na ugonjwa wa moyo
jambo lolote lililoruhusiwa na Mola lina hekima ndani yake, kama watu wote tungekuwa wachamungu kutoka moyoni swala kuoa mke zaidi ya mmoja hekima yake ingeonekana kwa wazi zaidi.
hata mimi nilikua na tabia hiyo japo nilikua sichukui muda mrefu nilikua sizidishi siku 3 kutokana na imani ya dini, mara nyingi tabia ya aina hii kwa waliowengi inaanzia kwenye malezi ya utotoni kama mama yako mzazi alikua anakupenda sana na kukudekeza ni rahisi ukioa ukawa una deka kwa mkeo...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.