Mabala The Farmer: Asante kwa comment yako. Kwa jukwaa huru kama JF where everyone dare to talk openly, ukiwa na tabia ya kuwatukana wale wanaosema yale unayopingana nayo, au yale usiyoyaamini je ndani ya mwaka mmoja utatukana wangapi? Kama JF ingekuwa na Forum ya watu kutoa mawazo yanayofanana...
Sina hakika endapo ni sahihi kwamba Dr. Ulimboka ni Mtumishi wa Serikali. Nadhani nimepata kusoma katika vyombo vya habari wakati wa ule mgomo wa kwanza wa Madaktari kuwa Dr. Ulimboka hakuwa Mtumishi wa Umma, isipokuwa Madaktari walikuwa na imani naye kuwa atawawakilisha ipasavyo kwenye madai...
Mimi si mtaaalamu wa coordinates, ila nadhani ulichokibainisha kwenye hoja yako kinamantiki kubwa kuliko kile kilichosemwa kwenye Hotuba ya Waziri Membe. Upo uwezekano kuwa Waziri Membe alipotoshwa kidogo na wataalamu wake wa hotuba. Lakini pamoja na hilo, hoja ya TZ kudai umiliki wa mpaka wake...
Hapana, siri iliyoibuliwa na Mzee Makamba ni kuwa Rais Kikwete hatokuwa na nguvu ya ushawishi ndani ya CCM katika kukichagulia Chama cha Mapinduzi Mgombea wa Urais..!:eek2:
Ni jambo la uungwana kwa Rais aliyepo madarakani kuhudhuria mazishi ya ya Rais mwenzake ambaye amefariki akiwa madarakani. Aidha, tangu lini tumekuwa na tabia ya kuamua nani akamzike nani? Kwa mujibu wa miongozo ya kidini na kimaadili kuwazika wenzio ni jambo la sudi hivyo Kidiplomasia...
Kwa gharama alizotaja Hydrobenga Jr ukilinganisha na gharama ulizoainisha wewe za CT Scans, bado utaona kuwa bado bei ya L/Cruiser Shangingi moja hailingani na CT Scan Mashine. Hivyo kauli kwamba CT Scan ni aghali kwa Shangingi bado ni sahihi. Ingawa kimsingi, bado si sahihi kwa Mawaziri na...
Binafsi, Jaji Werema alipoacha watu wa Zanzibar wajifanyie mambo mbalimbali kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na yeye akajikalia kimya tuu, niliamua kuwa si AG mahiri..! Mamlaka zilizomteua ziutazame upya uteuzi wake. Haitokuwa aibu kumbadilisha mara moja na kumpangia kazi...
Sina hakika na mfumo wa Tanzania wa Operesheni Maalumu. Ila kwingineko Maafisa wa Idara za Usalama hawafanyi Operesheni zao kwa kushirikiana na Polisi. Hivyo, nataka kuamini kuwa hata kwa Tanzania inaweza ni hivyo. Endapo nyuma ya sakata la Dr. Ulimboka kuna mkono wa TISS au Polisi, basi kwa...
Jamani, japokuwa mtoa mada hajaiweka wazi mada yake, lakini uamuzi wa kuanzisha Kiwanda ni lazima ufuate taratibu maalumu kwa mujibu wa sheria. Aidha, ili kuanzisha kiwanda kama cha mbolea ambacho kinatumia aina mbalimbali za kemikali hatari, ni lazima tathmini ya athari za kiwanda hicho kwa...
Kuhusu ajali, Padri Mapunda anasema kuwa 'haya ni matokeo ya kushindwa kwa waliopewa madaraka ya kusimamia maeneo hayo'. Hii ni kweli kabisa, kwa kuongezea, na mimi nasema kuwa hayo ni matokeo pia ya kukosa utaratibu wa kuwajibika pale tatizo linapotokea. Jamani viongozi wetu, kuwajibika...
Hongera Shibuda. Ni kweli ni aibu kwa Bunge la nchi kama Tanzania, tena Bunge la Bajeti kuwa na viti tupu kama ambavyo huonekana katika Luninga. Hawa Waheshimiwa sijui huwa wanakwenda wapi.
Hata kama wanakuwa na dharura za kibinadamu, ukifanya hesabu kitakwimu nagundua kuwa Bunge huwa na...
Honolulu,
hebu tafadhali tuwekee document yoyote inayoonyesha serikali kupewa fedha hizo, au hata picha inayoonyesha Waziri husika au Kiongozi yeyote wa serikali ya Tanzania akipokea fedha, ili na sisi tuanze kuchambua jambo hilo. Vinginevyo, utakuwa umeanzisha mjadala ili tuchangie kama vipofu...
Hongera sana Mheshimiwa.
Tabu ni moja tuu, mazuri mengi unayoyafanya katika utekelezaji wa ahadi zako mara nyingi huwa hayawi 'captured' ipasavyo na Wasaidizi wako na kuwafikia Wananchi kama taarifa. Hujachelewa. Waelekeze waandae jedwali linaloonyesha 'updates' za kile ulichaahidi, wapi na...
'A wise man changes his mind sometimes..'. Endapo Gazeti la Mwananchi kwa sababu yoyote ile iwayo, wamegundua kuwa waliandika habari ambayo haikuwa sahihi, ni uungwana kuomba radhi, hata kama kosa hilo la kibinadamu ni la muda mrefu. Big up Mwananchi..! Mmeonyesha njia, Vyombo vingine vya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.