Padri alishukia Bunge, serikali | Adai nchi inaelekea kubaya

Padre Mapunda ni mwanasiasa. Nilikuwa nikienda Kanisani pale Manzese miaka ya nyuma basi siku ikiwa ni zamu yake kuhubiri inakuwa ni siasa mwanzo hadi mwisho. Hahubiri neno tokana na somo yeye akiingia ni siasa tu.
 
Huyo Padri anawataka Wabunge yeye ni nani kama siyo kuingilia kazi ya Taasisi zingine. Hivi yeye akiambiwa aache tabia ya kula sadaka sa Waumini atajisikiaje?
 
Kuhusu ajali, Padri Mapunda anasema kuwa 'haya ni matokeo ya kushindwa kwa waliopewa madaraka ya kusimamia maeneo hayo'. Hii ni kweli kabisa, kwa kuongezea, na mimi nasema kuwa hayo ni matokeo pia ya kukosa utaratibu wa kuwajibika pale tatizo linapotokea. Jamani viongozi wetu, kuwajibika hakumaanishi kuwa wewe umetenda kosa, bali ni mfumo tuu wa kiungwana wa kukiri mapungufu na kuleta msimamizi mwingine wa kufanya kazi ambayo hukuifanya ipasavyo hadi ikaleta shida au watu wakapoteza maisha. Hivi, kwa ajali ya MV Skagit, haikuwa Sahihi kwa Waziri wa Uchukuzi Tanzania Bara kuwajibika pia? Tangu ajali ya MV Spice Islander, mbona bado vyombo chakavu vimeendelea kutumika kwa safari za Baharini na katika ziwa Victoria + Ziwa Tanganyika? Mbona bado hata Pantoni ivushayo abiria kwenda na kurudi Kigamboni, imeendelea kufanya kazi wakati maboya yakiwa pungufu, yamefungwa na kufuli kwenye 'grili' ilhali mwenye funguo hajulikani alipo? Au anangoja ajali itokee watu wafe? Ili wakati huo ndio afanyeje? Mbona safari hii watu wamekufa na hakuchukua hatua yoyote zaidi ya kukaa kimya? Hivi MV Skagit kutokuwa na hata ofisi pale bandarini DSM haitoshi kumfanya Waziri pamoja na Port Manager wa Bandari na CEO wa Sumatra kuwajibika? Wajiudhuru haraka vinginevyo Wanaharakati wawapeleke Mahakamani.
 
Huyo Padri anawataka Wabunge yeye ni nani kama siyo kuingilia kazi ya Taasisi zingine. Hivi yeye akiambiwa aache tabia ya kula sadaka sa Waumini atajisikiaje?
Amekula shiing' ngapi?..Msikimbie hoja!
Kuongoza waumini ni pamoja na kuhakikisha wanaishi katika uongozi unaofaa wa kidunia!
 
Padre Mapunda ni mwanasiasa. Nilikuwa nikienda Kanisani pale Manzese miaka ya nyuma basi siku ikiwa ni zamu yake kuhubiri inakuwa ni siasa mwanzo hadi mwisho. Hahubiri neno tokana na somo yeye akiingia ni siasa tu.

Halafu mahubiri yake huwa hayana mtiririko. Anashika hiki anaachia kile. Inakuwa taabu kuunganisha dots. Halafu huyu faza huwa hajali muda kabisa,.........ila anachosema ni ukweli
 
Back
Top Bottom