Ndugu wa Ahmed Msangi: Maisha yetu Hatarini; Hemedi Katumiwa!

Siyo hivyo tu, ila Msangi ajue anahesabu siku tu, maana jamaa lazima wammalize tu.
Ukiishi kwa upanga lazima ufe kwa upanga,
na yeye sasa inatakiwa awataje waliomtuma ili afe nao,hata akikaa kimya lazima watammaliza.
 
Rafiki yangu (ana Surname ya Msangi) alienda juzi Muhimbili kwa ajili ya check up ya meno. Dr alipomuuliza Msangi yupi, jamaa yangu akazuga na alipotoka nje hakurudi tena. Leo ameenda kwa advocate kubadili majina.
 
Hapo ndo naiona habari ka ya kupikwa hii

inaweza kuwa kweli mkuu..
nafikiri kuna mpango wa kumuondoa msangi, sasa wanataka kujua kama msangi aliwashirikisha/kuwaeleza nduguze kuwa kuna tukio la namna hilo wanategemea kufanya/wamefanya..
hii itawasaidia kuondoa ushahidi/watu wote wanaofahamu siri hiyo..
 
Sina hakika na mfumo wa Tanzania wa Operesheni Maalumu. Ila kwingineko Maafisa wa Idara za Usalama hawafanyi Operesheni zao kwa kushirikiana na Polisi. Hivyo, nataka kuamini kuwa hata kwa Tanzania inaweza ni hivyo. Endapo nyuma ya sakata la Dr. Ulimboka kuna mkono wa TISS au Polisi, basi kwa vyovyote vile itakuwa ni TISS peke yao au Polisi peke yao. Lakini, pamoja na hayo yote, hivi ni kwa nini Serikali ihusike na jambo la namna hii wakati ambapo tayari Mahakama ilishamzuia Dr. Ulimboka na wenzake kuendelea na Mgomo? Nina hakika kuwa endapo Dr. Ulimboka angetakiwa kudhuliwa na Serikali kazi hiyo isingetekelezwa katika mazingira kama yale tuliyosoma kwenye Vyombo vya Habari. Bila shaka wangemngoja Dr. Ulimboka anywe bia zake kisha wakati anaondoka akiwa kalewa wamsababishie ajali mbaya sana ya gari? Nani angehoji sana tukio la mlevi mmoja kupata ajali mbaya ya gari usiku mrefu kuwa na uhusiano na mkono wa Serikali? Kwa uelewa mdogo nilionao, na sinema nyingi za kijasusi nilizotazama, nachelea kukubali kuwa kuwa kuna mkono wa Serikali. My take: Mgomo wa Madaktari umesababisha maelfu ya Watanzania kupoteza maisha. Hebu pata picha mke wako yuko hospitali akiwa mja mzito na anakufa kutokana na kushindwa kujifungua kwa sababu mtoto amegeuka na hakuna Daktari wa kumfanyia upasuaji! Hivi ukikutana na Dr. Ulimboka anakunywa bia pale Leaders Club wakati unatoka Mortuary kumuhifadhi mkeo na kichanga chako, utamfanyaje? Najua hutomuua, ila utahakikisha kuwa unampiga sana, unamsababishia na yeye maumivu makali kwa kumg'oa meno, unamvuta kucha, kisha unamuacha alivuja damu na kujiondokea zako baada ya kuridhika kuwa cha moto kakiona.! Sasa kwa mtazamo wangu wa kina, hiyo ndio tofauti ya ya Hukumu ya Mwananchi mwenye hasira kali na kazi ya Maafisa wa TISS, Polisi au Serikali. Kama ingekuwa wao, naamini Dr. Ulimboka asingekuwa hai hivi sasa. Sasa jiulize watu waliokufa wakati wa mgomo kutokana na kukosa oxygen (maana nurse hajui afungue kiasi gani ili mgonjwa apumue salama); kukosa operesheni za tumbo, kichwa, viungo nk; ajali na kadhalika. Kati ya hao wote hapakuwa na hata mmoja ambaye jamaa/rafiki zake wenye hasira wangeweza kujichukulia sheria mikononi mwao na kumtafuta Dr. Ulimboka? Haya wana jamvi, mie napita tuu humu jamvini. Asalaam Aleykum.!
 
lazima wawe na mashaka kwa kuwa sifa kubwa ya majasusi if mission not complete you must be killed
 
Mshahara wa dhambi ni mauti,
Masikini tamaa ya kuwa RPC kama baba yakeo
ndo imekuponza.
Haya ona sasa unaishi kwa woga kama kunguru wa Zanzibar,

Hata wanyama tukiwachinja kwa chakula,
tumamshukuru Muumba kwa kutoa uhai wao,
wao wanakufa sisi tunaishi.
Sasa ukiua bin adam mwenzako,
unageuka na kumla nyama yake??

Sikuonei huruma Ahmed Msangi,
ila nakusikitikia sana Kijana Msangi,
umetumiwa kufaniisha uovu nawe ukakubali,
kwa sababu unapenda kutekeleza uovu,
sasa uovu u juu ya mabega yako,
umebandikwa kibaka bei yako imeshuka,
waliokutuma wanaitaka roho yako pia,
Mauti yako ndiyo salama yao.
 
Kwa kuwa Hemed anashutumiwa kuhusika katika sakata la Dr. Ulimboka nashauri angeondolewa kwenye tume ili kuepuka mgongano wa "Kimaslahi".
 
Kamwe Msangi hatapata amani ya kuishi.
Kwanza ana wasiwasi wa kuuawa na serikali kupoteza ushahidi
 
Sina hakika na mfumo wa Tanzania wa Operesheni Maalumu. Ila kwingineko Maafisa wa Idara za Usalama hawafanyi Operesheni zao kwa kushirikiana na Polisi. Hivyo, nataka kuamini kuwa hata kwa Tanzania inaweza ni hivyo. Endapo nyuma ya sakata la Dr. Ulimboka kuna mkono wa TISS au Polisi, basi kwa vyovyote vile itakuwa ni TISS peke yao au Polisi peke yao. Lakini, pamoja na hayo yote, hivi ni kwa nini Serikali ihusike na jambo la namna hii wakati ambapo tayari Mahakama ilishamzuia Dr. Ulimboka na wenzake kuendelea na Mgomo? Nina hakika kuwa endapo Dr. Ulimboka angetakiwa kudhuliwa na Serikali kazi hiyo isingetekelezwa katika mazingira kama yale tuliyosoma kwenye Vyombo vya Habari. Bila shaka wangemngoja Dr. Ulimboka anywe bia zake kisha wakati anaondoka akiwa kalewa wamsababishie ajali mbaya sana ya gari? Nani angehoji sana tukio la mlevi mmoja kupata ajali mbaya ya gari usiku mrefu kuwa na uhusiano na mkono wa Serikali? Kwa uelewa mdogo nilionao, na sinema nyingi za kijasusi nilizotazama, nachelea kukubali kuwa kuwa kuna mkono wa Serikali. My take: Mgomo wa Madaktari umesababisha maelfu ya Watanzania kupoteza maisha. Hebu pata picha mke wako yuko hospitali akiwa mja mzito na anakufa kutokana na kushindwa kujifungua kwa sababu mtoto amegeuka na hakuna Daktari wa kumfanyia upasuaji! Hivi ukikutana na Dr. Ulimboka anakunywa bia pale Leaders Club wakati unatoka Mortuary kumuhifadhi mkeo na kichanga chako, utamfanyaje? Najua hutomuua, ila utahakikisha kuwa unampiga sana, unamsababishia na yeye maumivu makali kwa kumg'oa meno, unamvuta kucha, kisha unamuacha alivuja damu na kujiondokea zako baada ya kuridhika kuwa cha moto kakiona.! Sasa kwa mtazamo wangu wa kina, hiyo ndio tofauti ya ya Hukumu ya Mwananchi mwenye hasira kali na kazi ya Maafisa wa TISS, Polisi au Serikali. Kama ingekuwa wao, naamini Dr. Ulimboka asingekuwa hai hivi sasa. Sasa jiulize watu waliokufa wakati wa mgomo kutokana na kukosa oxygen (maana nurse hajui afungue kiasi gani ili mgonjwa apumue salama); kukosa operesheni za tumbo, kichwa, viungo nk; ajali na kadhalika. Kati ya hao wote hapakuwa na hata mmoja ambaye jamaa/rafiki zake wenye hasira wangeweza kujichukulia sheria mikononi mwao na kumtafuta Dr. Ulimboka? Haya wana jamvi, mie napita tuu humu jamvini. Asalaam Aleykum.!

maelezo yako uliyoyatoa ni ya kitaalamu zaidi kuliko huu usalama wa taifa wa nchi hii unavyofanya. kwanza elewa viongozi wakuu katika idara hii wanaelimu ndogo sana wala usishangae kuona acting hafifu zinazobuniwa na idara hiyo. mauji kadhaa yameshafanyika ndani na nje idara hiyo nani wazi kabisa unajua nani aliyefanya hivyo na kwa sababu gani. kinachofanya uhalifu wa idara hiyo usijulikane kwa sasa ni kwa sababu hakuna tume huru inayoundwa kuchunguza uonevu unaofanywa na hao usalama wa taifa.
 
[/QUOTE]uzoefu wangu wa kusoma tabia za watu kupitia picha inaonyesha ni mtu muungwana.sina shaka huko aliko anajuta kufanya tukio lile na kuwachukia waliomtuma,sitashangaa siku nikisia taarifa kuwa tiss wamemnyamazisha jumla.kwa tanzania yetu tunayoijua lolote linaweza kutokea.
 
Back
Top Bottom