Recent content by Johnkitime Blog

  1. Johnkitime Blog

    MAPENZI BONGO STYLE

    Mapenzi ya Kibongo ni ya aina yake duniani, yaani hakuna pa kulinganisha, hivyo nimeona leo nitoe somo ili kuwasaidia vijana na wazee, wake kwa waume namna ya kuishi kwa furaha katika mapenzi ya Kibongobongo. Pia elimu hii itawasaidia wanaofika Bongo kwa mara ya kwanza, au wale ambao waliondoka...
  2. Johnkitime Blog

    Kiboko ya aliyependa kupiga mkewe

    Kuna wanaume ambao mpaka leo wanadhani, kwa akili zao fupi kuwa kupiga wake zao ndio kuonyesha kuwa wao ndio wanaume wa ukweli. Juzi kati hapa kwetu jamaa mmoja mwenye akili fupi kama hizo, ambaye daima haoni tabu kumshushia mkewe kipondo yalimkuta makubwa maana siku hizi anatembea huku...
  3. Johnkitime Blog

    DJ wa Uswazi ndani ya harusi ya kishua

    Dahh nimeamka kichwa kinagonga, masikio yameziba halafu nimekasirika sana. Na wala sio malaria inayonisumbua, tatizo limetokana na ishu ya kupeana tenda kirafiki bila kupimana ujuzi. Unajua kila kazi ina ujuzi wake, usidhani kwa kuwa kila anaejua kupaka rangi kuta za nyumba ni mchoraji, ukataka...
  4. Johnkitime Blog

    Yule mdada aliyekufa kafufuka

    MKE: Ulilala wapi? Unanidharau sana unanirudia mie alfajiri, leo lazima unambie huko ulikolala MUME: Mke wangu mpenzi jana nilichanganyikiwa, si unamfahaamu rafiki yangu Joshua, basi jana dada'ke kaanguka kafariki ghafla basi nimelazimika kulala huko kumliwaza. MKE: Ok basi ngoja na mie nioge...
  5. Johnkitime Blog

    Mnyalu aliyezaliwa Kwazulu Natal

    Baada ya kuzamia Ulaya jamaa yangu mmoja kutoka Nyanda za juu kusini, kijiji chao kikiwa jirani kabisa na kijiji chetu, hatimae akawa anaishi Uswisi. Lakini maisha yake yalikuwa ya kujifichaficha maana alikuwa hana vibali vya kuishi Uswisi. Washikaji wenzie wakamtonya kuwa dawa kubwa ya kuishi...
  6. Johnkitime Blog

    Usilolijua halitakusumbua

    YAMEMKUTAjamaa yangu wa karibu sana, hana raha kabisaa. Ile methali ya kusema usilolijua halikusumbui, ndugu yangu kaigundua kuwa ni ya kweli. Mimi kwa kweli namuonea huruma. Naomba na wengine mtakayoisikia jifunzeni kutokupekua mambo yaliyopita, au kuuliza maswali magumu unaweza kupata majibu...
  7. Johnkitime Blog

    Hajuna mjinga zaidi

    SI MCHEZO duniani kuna watu. Juzi juzi nilihadithiwa mkasa nikagundua kuwa binadamu tunapishana barabarani lakini akili zetu tofauti. Jirani yangu juzi kanambia alikwenda kwao, si unajua ndugu zetu wengine wakiona dili zinakataa wanarudi kwao kusafisha nyota, sasa alipokuwa huko kusafisha nyota...
  8. Johnkitime Blog

    Wizara ya viwanda na biashara yatayarisha regulations za ulipaji mirabaha, kwa ringtones, radio , tv

    JANA tarehe 13.3.2015 kulikuwa na wadau kukutana na kujadili kanuni za COPYRIGHT AND NEIGHBOURING RIGHTS COMMUNICATION TO THE PUBLIC REGULATION 2015. Katika kanuni hii kunatayarishwa njia rasmi za kisheria za kulipia mirabaha kwa kazi zote za muziki zitakazotumika hadharani ikiwemo matumizi...
  9. Johnkitime Blog

    Familia ya mbaraka yaingia mkataba mpya wa usambazaji

    Tarehe Januari 12, 1979 ndipo siku kiongozi wa Super Volcano, mpiga gitaa na muimbaji maarufu alipopata ajali ya gari katika jiji la Mombasa, ambapo alipoteza maisha yake. Hivyo ni zaidi kidogo ya miaka 36 sasa toka siku hiyo. Katika hali inayothibisha faida za Hakimiliki, familia ya...
  10. Johnkitime Blog

    Nikichaguliwa mkuu wa naninilii, mtaipata

    WE ACHA TU, Kuna vitu najua Mungu anajua akivipitisha kwangu itakuwa shiiidaaaa. Kwa mfano ikitokea nipate zali la mentali, Mkuu akiamua kunichagua kuwa Mkuu wa Wilaya, hapo jueni kabisa ntakuwa vipa umbele vya muda mfupi na muda mrefu. Na hivi vya muda mfupi nitahakikisha kuwa lazima...
  11. Johnkitime Blog

    Je unaitumia Maikrofoni kikamilifu jukwaaani?

    Mara nyingi huwa tunazipata picha za wasanii wetu waimbaji wakiwa wameshika microphone wanaimba au kuchana mistari. Kutokana na wao kuona picha za marapa wengine jinsi wanavyoshika maik nao huiga ushikaji huo. Bahati mbaya sana mara nyingi ushikaji wa maik huwa si sahihi hivyo sauti ambayo...
  12. Johnkitime Blog

    Johnkitime Blog

    Aksante sana
  13. Johnkitime Blog

    Johnkitime Blog

    Hodi humu ndani, sisi ni blog johnkitime yenye habari za muziki, historia ya muziki wa Tanzania na nchi jirani na pia blog yenye habari picha na vichekesho vya kiswahili. Pia tunatoa elimu ya hakimiliki kwa yoyote atakaekuwa na haja ya kufahamu jambo moja au jingine Asante sana
Back
Top Bottom