MAPENZI BONGO STYLE

Mar 4, 2015
13
12
Mapenzi ya Kibongo ni ya aina yake duniani, yaani hakuna pa kulinganisha, hivyo nimeona leo nitoe somo ili kuwasaidia vijana na wazee, wake kwa waume namna ya kuishi kwa furaha katika mapenzi ya Kibongobongo. Pia elimu hii itawasaidia wanaofika Bongo kwa mara ya kwanza, au wale ambao waliondoka Bongo zamani sasa wamerudi tena, au wale ambao wazazi wao ni Wabongo, lakini wazazi walisepa zamani na kuishi nje ya Bongo sasa watoto wameamua kurudi Bongo. Mapenzi ya kibongo yako katika staili mbalimbali, kwa mfano mapenzi ya Kibongo hayashughuliki na mambo madogomadogo kama eti kupeana maua, sijui kadi au eti kutembea beach mmeshikana mikono, hizo ishu ni za kwenye sinema tu za kihindi au labda Ulaya. Hapa Bongo ukimwambia mpenzi wako twende beach, anajua huko lazima kuna mibia na minyama choma, tena mnaweza kwenda beach hata mwaka mzima msiguse maji hata ziku moja, mkifika huko ni mibia tu. Ukipendelea kumpa mpenzi wako maua ujue akiwahadithia wenziewatakucheka na unaweza pewa jina la Bwana Kilimo au mzee wa Nyuki. Wapenzi wa kibongo wa ukweli huwa hawahangaiki kuelezana eti I love you au nakupenda sana , aaa wapi, hayo mambo utayasikia kwenye Bongofleva na Bongomuvi tu, uraiani mambo tofauti sana, mdada akiwa na mapenzi ya ukweli utaona anampikia mpenzi wake msosi wa ukweli, hata kama jamaa hajaacha hata senti tano mdada atahangaika kuzipata kutoka kwa wale asiowapenda, na mara nyingi hawa atawaita bebi, na kuwambia I love you, ili watoe hela apate za kumpikia anaempenda. (By the way ukiambiwa I love you, kaa chonjo ujue we sio yuko mwenyewe). Na mswahili anapokuta msosi wa bure kila siku utasikia anajisifu anavyopendwa, na mdada akiona jamaa anakula sana anajua anapendwa, hawahangaiki kuitana bebi wala nini, hayo ndio mapenzi ya kibongobongo.Ukiwa na mpenzi kama huyo unakaribisha na wenzio waje wale chakula ambacho hujalipia, na wenzio utasikia ‘Aise shemeji anakupenda sana kakupikia chakula kitamu hivi?’.

Katika aina nyingine ya mapenzi ya Kibongo bili zote mwanaume lazima ulipe. Mkiwa mmekaa baa mmeshakula na kunywa sana hata kama mwanaume unaona mdada kaanza kushika pochi kama vile anataka kulipa jua ni geresha tu, anajua unampenda hivyo utalipa tu. Hata wale wadada waliowahi kuishi Ulaya wanajua system ya Bongo ni mwanaume kulipa, wakirudi huku nao wanasisitiza mwanaume lazima alipie kila kitu kama anampenda. Ampangie chumba, anamnunulie nguo chakula, amtoe aout, ampe mkwanja wa kutambia wenzie, huyo ndio naitwa mwanaume, au la utapewa jina Mwanaume Suruali. Halafu kuna dizaini nyingine ya mapenzi ya Kibongo ambapo mdada hata amkute bwana wake na binti mwingine, hata kama wamekaa kihasara anatakiwa kuonyesha mapenzi bila kusita, lazima kufanya kama hajaona na anatakiwa asigusie kama aliwahi kuona chochote. Hii inahakikishia jamaa kuwa kweli anapendwa, lakini marufuku mdada kukutwa amekaa kihasara na bwana mwingine hali ya hewa itabadilika mara moja. Kuna hii staili nyingine ya mapenzi, ambapo ili mpenzi wa Kibongo aonyeshe ana mpenda sana mwenzi wake wivu huwa muhimu, mwanaume haruhusu mwanaume yoyote, hata kama ndugu kumsalimu au kutuma mesej au kuchat kwenye simu, na mpenzi wake, halikadhalika wadada nao hutoa masharti hayohayo, hata kama ni dadako lazima kuweko na utaratibu wa kutumiana mesej. Jambo lingine muhimu katika mapenzi ya Kibongo, mwanaume wa Kibongo marufuku jikoni, kwa sababu mdada anakupenda hata ukirudi saa kumi za usiku na unamkuta ana malaria kali, lazima ajikongoje aingie jikoni. Mwanaume ukikosea tu uanze kuingia jikoni kupika ujue umeanzisha mtindo utakaokukosti akipona atadai uendelee kupika na kuosha vyombo na kadhalika. Kuna hili neno ambalo watu wasio na hela, na ndugu wenye wivu wamelianzisha eti, “Kuchunwa”. Katika mapenzi ya Kibongo hakuna anae chunwa, ni mapenzi tu mtu kuamua kumpa mpenzi wako mshahara wote. Na kiukweli hata mimi nimemuandikisha mchuchu wangu ndio awe anapita kazini kuchukua mshahara, halafu nikifika home tunagawana. Hayo ndio mapenzi ya Kibongo. Kwa wenye maswali tuma hapo chini inbox………
 
Back
Top Bottom