Kiboko ya aliyependa kupiga mkewe

Mar 4, 2015
13
12
Kuna wanaume ambao mpaka leo wanadhani, kwa akili zao fupi kuwa kupiga wake zao ndio kuonyesha kuwa wao ndio wanaume wa ukweli. Juzi kati hapa kwetu jamaa mmoja mwenye akili fupi kama hizo, ambaye daima haoni tabu kumshushia mkewe kipondo yalimkuta makubwa maana siku hizi anatembea huku anachechemea.

Watu wote tulikuwa vyumbani mwetu. Hizi nyumba za kupanga zisizo nadari unasikia kila mtu anafanya nini, kila chumba kimefungua redio au TV ya stesheni tofauti, wengine unasikia wakikoroma wengine wakicheka ndi mambo yetu tena, ghafla tukaanza kusikia vikombe na sahani zikivunjwa, kelele za mambishano makali yakaanza, tukajua jamaa yetu kishalianzisha kwa mkewe kama kawaida. Kisa haswa kilikuwa jamaa katafuta chupi yake haioni.

Taabu ikaanza jamaa kama kawa akaanza kumshushia kipondo mkewe puu,puu,mama wa watu akaanza kulia kwa uchungu, tukaenda kuamulia tukakuta wamejifungia ndani, ikawa tunajaribu kumsihi jamaa toka kwenye korido. Kila tulipogonga kumsihi jamaa afungue mlango, alitujibu ‘Hayawahusu tokeni’ Tukabaki kusikia tu kilichokuwa kikiendelea kule ndani.

MUME: Shenzi wewe (puu) , huna akili(puu,puu,puu) chupi yangu iko wapi, umeshahonga kwa mambwana zako, (puu)….ni wazi mwanamke alikuwa anasindiliwa ngumi nzito.

MKE: Uuuuuuuuuuuuh mume wangu unaniua bure sijui mwenyewe umeweka wapi

MUME: Kufa(puu), kufa shenzi we (puu)

MKE: Baba nisamehe kumbukua mimi mjamzito, muogope Mungu

MUME: Kwanza mimba siyo yangu (puu), Malaya mkubwa (puu).

Ghafla kunatokea kimyaaaaaaa, mke halii wala mume haongei na ngumi zimesimama. Tukajua jamaa kauwa mkewe……dakika chache baadae tukasikia sauti ya ukali

MUME: We Malaya ntakuua, nasema ntakuua………(kimya)

MUME: Nakwambia niache……….(kimya)

MUME: Aise ntakufanya kitu kibaya sana niachie (kimya)

MUME: (Kwa upole) Unajua unaniumiza mwenzio (kimya)

MUME: Aise niache bwana (kimya)

MUME: Malisa mke wangu Please niache, naomba uniache…unajua utaniua kizazi mke wangu,niachie nakuomba. Mama mpenzi naomba niachie..ohhh.

Huku nje tukashangaa vipi leo mtemi anabembeleza? Kuna nini?

MUME: Ndugu zangu nisaidieni mke wangu ananiua,uwiii ananiua ameshika nanihii jamani nisaidieni..

Kwa kuwa mlango ulikuwa umefungwa ilituchukua muda kuuvunja, wakati huo jamaa tumemkuta hoi machozi na jasho vinamtoka kwa pamoja, mke katulia katulia ameminya sehemu nyeti jamaa yetu kawa mpole kuliko mdoli wa kuchezea
 
!
!
Mimi ukimpiga dada yangu uwe na uhakika unaweza kunidhibiti. La sivyo nitakushigulikia mpaka ujute. Ntakudunda mpaka nikuvinje mguu ndio nikuachie.
 
Kama Ningekua Mimi Wala Nisingepata Tabu Ya Kum bembeleza Aachie Mali asili Yangu. Yani Hapo mimi Pia Ningedandia Chakula Cha Mtoto Nikaaza Kubembea Kwa Nguvu. Maana Ukifanya Hivyo Wala Hapachukui Muda Utaona Tu Yeye Mwenyewe Anasalim Amri!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom