Ni bahati mbaya sana kwa kijana wetu Samatta kuwa na tabia ya upole asiyetaka makuu hata yale yanayomstahili. Wanaomfahamu kiundani tangu akiwa mtoto mdogo wataelewa nisemacho. Ni bora kujitokeza na ushauri wa kumjenga kuliko kumponda.
Umenena! Hofu yangu ni kuwa uvumilivu huwa una mwisho. Si vema kuufikisha umma; hata kama ni mtu mmoja; kwenye kilele cha uvumilivu. Au tumesahau yaliyotokea Tunisia yalianzia kwa mtu mmoja tu kujilipua kwa moto kwa hasira ya kuonewa na kunyanyaswa? Tusiifikishe Tanzania yetu huko.
Inawezekana; kama ndiyo CHADEMA walioamuru wachimbaji wadogo wafukiwe walipogoma kuondoka kwenye machimbo yao kupisha wawekezaji kule Kahama ambao leo tunawaita wezi. Kweli naamini nchi hii ina LAANA.
Ni vema Speaker wa Bunge letu Tukufu akatambua kuwa hao anaosema wapo Upinzani na hivo waweza kuathiriwa na hoja ya Mbunge wa Kilombero hawana KINGA. Kama wana makosa, ni juu ya vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua stahiki. Hawawezi kulindwa ili kuwalinda viongozi walio na kinga...
Tofauti iliyopo ni kuwa Gadaffi hakuwa part and.parcel ktk mkataba wa awali. Hivo siyo sahihi kulinganisha. Waliotufikisha hapa waungame kwanza kuwa walilikosea Taifa na isiwe ni ngonjera tu za kisiasa kwa malengo ya kisiasa.
Mapendekezo yamekuwa yakiimbwa tangu miaka ya tisini. Sasa ni "mapendekezo" gani tena unataka yatolewe? Kupinga sheria kupitishwa kwa hati za dharura siyo "mapendekezo"? Tutumie mbongo na si ushabiki ktk kujadili masuala.
Asiyepata bahati ya kuishi na mtoto wake akiwa na umri wa miaka kuanzia 2 hadi 4 atakuwa amekosa uhondo wa kupindukia. Ndiyo kipindi kizuri cha kufurahia ubunifu wa mtoto aliyeanza kuongea kabla hajaanza utundu wa shuleni. Ni kipindi cha faraja ya ajabu kushuhudia ubunifu wa kiasili wa binadamu...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.