Inanishangaza kuwa watendaji hawakumshauri Rais wetu kutuma salamu za rambirambi, au hata kulisemea tu kwa wazi, kwa msiba huu uliolipata jiji la Dar es Salaam.
Tutumai na kuomba aishie hapo. Wasiwasi wangu kuwa wasije wakatushauri oia tutumie mahabara na vipimo vya waganga wa asili.
Wakati tunatumia madawa hayo tujiandae pia kwa madhara yake ya muda mrefu.
Hakika utamaduni unadumu hata ukibafilika vipi!
Ukiingia kwenye siasa unajifunza kuwa laghai hata kama wewe ni mwanasayansi inaikataa sayansi! Mbaya unawafanya watu wote ni wajinga na kwamba wewe tu ndiyo mwerevu
Angefanya hivyo mapema na kwa kufuata taratibu ingeeleweka. Kubambikiwa kesi ni halisi na wanaofanya hayo wanashirikiana na ofisi yake au na 'yeye mwenyewe'
Tunanunua ugomvi ambao tunajua hatuwezi kushinda. Yesu alisema mfalme anayetaka kwenda vitani hufanya hesabu kwanza ya uwezo wa jeshi la adui. Akiona lina uwezo kumzidi hufanya majadiliano kabla ya kuingia vitani. Hii ndiyo hekima!
Sisi tunayoyaona huku mitaani hayahakisi hayo maoni yake. Labda ana wapiga kura wengine nje ya wananchi tunaoishi nao na wamaoudhuria mikutano ya wagombea!
Yawezekana mkawa na uhalali wa kisheria lakini bado mkawa bandia! Kwa miaka zaidi ya 25 bado hamjapata mbunge hata mmoja wala madiwani mnapata wapi uhalali wa kisiasa kama siyo kutumika tu!
Dr Mahera usisahau kuwa wewe ni refa na mwamuzi. Wewe siyo kuwasemea wapiga kura wanachokitaka au siyo wewe unayeshauri vyama vya siasa viwe na sera zipi?
Huyu naye vipi? Yaani TBC wanasubiri kualikwa! Mara ya mwisho nilifikiri TBC ni chombo cha habari, tena cha umma na kina waandishi wa habari wanaotakiwa kutafuta taarifa na kutuletea sisi wananchi tunaowalipa. Kumbe wanasubiri kualikwa ili waende 'harusini' 🤔
Sidhani kwamba ni tatizo la vyama vya siasa kutojipanga Mh Dr Mahera. Najua umetumia maneno hayo ili kuwalinda hao wasimamizi. Tume fikirieni hao wasimamizi ikiwa bado wana uhalali wa kusimamia maeneo hayo. Sijui kama vyama husika na wapiga kura wake winawaona kwamba hawana upande - yaani impartial
Nafikiri kwa kulinda na kujali uhai wa kila mmoja wetu siyo lazima tusubiri ndugu wa marehemu. Ni wajibu wetu na serikali kuhakikisha uhai wa kila mmoja wetu unahifadhiwa na kulindwa. Kumbuka kuna watu wako mjini hawana hao ndugu wa kuwasemea kwa mara moja. Wanaweza kufa isijulikane, lakini...
Ingekuwa vyema kama mauaji hayo yangekuwa yanachunguzwa kwa mujibu wa sheria ya vifo tatanishi. Kuna uwezrkano kwa watu wema kuuuawa. Ni vizuri pia kupatikana ukweli wa mauaji yoyote ya binadamu. Haya yatatuwezesha kuongeza ufanisi katika utendaji wa polisi na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.