Dar es Salaam: Polisi waua majambazi wanne na kufanikiwa kukamata silaha mbalimbali

Hakuna cha uchunguzi, polisi wanawafahamu akina Nuru ukimpleka mahakamani anakaa miezi minne rumande kesi inatupwa hakuna ushahidi anarudi mtaani kuwasumbua raia.
Hapana ndugu, kuna watu wamewahi kuuawa halafu tukaambiwa ni majambazi kumbe majambazi ni polisi walioua ili wapole mali. Wengi wamesingiziwa hizi tuhuma na kuuawa. Polisi hawa na matendo wanayoyafanya hawaaminiki.
Ndio maana kuna jamaa hapa mwenge dsm aliwahi kukimbilia kwa wanajeshi baada ya kutofautiana na polisi. Yaani bora kukimbilia kwa JWTZ kuliko polisi wakupeleke sehemu ambapo hawaonekani na jamii.
Ukikamatwa na polisi hakikisha hautoki kwenye macho ya jamii la sivyo tutaletewa kwamba ulikuwa unakimbia wakakupiga risasi bahati mbaya ukafa au ulikuwa unashambulia kwa risasi ukafa.
I have bad experience with polisi
 
Hizi taarifa za polisi za kuua majambazi siku hizi siziamini tena, na wala msiwe mnaziamini kirahisi. Polisi wetu ni wauaji makatili wa kuogopwa zaidi ya ukoma. Ukweli siwaamini Polisi wetu hata kidogo. Mara nyingine wanaua watu wanasingizia majambazi. Wanazo silaha tele huko vituoni na maganda ya risasi, wanayaweka eneo walilotupa maiti za watu waliowaua halafu wanasema majambazi wameuwawa katika mapambano makali!

Mara ngapi umesikia kuwa polisi ameuwawa katika haya mapambano makali? Ikiwa Kigoma wananchi waliweza kuua polisi wawili kwa silaha za jadi katika mpambano kati ya polisi na wananchi, iweje siku zote majambazi walio na silaha za moto wanashindwa kuua angalau polisi mmoja, au hata kujeruhi askari kwa risasi? Kwamba hao majambazi wanaambiwa nyie pigeni risasi hewani wakati sisi tukiwatwanga risasi?

Tatizo Tanzania hatuna chombo cha kuchunguza taarifa hizi magumeshi. Wanalosema polisi ndio kauli ya mwisho. Ndio, polisi wanasaidia usalama wa raia kwa kiasi fulani, lakini watu wa ovyo sana hawa hapa nchini. NI polisi wachache sana walio waaminifu, na wapo ambao wanachukizwa sana na haya matendo maovu ya wenzao.

Tatizo Tanzania wengi wetu ni malofa wa kudanganywa kirahisi sana na kumeza tu uongo tunaopewa. I hate these liars.
Bahati mbaya wakishauawa hawawezi kuelezea upande wao wa kilichotokea! Mimi si muumini hata wa hukumu ya kifo sembuse mauaji ya mtu mwingine yeyote.
 
Hapana ndugu, kuna watu wamewahi kuuawa halafu tukaambiwa ni majambazi kumbe majambazi ni polisi walioua ili wapole mali. Wengi wamesingiziwa hizi tuhuma na kuuawa. Polisi hawa na matendo wanayoyafanya hawaaminiki.
Ndio maana kuna jamaa hapa mwenge dsm aliwahi kukimbilia kwa wanajeshi baada ya kutofautiana na polisi. Yaani bora kukimbilia kwa JWTZ kuliko polisi wakupeleke sehemu ambapo hawaonekani na jamii.
Ukikamatwa na polisi hakikisha hautoki kwenye macho ya jamii la sivyo tutaletewa kwamba ulikuwa unakimbia wakakupiga risasi bahati mbaya ukafa au ulikuwa unashambulia kwa risasi ukafa.
I have bad experience with polisi
Enzi hizo jambazi unaweza ukawa raia mwema, raia mwema kuwa jambazi.Awamu hii jambazi ni jambazi fuatilia kwa makini wote ambao polisi inasemaga waliodondoshwa kwenye majibizano ya risasi kama hawana rekodi ya kwenda ndani kwa makosa ya mitutu.
 
Unakamatwa unapelekwa sero unadundwa hadi unakufa..wanachukua mwili wako wanaunganisha na wafu wengine wanasema ni majambazi
 
Enzi hizo jambazi unaweza ukawa raia mwema, raia mwema kuwa jambazi.Awamu hii jambazi ni jambazi fuatilia kwa makini wote ambao polisi inasemaga waliodondoshwa kwenye majibizano ya risasi kama hawana rekodi ya kwenda ndani kwa makosa ya mitutu.
Mkuu itakuwa hauwajui hawa watu wanaitwa polisi. Hawa hawashindwi jambo hasa katika kipindi wakikufanyia ubaya wanapandishwa cheo. Hakuna wa kuwauliza, yaani hapa hata mkikosana kidogo utajuta iwapo utabaki hai.
Siwapendi polisi hata kidogo, na hata nikikutana naye njiani hapo anashida nampita
 
Enzi hizo jambazi unaweza ukawa raia mwema, raia mwema kuwa jambazi.Awamu hii jambazi ni jambazi fuatilia kwa makini wote ambao polisi inasemaga waliodondoshwa kwenye majibizano ya risasi kama hawana rekodi ya kwenda ndani kwa makosa ya mitutu.
Ingekuwa vyema kama mauaji hayo yangekuwa yanachunguzwa kwa mujibu wa sheria ya vifo tatanishi. Kuna uwezrkano kwa watu wema kuuuawa. Ni vizuri pia kupatikana ukweli wa mauaji yoyote ya binadamu. Haya yatatuwezesha kuongeza ufanisi katika utendaji wa polisi na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
 
safi sana,
kwani dawa ya moto ni moto,
tena kipindi hiki jeshi letu linapaswa kuwa macho sana na vitendo vya uhalifu, patrol inahitajika sana ktk kipindi hiki cha uchaguzi, vitendo vya uhalifu vitakithiri sn
 
Ingekuwa vyema kama mauaji hayo yangekuwa yanachunguzwa kwa mujibu wa sheria ya vifo tatanishi. Kuna uwezrkano kwa watu wema kuuuawa. Ni vizuri pia kupatikana ukweli wa mauaji yoyote ya binadamu. Haya yatatuwezesha kuongeza ufanisi katika utendaji wa polisi na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Ndugu kama Baba,mama,wake zao wanaruhusiwa kupeleka malalamiko kwa mujibu wa sheria.Unakumbuka yaliyomkuta Zombe na Bageni?hiyo ni baada ya ndugu kutoa malalamiko kuwa walikuwa wauza madini ni siyo majambazi.Kuna somo askari walijifunza kupitia lile tukio.
 
Nafikiri kwa kulinda na kujali uhai wa kila mmoja wetu siyo lazima tusubiri ndugu wa marehemu. Ni wajibu wetu na serikali kuhakikisha uhai wa kila mmoja wetu unahifadhiwa na kulindwa. Kumbuka kuna watu wako mjini hawana hao ndugu wa kuwasemea kwa mara moja. Wanaweza kufa isijulikane, lakini tunao wajibu wa kulinda maisha yao. Ya akina Zombe ilikuwa siyo ndugu tu bali hata kelele za watu vikiwemo vyombo bya habari vilisaidia...na ilikuwa mwanzo kabisa wa serikali ya awamu ya nne.
 
Sasa mbona Nuru naye wamemuua wakati ndie aliyewapeleka kuwaona wengine, maana yake walikuwa naye kwenye gari au alikuwa chini ya ulinzi wao
Alikufa kwenye zoezi la kuwanyang'anya silaha majambazi, yeye ni casualty of war against robbery.
 
Ingekuwa vyema kama mauaji hayo yangekuwa yanachunguzwa kwa mujibu wa sheria ya vifo tatanishi. Kuna uwezrkano kwa watu wema kuuuawa. Ni vizuri pia kupatikana ukweli wa mauaji yoyote ya binadamu. Haya yatatuwezesha kuongeza ufanisi katika utendaji wa polisi na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Bora mheshimiwa flan yeye alitajwa kumiliki zaidi ya gani 10 akizitumia kutafuta kitoweo mbugani. At least huyu hakuhatarisha maisha ya citzens. Mheshimiwa tuko pa1
 
Nafikiri kwa kulinda na kujali uhai wa kila mmoja wetu siyo lazima tusubiri ndugu wa marehemu. Ni wajibu wetu na serikali kuhakikisha uhai wa kila mmoja wetu unahifadhiwa na kulindwa. Kumbuka kuna watu wako mjini hawana hao ndugu wa kuwasemea kwa mara moja. Wanaweza kufa isijulikane, lakini tunao wajibu wa kulinda maisha yao. Ya akina Zombe ilikuwa siyo ndugu tu bali hata kelele za watu vikiwemo vyombo bya habari vilisaidia...na ilikuwa mwanzo kabisa wa serikali ya awamu ya nne.
Mzee inaelekea bado huwajui majambazi
Achana kabisa na jambazi kwanza Ana mipango
Mingi connection ya kutosha..... Ndomana polisi wanaamuwa kuwaua Maana ni ngumu ku deal nao

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom