Nina uzoefu wa kufanya malipo ya nje kupitia bank moja (nilikua nafanya online banking).
Baada ya kuwa nimeambatanisha nyaraka, siku ya kwanza huonesha status ya "warehouse" na siku ya pili jioni ndo status hubalika kuonesha pesa imetoka.
Siku ya tatu napakua swift yangu natuma kwa mpokeaji.
Pole sana.
Inaonesha hauna ndugu wa tumbo moja. Hii inanipa taswira tofauti juu ya uhusiano wako na wazazi. Pengine (utaniwia radhi) walikuasili kutokana na wao kutokuweza kupata mtoto (jaribu kuchunguza).
Yote kwa yote, jitahidi kuwatendea wema wazazi wako hata ikiwa hawataki.
Mimi sio mjuzi sana wa hii kada Ila jitahidi sifa hizi unazo orodhesha ndio hizo hizo watu wako wa karibu wanaweza kuzisema kuhusu wewe.
Jitahidi watu wako wa karibu wajue taarifa zako muhimu kuhusu wewe, marafiki zako waweze kusema mazuri kuhusu wewe, marafiki wa wazazi wako waweze kutoa...
Bwana muhasibu inabidi aombe radhi na kusema Yanga waoneshe kwenye makabrasha yao
DR: Intangible Asset ... TZS 400mil
CR: Revaluation gain... TZS 400mil (to the maximum of transfer right and cost incurred to acquire transfer right of/to sign Aziz Ki).
Mkishacheza game la nyoka tu, jiandae kutafuta kazi nyingine. Atakuja kukubebesha jumba bovu hutakuja kuamini zaidi ya kujipamoyo hajaondoka nayo imebaki vile vile.
Hakuna umuhimu wa kufanya hivyo. Kinachotakiwa ni heshima kuwepo baina ya mume/mke na wakwe zake.
Heshima ikiwepo, malalamiko na migogoro ya ndoa itatatulika kwa heshima na nidhamu. Kuheshimiana kwa pande zote mbili ni bora zaidi ya kuwateka wakwe (aidha juu ya umasikini wao, tamaa ya vitu...
Tatizo unapenda wanawake wenye muonekano mzuri (kimavazi na vitu wanavyo tumia). Ili uachanae na tabia ya kuruka ruka ni vyema utafute mwanamke wa daraja la kuendana na uwezo wako.
Ukipata ambae anavyaa vitenge, vijora, anasuka kawaida na hapendi kwenda na wakati sana unaweza akatulia na wewe...
Ikiwa unamaanisha kutokuonekana kwenye taskbar, inawezekana.
Kama unatumia window 10 jaribu hivi:
Setting app > personalization > taskbar > select which icons appear on the taskbar > kisha turn off icons ambayo hutaki ionekane.
Kama sio hicho ulicho maanisha, wajuzi watakuja kukusaidia.
Kichwa cha habari kizuri ila yaliyomo yanaukakasi sababu ya mbinu ya kukusanya taarifa juu ya ulicho kisema.
Mathalani, ungenyambulisha katika kundi la wanaume 50 kuna warefu wangapi na wafupi wangapi.
Mfano: Ikiwa 80% ni warefu, hawa watasema urefu unashabihiana kuficha kuonekana wana ukubwa...
Watazania wengi wanasoma vitu kwa kuangalia urahisi wa kuajirika na sio nini mtu anahamasa nacho na uwezo wa kufanya zaidi. Na hii ndio inaumiza wasomi wengi.
Elimu kubwa ila ufanisi ni mdogo sababu ya dhana ya elimu-ajira-maisha bora
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.