Unatumia njia gani kuwateka ukweni kwako

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Ndio, kuwateka namaanisha wawe upande wako...wakukubali kuwa kweli wewe nimtu sahihi kwa mtoto wao.

Mara nyingi wanawake wanawateka mama mkwe zao hasa kwa vitenge, kanga na vijizawadi vingine vya hapa na pale. Yaani pamoja nakwamba nivitu vya kiupendo Ila vinaplay nafasi ya rushwa flani hivi.

Mwanaume ambaye mkewe kamteka mamamkwe hana ujanja wakumtesa ama kumwacha huyo mwanamke. Labda mwanamke mwenyewe ndo azingue. Utakuta mama anamtetea mkwe wake hadi kufikia hatua ya kutoa vitisho kuwa hataki kusikia kijana analeta mke mwingine zaidi ya huyo wanaye mfahamu.

Kwa wanaume wao huwa wanateka nyumba nzima ya ukweni. Yaani kuanzia wazazi hadi mashemeji.
Mwanamke utaanzaje kumletea mumeo zakuleta. Familia yenu yote itakuona mwehu usiye faa.Hapa napo labda mwanaume ndo awe na mambo yasiyovumilika.

Hali hii wakati mwingine inasababisha wanandoa kuteseka kwani unakuta Yule anyenyanyasika akipeleka malalamiko kwao anaonekana ni mwongo na pengine yeye ndo mbaya.

Kumbuka pande hizi mbili sio lazima kutekwa kwa zawadi na mali zingine,nooo....! wengine wana uwezo mzuri kiuchumi'hivyo hawaoni jipya kwenye vitu vyako. Wengine wanahitaji tu mawazo na akili yako yakimaisha basi ndo unakuwa umewateka hivyo.

Je, kuna umuhimu wakuwateka wakwe zako ili wawe upande wako in case Kuna matatizo ndani ya ndoa?

Wasalaam!
 
Seat ya mbele kabisa upande wa dereva kushoto..maada nzuri umeiweka vzr Sana nasubir maoni ya wadau ila kubwa kabisa wote tunajua NI tutafuteni hela
 
Ndio, kuwateka namaanisha wawe upande wako...wakukubali kuwa kweli wewe nimtu sahihi kwa mtoto wao.

Mara nyingi wanawake wanawateka mama mkwe zao hasa kwa vitenge, kanga na vijizawadi vingine vya hapa na pale. Yaani pamoja nakwamba nivitu vya kiupendo Ila vinaplay nafasi ya rushwa flani hivi.

Uwateke ukweni ili wakupe mke mwingne au!???

Wewe jitume tafuta hela familia yako ile vizuri, iishi nyumba nzuri, watoto wasome shule zenye ubora... Hili ndio jukumu kuu la msingi kwa sisi wanaume,

mengneyo kwa ukweni yabaki kama msaada endapo ukiombwa kusaidia,,, ENDAPO UKIOMBWA KUSAIDIA
 
Tafuta noah nyeusi weka namba za Singapore zama pale wapakize wote peleka mbuga ya wanyama wale bata na wakati wa kurudi wapitishe mjini kwenye duka la maana wajichagulie kila mmoja akipendecho.
Fanya hivi mara moja kwa mwaka
 
Je, kuna umuhimu wakuwateka wakwe zako ili wawe upande wako in case Kuna matatizo ndani ya ndoa?
Hakuna umuhimu wa kufanya hivyo. Kinachotakiwa ni heshima kuwepo baina ya mume/mke na wakwe zake.

Heshima ikiwepo, malalamiko na migogoro ya ndoa itatatulika kwa heshima na nidhamu. Kuheshimiana kwa pande zote mbili ni bora zaidi ya kuwateka wakwe (aidha juu ya umasikini wao, tamaa ya vitu, njaa, mali na kupenda sifa) hii itasaidia sana.

Kwa maisha ya sasa wanandoa wengi hawaelezi chanzo / matatizo halisi ya ndoa zao, pale wanapotofautiana au kugombana, bali wanatafuta huruma na namna ya kuonekana wema katika ndoa zao pale ambapo wataamua kutoa migogoro yao nje ya ndoa.

Kuwepo kwa heshima ni rahisi kwa chanzo cha migogoro/matatizo ya ndoa kuwekwa wazi na kutatulika ukilinganisha na kukiwa na pande moja inayopendwa na kuonekana iko sahihi muda wote (kuteka wakwe), hii itapelekea kibri na jeuri kwa mume na mwisho wa siku migogoro itaongezeka bila kutatulika (pia husababisha vipigo, vitendo viovu waziwazi, kudharauliana, nakadhalika..).

Mwanaume jenga heshima ukweni kila kitu kitaenda kwa mpangilio sahihi, ila kuwateke wakwe itakupa kiburi, jeuri and dharau kwa mkeo na hata wakwe na ndugu wote.
 
Fanya yako na mtunze sister na wajomba zangu wakue vizuri

Maana Shemu sikufichi hizo hela unazonipa na zawadi unazo mpa mother ukiondoka huku nyuma tunakusema unanuka miguu halafu tunacheka
 
Tafuta noah nyeusi weka namba za Singapore zama pale wapakize wote peleka mbuga ya wanyama wale bata na wakati wa kurudi wapitishe mjini kwenye duka la maana wajichagulie kila mmoja akipendecho.
Fanya hivi mara moja kwa mwaka
Ufanye kila siku lakini
 
Back
Top Bottom