Haiwezekani tuwe na Kiongozi wa nchi asiyejua kiini cha matatizo yanayowasibu 'watu wake'. Amefanya juhudi gani kutafiti hata aje na majibu marahisi rahisi kwa tatizo gumu. Laikini hata pale alipodai bila kulazimishwa na mtu kuwa anawajua wauza madawa ya kulevya, ni hatua gani aliwachukulia...
Mimi nadhani haya pia ni maendeleo. Kumbuka Chama anachokiwakilisha kinaitwa Chama cha demokrasia na maendeleo. Huwezi kuleta maendeleo katika nchi au halmashauri isiyozingatia demokrasia. Arusha imelalamikiwa kuweka meya bila kuzingatia sheria au demokrasia. Unadhani haikuhitajika kupigania...
Hawa wanaomsifu Mnyika kwa nini hawakuwahi kumsifia aliposema "tumefika hapa kwa udhaifu wa Raisi Kikwete..."? Ni wachonganishi au Wanafiki? Mtanzania wa kule Liwale anahitaji msomi au mtu atakayemtetea alipwe mazao yake kwa bei iliyo kwenye makubaliano? Kama Mnyika ni mfano mzuri wa Viongozi...
Kwenye nchi hii kukamatwa hakutegemei mtu kuwa na kosa la jinai. Kama ni hivyo Kamanda Kamuhanda angekuwa amekamatwa kwa kuwa tume ya haki za binadamu ilimuona amehusika katika mauaji ya Mwangosi. Akili ya kawaida inaweza kukutuma kuamini kuwa kushinda kwake ubunge na kauuli zake za hivi...
Pengine sababu ni kwa kuwa alisema anao ushahidi kuwa Raisi anaunga mkono vikundi vinavyochochea udini. Unadhani hilo limemfurahisha mkuu wa nchi na wasaidizi wake?
Nani anapenda mijadala hii iendelee na kwa manufaa ya nani. Hoja ni kuwa ipo tuhuma dhidi ya baadhi ya watendaji wa chombo hiki ambayo haipaswi kupuuzwa. Kuipuuza ni kukubali kuwa haki ya watu fulani kuishi itatawaliwa na utashi wa chombo hiki na hakuna anayepaswa kuhoji. Mwenye wajibu wa...
Jambo ambalo hawalisemi waziwazi ni kuwa je inawakera wanapoona vitendo hivi vya watu kung'olewa kucha, meno na macho? Hata kama wanaong'olewa si Dr. Slaa wala Mbowe hao waliotendewa hayo walistahili kutendewa? Kwa nini ikiwa wanakerwa na vitendo hivi hawajamuhoji Ulimboka awasaidie kutambua...
Ni ukweli ulio wazi kuwa Jeshi la polisi Tanzania limepoteza umakini na uhalali wa kushughulikia kadhia hii ya Rwakatare na wenzake kwa kuwa zipo kadhia nyingi zenye ushahidi wa kujitolea amabzo hawajazishughulikia wala kuzitolea maelezo yaliyosimama hadi leo. Sijui kuwa huu ni ujeuri wa Saidi...
Usije shangaa hili likaipatia umaarufu Chadema. Naanza kuiona kama ni movie iliyopangwa kila upande ukitaka kumwingiza mwingine matatani. Wasipocheza vizuri CCM watajikuta wamenasa kwenye mtego wa Chadema. Nani alijua Lema angerudishiwa ubunge baada ya kuvuliwa na mahakama? Katika mazingira haya...
Pengine kabla ya kuwalaumu Watanzania kijumla jumla ungejihoji wamefikiaje hatua hiyo ya kutoona tija ya hatua zinazochukuliwa na polisi. Polisi wamewafikisha watanzania hapo. Hawajafanya lolote juu ya tuhuma za waliomtesa Ulimboka zilizotolewa na Mwana Halisi, wala hawajui kinachoendelea juu ya...
Sijui lengo la hoja yako ni kumlaumu huyu mwalimu unayemtuhumu kuwa ni mjinga au unamlaumu aliyempa mwalimu mjinga jukumu la kuondoa ujinga. Kama kuna uwezekano wa mwalimu mjinga kupata ajira hapo tatizo si la mwalimu hasa bali ni la mwajiri. Na tatizo la mwajiri linaweza kuwa na yeye ni mjinga...
Hoja yako imesimama. Mtu anahitaji akili ya mwendawazimu kukanusha hali ya kukatisha tamaa uliyoielezea. CCM inaweza kuzinduka usingizini kwa kufanya maamuzi magumu ili kionekane kinajali maslahi ya wanyonge. Wasingekuwa wanakwenda mbele na kurudi nyuma katika mkakati waliousanifu wenyewe wa...
Hakuna mapambano yasiyo na mkakati. Makamanda wa mikakati ya CHADEMA wapo CHADEMA hawawezi kutokea CCM. Hao wanaojinadi hapa kama washauri wa kile ambacho Viongozi wa CHADEMA wangefanya ili kufanikisha mapambano yao na hali hawaitakii jema CHADEMA wanawahadaa watu. Kama wana huo uwezo kama...
Nyerere alifanya makosa mengi kama binadamu, makosa ambayo hata leo yangali yakifanywa na viongozi walioko madarakani. Moja ya makosa hayo ambayo wakati huo yalionekana kuwa na maana nzuri ni kung'oa reli ya Mtwara - Nachingwea. Reli hiyo ingeachwa ingeweza kuwa kichocheo kikuu cha maendeleo ya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.