Ifike hatua wabongo tuwe wastaarabu pia, sasa unang'oa koki ili kiwe nini ndo maana watu wakaona suluhisho ni kuweka kamera, ukishindwa kujiheshimu hakuna ambaye atakuheshimu.
Kwa majibu ambayo mtoa mada aliyapata kwenye thread yake ya awali, sikutarajia kama angeandika uzi unaofanana na wa awali.
Kwa umri huo hata uende mahakama kuu, watasikiliza tu halafu waendelee na mengine. Huwezi pata chochote,maana haingii akilini udai mali ambazo sio zako. Ukizingatia mwenye...
Nilikuwa najiuliza sana hili swali, kwa nini wenye elimu ndogo wanakuwa na roho mbaya.
Kuna mmoja mpaka kesho na certificate yake ana kinyongo na mimi, kwa vile nilikabidhiwa ofisi pindi Boss yuko likizo.Heshima kwa wafanyakazi wote wenye elimu kuanzia Degree na kuendelea.
Kwa hiyo mkuu nawe ulikuwa unaamini ni fedha za ndani. Na huku wakizunguka kwenye makorido ya benki ya dunia, shirika ka fedha duniani kukopa fedha za miradi.
Huyu jamaa alikuwa bonge la mtangazaji, hususani enzi zile yuko RFA.
Japo umauti umemkuta akifanya kazi Clouds, na siku za usoni alikuwa hasikiki kwenye kile kipindi cha Power Breakfast.
Hakika sisi sote ni wa mwenyezimungu na kwake tutarejea.
Kiongozi mbona kauli ya rais Samia Suluhu iko wazi. Uwepo wa mabango tafsiri yake ni kwamba wateule wake hawawajibiki.
Kwa mantiki ya kwamba viongozi wa ngazi za chini wapige kazi kutatua kero za wananchi. Ndo maana akasema kila bango litaondoka na mtu/kiongozi.
Kama vinahatarisha usalama wa raia na mali zao bora visimamishwe kusubiri marekebisho. Kufumbia uozo wa vivuko ni kuweka maisha ya watu rehani.
Ila naibu waziri asitoe tu zile kauli alizowahi kutoa kiongozi mmoja pale Dar ferry kwenda kigamboni. Anayeona nauli ya kivuko ni kubwa apige mbizi.
Duh mkuu kumbe siku hizi hiyo ruti ndo ina ujinga huo wa kurudi tena Ubungo utokapo mawasiliano.
Mara ya mwisho kupanda hizo gari ilikuwa ukitoka simu 2000, unaingia barabara ya shekilango/Sinza -mlimani city na kuelekea Kawe/Makumbusho.
Kijana pole sana kwa hiyo changamoto unayopitia.Ushauri wangu ni kwamba wawe usijishtukie uonapo watu wanacheka.
Kwa vile bado uko shuleni soma sana na ipo siku hao wanaokucheka watakuja kukupigia magoti kukuomba msaada. Mwisho tambua tu kuwa mungu kamuumba kila mtu kwa mfanowe.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.