Manyara: Baba mbaroni kwa kuwabaka binti zake watatu

Polisi wanamshikilia baba mwenye miaka 57 mkazi wa Kijiji cha Ndaleta mkoani Manyara kwa tuhuma za kuwabaka binti zake watatu wenye miaka 15, 17 na 18. Wizara ya Maendeleo ya Jamii imesema watoto hao tayari wamepatiwa matibabu na wanaendelea kupatiwa msaada wa kisaikolojia.

---
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 57, mkoani Manyara Kaskazini mwa Tanzania anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa tuhuma za kuwabaka watoto wake watatu wa kike alhamisi ya juma lililopita.

Akitoa taarifa jijini Dodoma mapema leo, Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Prudence Constantine amesema kuwa baba huyo anadaiwa kuwafanyia tendo hilo la kikatili mabinti zake hao wenye umri wa miaka 15, 17 na 18 katika Kijiji cha Ndaleta, wilaya ya Kiteto.

Constantine alisema kuwa wizara imesikitishwa na taarifa za tukio hilo na inapenda kutoa taarifa kuwa tayari mtuhumiwa yupo mikononi mwa polisi kwa taratibu zaidi za kisheria.

Aidha, amesema kuwa watoto wameshapatiwa huduma za kiafya na wanaendelea kupatiwa huduma za msaada wa kisaikolojia na kijamii.

Mkuu huyo alisema kuwa hivi karibuni kwenye jamii kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili kwenye makundi yote ya jamii ikiwemo watoto.

Hivyo alisema kuwa Wizara inawaomba wananchi kuungana kupinga ukatili wa makundi yote kwa ujumla wake na kutoa taarifa mapema kwenye vyombo vya serikali na vyombo vya kijamii vinavyoweza kutoa msaada wa haraka pale tukio linapotokea.

Chanzo: BBC
Disgusting
 
Hizi habari huwa ni za ukweli au ni abrakadabra tu? Yaani baba abake watoto wake wa kuwazaa haingii akilini. Kwanza hao mabinti ki umri ni wakubwa kuweza kumkatalia baba yao na kumkimbia wasibakwe. Labda huyo baba akili zake haziko sawa kiasi cha kutokuona aibu ya kubaka wanawe wa kuzaa na hana maadili ya dini

Pale unapojidai unaishi Geneva Na hujui yanayoendelea mazense
 
Hizi habari huwa ni za ukweli au ni abrakadabra tu? Yaani baba abake watoto wake wa kuwazaa haingii akilini. Kwanza hao mabinti ki umri ni wakubwa kuweza kumkatalia baba yao na kumkimbia wasibakwe. Labda huyo baba akili zake haziko sawa kiasi cha kutokuona aibu ya kubaka wanawe wa kuzaa na hana maadili ya dini
Lazima itakuwa inahusiana na ushirikina
 
Samahani madam .
Is that you ktk dp!?
Una tatizo kubwa Sana kisaikolojia kuhusu unyanyasaji wa kingono kwa wanawake, comments zako kwwnye mada Kama hizi huwa hazifurahishi, wacha nikuongeze kwenye ignore list
Wako mtiifu,
Snap J
 
Anawaita mmoja baadae mwingine hivyohivyo labda anaweza mwambia mkwe wake wanamazungumzo ya kifamilia, anawatoto wa kike wanne, mmoja tu ndio alikataa kufanya upuuzi wao, wengine waliobaki wanaendelea na ujinga wao
Dah!....hii inatisha...huyo mzee na hao watoto wote wana ugonjwa wa akili.
 
Kuna kipindi niliishi kwa aunt yangu kukawa na mgogoro baina ya aunt na uncle, Aunt akaanza kumpanga mtoto wake wa kike kuwa atafungua kesi kuwa uncle alitaka kum'baka mwanae ikafika hatua Hadi mtoto akayavaa Yale maneno bn, Asee sijui iliishiaga wapi lakini ninachoshukuru hayakufika huko Ila kiukweli mama anaweza akala ubia na watoto wakakupoteza.... Sizungumzi kuwa huyo jamaa kasingiziwa, hapana. Ila tusiblame maana hakuna ajuae ukweli kati yetu...
 
Polisi wanamshikilia baba mwenye miaka 57 mkazi wa Kijiji cha Ndaleta mkoani Manyara kwa tuhuma za kuwabaka binti zake watatu wenye miaka 15, 17 na 18. Wizara ya Maendeleo ya Jamii imesema watoto hao tayari wamepatiwa matibabu na wanaendelea kupatiwa msaada wa kisaikolojia.

---
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 57, mkoani Manyara Kaskazini mwa Tanzania anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa tuhuma za kuwabaka watoto wake watatu wa kike alhamisi ya juma lililopita.

Akitoa taarifa jijini Dodoma mapema leo, Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Prudence Constantine amesema kuwa baba huyo anadaiwa kuwafanyia tendo hilo la kikatili mabinti zake hao wenye umri wa miaka 15, 17 na 18 katika Kijiji cha Ndaleta, wilaya ya Kiteto.

Constantine alisema kuwa wizara imesikitishwa na taarifa za tukio hilo na inapenda kutoa taarifa kuwa tayari mtuhumiwa yupo mikononi mwa polisi kwa taratibu zaidi za kisheria.

Aidha, amesema kuwa watoto wameshapatiwa huduma za kiafya na wanaendelea kupatiwa huduma za msaada wa kisaikolojia na kijamii.

Mkuu huyo alisema kuwa hivi karibuni kwenye jamii kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili kwenye makundi yote ya jamii ikiwemo watoto.

Hivyo alisema kuwa Wizara inawaomba wananchi kuungana kupinga ukatili wa makundi yote kwa ujumla wake na kutoa taarifa mapema kwenye vyombo vya serikali na vyombo vya kijamii vinavyoweza kutoa msaada wa haraka pale tukio linapotokea.

Chanzo: BBC
Huu ni unbea. Taarifa hazijajitosheleza.
 
Masharti ya mganga hayo. Haiwezi kuwa akili yake, unasimamia kucha kabisa kwa mtoto wako.
 
Kuna kipindi niliishi kwa aunt yangu kukawa na mgogoro baina ya aunt na uncle, Aunt akaanza kumpanga mtoto wake wa kike kuwa atafungua kesi kuwa uncle alitaka kum'baka mwanae ikafika hatua Hadi mtoto akayavaa Yale maneno bn, Asee sijui iliishiaga wapi lakini ninachoshukuru hayakufika huko Ila kiukweli mama anaweza akala ubia na watoto wakakupoteza.... Sizungumzi kuwa huyo jamaa kasingiziwa, hapana. Ila tusiblame maana hakuna ajuae ukweli kati yetu...
Hoja yako ni muhimu mno.... Naomba wadau waizingatie... Hoja yako isipuuzwe!!!
 
Anawaita mmoja baadae mwingine hivyohivyo labda anaweza mwambia mkwe wake wanamazungumzo ya kifamilia, anawatoto wa kike wanne, mmoja tu ndio alikataa kufanya upuuzi wao, wengine waliobaki wanaendelea na ujinga wao
Hawana akili na mama yao yupo wapi mpaka wote anawatafuna, au ndiyo mkewe anamfanya msukule anayetembea mchana laana nyingine hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom