Recent content by Erythloblastosis

  1. Erythloblastosis

    Tuliosema Magufuli aliteua bila kufanya vetting tuombwe radhi

    Duuh! Kuna Mkurugenzi mmoja kule mkoa wa Singida hata kuandika barua ya kikazi hawezi. Yaani ukiona hizo barua zake Unadhani ameandika mtu ambaye hajawahi kuwa hata Katibu wa kitongoji. Mheshimiwa Rais tunakuomba uchunguze Elimu za wateule hawa ili ujiridhishe na Elimu zao.
  2. Erythloblastosis

    Dr. Mwakyembe usimchafue Kikwete bure, ulihamishwa wizara kwa kushindwa kazi

    Hii ndiyo dalili ya wazi kuwa ndani ya Serikali ya Tanzania Rais ndiye Mungu mtu. Mwakyembe anatuaminisha kuwa yeye kama Waziri hakutekeleza wajibu wake kwakuwa JK alimzuia, hivyo hivyo huenda hata sasa akashindwa kutekeleza wajibu kama Magufuli atamzuia. Sasa kuna haja gani ya yeye kuendelea...
  3. Erythloblastosis

    Ningekuwa RC, DC, RPC ama DED Jiji la Mwanza Ningejiuzulu

    Daah, kwa aina ya Watawala tulionao si rahisi. Asilimia 100 ya viongozi /Watawala wetu hawajali wala kuthamini utu wao katika kusimia Falsafa zao bali huthamini Mshahara na kujikomba kwa wakubwa. Hii ni aina nyingine ya Utumwa kwa wasomi wetu.
  4. Erythloblastosis

    Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

    Kuwa na mimba huku una mtoto mchanga si tatizo na si ajabu. Unachotakiwa kufanya ni kulea mimba na mtoto bila kuathiri kimoja kati ya hivyo. Tembelea Kliniki ya Mama na mtoto iliyopo karibu kwa ushauri na msaada zaidi. Hongera!
  5. Erythloblastosis

    Viwanda 1,845 vyaanzishwa mwaka mmoja

    Serikali imetoa taarifa kuwa katika kipindi cha mwaka moja wa Serikali ya awamu ya tano, vimeanzishwa Viwanda vipya 1800. Hata hivyo Serikali inaarifu kuwa hadi sasa Tanzania ina takribani Viwanda 54,000 vinavyofanya kazi. Kwa takwimu hizi Tanzania ina Viwanda vingi kuliko Shule zote za Msingi...
  6. Erythloblastosis

    Rais Magufuli kuwa makini na Ma DC na Wakurugenzi.

    Kwanza naomba nikiri kuwa mimi ni Mwanachama wa CCM na Kiongozi wa UVCCM katika ngazi ya kata. Pili naomba nikiri kuwa mimi ni miongoni mwa wana CCM waliotumia nguvu na gharama kubwa binafsi kukinadi Chama Cha Mapinduzi katika uchunguzi wa mwaka 2015. Tatu, naomba niweke wazi kuwa mimi ni...
  7. Erythloblastosis

    Hivi ni faida gani ambayo wasanii wa Tanzania wamepata kwa kuisaidia CCM wakati wa uchaguzi?

    Nadhani wanapaswa kutubu kama nilivyo tubu mimi kabla Mwenyezi Mungu hajateremsha adhabu yake. Najua ni vigumu sana kukiri Makosa lakini kwa hili ni vema wakakiri na ikibidi wajitokeze hadharani kuwaomba radhi wahanga wote wa dhuluma zinazofanywa na Serikali hii. Najua kuna watu wanaajira zao...
  8. Erythloblastosis

    Tetesi: Mkuu wa wilaya Manyoni atumbuliwa, Ni aliyerudisha kodi ya kichwa kwa wananchi

    Naam, kuna usemi kwamba "Mshahara wa dhambi ni mauti". Huyu jamaa na wakurugenzi wake wanatutesa sana wananchi. Namuomba Mheshimiwa Rais awamulike na Mkurugenzi wa Itigi maana dhambi anazofanya ni kubwa sana. Napata shaka na watu hawa juu ya weledi wao.
  9. Erythloblastosis

    Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka CCM

    Hongera CCM chama changu. Ni vema kama taarifa hii ingekuwa na takwimu badala ya kutumia maneno ya jumla. Mfano barabara ngapi zimejengwa, ndege ngapi zimenunuliwa (siyo zinazotarajiwa). Hii itatusaidia kupima kasi ya utekelezaji wa Ilani.
  10. Erythloblastosis

    Mrema: Makonda na Sirro, kupelekwa kwa Rais Magufuli kuhusu Polisi Jamii

    Mrema anafanya kazi nzuri sana tatizo ni Uhusiano uliopo kati ya Cheo chake na mambo anayotakakufanya. Labda Rais angempa miongozo ili ajue mipaka yake.
  11. Erythloblastosis

    Mwinjilisti amvaa Rais Magufuli, amuonya

    Kama kuna mtu atajiita "Kiongozi wa dini" halafu haioni na kuitenda haki basi huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu. Kiongozi wa dini ni mwangalizi wa haki na Usawa na anapaswa Kunena juu hayo kila sekunde ya Uhai wake.
  12. Erythloblastosis

    Kikwete azidi kuwa lulu kimataifa, Kweli chema chajiuza...

    You won't notice the quality of Jakaya Kikwete unless you are intelligent enough. He is the second clever president of Tanzania after Julius Nyerere. Opponents of Jakaya Kikwete have one common feature "Low Thinkers".
  13. Erythloblastosis

    Hii kauli ya Rais kuhusu Wahehe inanikera sana

    Presidential personality ni suala muhimu sana. Kauli ni msingi mkuu wa Haiba ya kiongozi mkuu wa nchi. Hata kama anafanya utani ni vema akatazama upya faida na hasara za utani huo.
  14. Erythloblastosis

    JamboLeo: Watanzania wakosa imani na 'Rais'

    We have been talking about this :"Africa needs strong Institutions but not strong people ". There is no good leader in Weak institutions.
Back
Top Bottom