DC Singida: Atakayeugua kipindupindu afikishwe mahakamani

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,846
5,057
Wale tuliohoji juu ya uteuzi unaofanywa kwa kuzingatia kigezo cha ukada tu, ipo siku tutaeleweka

========

Watu wawili wakazi wa jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida, wamefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa hatari wa Kipindupindu unaotokana na uchafu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana ofisini kwake, Mkuu wa wilaya ya Singida, Elias Tarimo, alisema Novemba, 26 mwaka huu, ugonjwa huo wa Kipundupindu ulibainika katika vijiji vya Merya na Msange jimbo la Singida kaskazini.

Hata hivyo, alisema kuwa ilichukua muda mrefu mno mamlaka zinazohusika kutoa taarifa ya ugonjwa huo, kitendo kilichochangia idadi ya wagonjwa kuongezeka na kufikia 30.

“Urasimu huu umesababisha hatua stahiki za kudhibiti ugonjwa huu, kuchelewa kuchukuliwa na hivyo kuchangia wananchi wawili kupoteza maisha. Kwa sasa tumebakiwa na wagonjwa sita kambi ya Merya na Msange wapo watatu,” alisema Tarimo.

Mkuu huyo wa wilaya, alisema baada ya kupata taarifa hizo kwa kuchelewa, hawakulala walipiga kampeni ya nguvu kuhimiza usafi wa mazingira, matumizi bora ya vyoo na kuchemsha maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

“Aidha, wataalam walipima maji ya visima 14 yanayotumiwa na wananchi wa vijiji hivyo, na 12 kubainika vina vidudu vinavyochangia ugonjwa wa kipindu pindu. Baada ya kugundua hivyo, tumepiga marufuku maji ya visima hivyo kutumika,” alisema.

Akifafanua, alisema wamewaelekeza wananchi kutumia maji ya bomba na wamechukua mashine kubwa ya kupampu maji kutoka kijiji cha Sagara.

“Mashine hii tumeisimika na itasambaza maji ya bomba katika vijiji hivyo vya Msange na Merya. Hatujaishia hapo, tunaendelea kuwahimiza wananchi kutumia vidoge vya waterguird kwa ajili ya kutibu maji yawe safi na salama. Vile vile tanawahimiza kutumia vyoo na kuacha tabia ya kujisaidia ovyo kwenye vichaka,” alisema.

Katika hatua nyingine, Tarimo alisema kuwa baada ya kufanya kampeni ya kuhimza usafi, mwananchi yoyote atakayeugua Kipindupindu, atatibiwa na akipona, mara moja atafikishwa mahakamani, kujibu tuhuma ya kutaka kujiuawa kwa makusudi.

Wakati huo huo, katika kuchukua hatua kudhibiti Kipindupindu, Manispaa ya Singida imechukua hatua mbalimbali, ikiwemo ya kupiga marufuku wafanyabiashara wa matunda, kumenya matunda. Imeagizwa kuwa matunda yote yaliwe nyumbani baada ya kuoshwa vizuri kwa maji.

Pia kila kaya imeagizwa kutumia vyoo bora na kunawa mikono kwa sabuni kabla ya kula chakula na baada ya kutoka chooni.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Bravo Kizito Lyapembile, amesema mtu ye yote akikamatwa kwa kuchafua mazingira, atatozwa faini kati ya shilingi 30,000 na 300,000.

Chanzo: Mpekuzi
 
Nnavyofahamu, wagonjwa upelekwa hospitali na si mahakamani. Sasa hili la kuwapelekwa wagonjwa mahakamani likoje tena? Au mahakama siku hizi zinatibu magonjwa?

Napita tu.
 
serikali inataka kuleta mchezo wa kukusanya mapata kwenye matukio mf rambirambi za wahanga bukoba na hii sasa wanasubiria ili kipindupindu kienee kisha watakuja na sound ya kusaidiwa.


swissme
 
Kipindu pindu kikitokea hiyo inamaanisha umeshindwa kuweka miundombinu na taratibu mbalimbali za kufuatwa ili kuepuka ugonjwa huo.
Napongeza hatua alizochukua lakini hizi ilibidi zichukuliwe tangu mwanzo. Hao waliosababisha taarifa zisifikie mapema hajawachukulia hatua anataka kuwachukulia hatua wananchi? Hii ni kwakua anaogopa kuenguliwa kwenye nafasi yake ilishasemwa ikigundulika ulipo kuna kipindu pindu utaenguliwa.

Kufanya kazi kwa ajili ya tumbo huku bosi ni kichomi unajikuta unaongea kama hivi.
 
Kamuiga makonda-atakayeugua magonjwa yasiyoambukiza kwa kutofanya mazoezi atozwe gharama mara mbili.
 
...hivi kwa mfano mimi nikila chakula ambacho si kisafi (bila kujua) kwenye restaurant au kwa mama lishe hapo singida kisha nikaugua kipindua-pindua nitakuwa na kosa la kustahili kushtakiwa kweli......??!!
 
Hawa politicians ni shida. Watu hawana maji safi ya bomba 55 years after independence. Wanachimba chini na kupata hayo machafu. Badala ya DC kufuatilia ajue hizo cholera hotspots zinakumbwa na challenge gani, yeye anatoa vitisho tu.

Sasa watu haws masikini wataanza kuugulia nyumbani na waishie kufa tu. Wauguzi nao wataanza kuficha cholera cases na kudai ni acute watery diarrhoea maana kuna hatari na wao kutiwa ndani. Akina Kigwangallah wapo wapi kutoa guidance?
 
Mtu umetoka zako hospitali badala ukapumzike kwanza urudishe afya, unaswekwa ndani kwa kosa la kuumwa...tehteh
 
da hii nayo kali skuiz kupata kese kesi za hapa na hapa ni rahis kiasi hivo kweli tunaenda au tume-stuck some where
 
Back
Top Bottom