Ndiyo matatizo yenu nyie waajiri wa hawa wadada wasaidizi. Mnapowaajiri muwafundishe namna ya kufanya vitu mbali mbali ndani ya nyumba badala ya kuwaachia nyumba huku wakiwa hawajui mengi kuhusu kazi za ndani. Umekosea sana kwa kumpiga, wewe na mkeo ndio wa kulaumiwa hapa na siyo huyo binti.
Ulichosema ni kweli tupu Mkuu. Rais kwenye sakata hili yuko kimya, Waziri wa mambo ya ndani yuko kimya, Mkuu wa TAKUKURU yuko kimya. Nchi yetu imeoza tena sana si ajabu hizo pesa za mafisadi wamesharudishiwa wenyewe na huyo aliyekamatwa kishaachiwa huru.
Hatuna sababu ya kuacha kutumia akili zetu ambazo ni zawadi toka kwa Muumba wetu, wewe unayedumaza akili yako kwa kuamini ulichoambiwa kwamba fisadi Magufuli anastahili kuwa Rais endelea kuidumaza hiyo akili...
Nenda kamwambie kwamba pressure aliyokupa ya wewe kumpa ujauzito ilikutia hofu kwamba labda nawe una matatizo huna uwezo wa kujaza mimba hivyo ulicheza nje na bahati nzuri ukampa mimba huyu binti hivyo kuthibitisha uko fit. Sasa uko tayari kumchukua mtoto na unataka amlee kwa upendo wake wote...
Anastahili kufungwa huyu Mwizi na fisadi, na hili lisemwe kwenye kampeni nchi nzima na kuna ushahidi wa kutosha kuhusu wizi na ufisadi wa huyu fisadi na ushahidi uwekwe hadharani wakati wa kampeni nchi nzima.
Iliwahi kusikiliza hotuba ya Baba wa Taifa aliposema Watanzania wanataka maendeleo, wanataka mabadiliko, Watanzania wamechoshwa na rushwa, Watanzania wamechoshwa na ufisadi yao kama vyote hivi wasipoviona, wasipovipata ndani ya CCM wataenda kuvitafuta nje CCM. Unadhani Mwalimu hakuona tatizo la...
Acha kuwafuatafuata wanawake na mavazi yao. Kama hutaki kuwaona waliovaa nguo fupi basi ukiwaona angalia pembeni au fumba macho yako. Watu wengine banaaa mnapenda kufuatilia mambo madogo madogo yasiyowahusu hata chembe.
Tatizo kubwa la Watanzania wengi ni ujinga. Eti kwa kuteuliwa Magufuli wamesahau kashfa zote kubwa ambazo zimeligharimu Taifa matrilioni ya shilingi. Wanasahau baadhi ya kashfa ambazo zimeligharimu Taifa pesa chungu nzima baadhi zimesababishwa na fisadi Magufuli ikiwemo uporwaji wa nyumba za...
Tangu lini chama cha siasa kikachagua yule anayestahili kugombea toka upinzani? Mnaogopa nini kwa kutotaka Dr Slaa asimame kama mgombea wa UKAWA? Kama hana mvuto si ndiyo mtapata ushindi wa kirahisi na wa kishindo? Naona mmeanza kuweweseka mapema katika juhudi zenu za kumpiga vita Dr Slaa kwa...
Hata ukifanya booking utawekwa kwenye waiting list ndefu, pamoja na gharama kubwa za kulala kwenye hiyo suite kwa siku lakini demand yake ni kubwa sana kutoka kwa wateja mbali mbali duniani.
Wewe kweli hujitambui. Hivi unajua kwamba uchaguzi wa Tanzania si huru na si wa haki? Kama unajua hivyo kwanini kujitoa ufahamu na kuandika yasiyo na mashiko? Kama hujui unaishi chini ya ardhi hujui yanayoendelea ndani ya Tanzania kuhusu uchaguzi na pia maoni ya katiba tunayoitaka Watanzania...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.