Elections 2015 Lowassa: Je, alikosea wapi? Akiamua kuendelea, arekebishe wapi?

Hawajazaa tu tangu alipotwambia kwamba wako 800? Kaibu mwaka sasa tangu atwambie kwamba ana ng'ombe 800

Akapumzike tu kwao Monduli na Regina ili akachunge ng'ombe wake 800. Siasa zimeshamtupa mkono. CCM nawapongeza kwa kumbwaga huyu fisadi
 
Mkuu Nguruvi3,

Umechambua Vyema Sana. Naomba nikuulize maswali matatu:

1. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwake kisiasa?

2. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama atakachohamia?

3. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama chama cha mapinduzi?

Maswali mazuri sana haya Mchambuzi.

Binafsi nafikiri majibu/jibu la maswali haya limelala kwa namna CCM wanavyomtazama EL.

Nafikiri CCM hawamwoni EL kama "individual" bali wanamwona EL kama "organization" mpya ndani ya chama chao.

Hivyo naona CCM strategist wana-contain EL waves kama wanavyocontain waves zingine zinazotishia usalama wa taifa.

Tofauti na fikra za wengi kuwa EL ni tishio kwa CCM wao CCM wanamwona EL kuwa ni tishio LA usalama wa taifa.

Kwa mtazamo huu wa CCM ni vema hekima na busara zituame kwenye fikra za EL organization ili kuepusha potential fatalities. Ikitokea akatekeleza moja ya dynamics ulizohypothesize hapo juu, damage kwa EL Organization itakuwa kubwa mno, pia chama/vyama vya siasa vitakavyompokea vitakuwa vimejichimbia kaburi la kisiasa. Historia ya utumishi wa EL akiwa serikalini na ndani ya CCM pamoja na kumbukumbu za Dr Slaa ndio itakuwa silaha rahisi zitakazommaliza kabisa EL.
 
Mkuu Nguruvi3,

Umechambua Vyema Sana. Naomba nikuulize maswali matatu:

1. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwake kisiasa?

2. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama atakachohamia?

3. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama chama cha mapinduzi?

Kwa umri na alipofikia kisiasa Lowasa has nothing to lose in politics akiamua kuingia opposition, aingie upinzani akajaribu karata yake ya mwisho,kubakia CCM haitamsaidia chochote na wala hatakuwa na legacy yeyote zaidi ya ufisadi na KUKATWA,na nina uhakika akienda upinzani CCM itayumba ingawaje not necessarily will lose na anaweza kushinda vilevile who knows,aache kuwa soft apigane kiume mpaka mwisho na ajue siasa ngumu na kila mtu anataka
 
Lowassa alikuwa anadanganywa na wapambe hakusoma alama za nyakati. Sakata la Richmond ndilo lilomtafuna. Wabaya wake walijua akipita huyu basi kila mtu atalipa hukumu iliyomkabili yeye ndio maana wamemtosa mbali YA afya yake kudorora ambacho pia kimekuwa kikwazo ccm kumpa madaraka akiongoze chama. Ajue kuchambua pumba na mchele sio kila king'acho ni dhahabu. Alijijenga kwenye misikiti na makanisa alisahau chama chake ndio Saudi YA mwisho. Tunajifunza kutokana na makosa.
 
Mkuu Nguruvi3,

Umechambua Vyema Sana. Naomba nikuulize maswali matatu:

1. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwake kisiasa?

2. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama atakachohamia?

3. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama chama cha mapinduzi?

Kuna hisia potofu kuwa kwa CCM kumtema Lowassa, basi sasa chama kimejisafisha na kansa imeondolewa. Lakini cha kustaajabu ni kuwa, kuna nguvu nyingi sana zinazotoka ndani ya CCM na vyombo vya usalama (tetesi la muda mrefu) kumdhibiti Lowassa asiondoke CCM na kwenda upinzani.

Hii inatokana na ukweli kuwa Lowassa kaondolewa kimizengwe, Lowassa ana ufuasi mkubwa sana wa ndani na nje ya CCM na pia CCM inahofia kupoteza Ikulu na nguvu kubwa Bungeni kutokana na Lowassa kuhamia upinzani.

Hii inaashiria nini?

Hii inaonyesha wazi kuwa CCM ni chama cha ubabaishaji, inatumia mbinu chafu kuendelea kushikilia madaraka na kama Kikwete alivyosema Jumamosi, wao wanataka mgombea atakayewarudisha Ikulu (si kiongozi wa kuongoza Tanzania au kuiongoza CCM).

Lowassa ni mtaji mkubwa wa kisiasa na pia ni mzigo mkubwa wa kisiasa. CCM wameshindwa kumshikisha hatiani na tuhuma zote za rushwa na woga wao ni kuwa akija kugombea, wakifungua mdogo kusema Lowassa mchafu, atawauliza ushahidi na CCM hawana ushahidi na mbaya zaidi watatapisha mfereji wa maji machafu utakaowasomba wao CCM na kuwapotezea hatamu za uongozi.

Kama kweli CCM kilikuwa ni chama makini chenye nia ya kuzaliwa upya na kujivua magamba, wasingepeleka kwenye 5 bora au 3 bora watu ambao wana chembechembe za tuhuma na harufu za uchafu.

CCM mwaka huu ilikuwa na mgombea kuchaguliwa mmoja tu, ambaye alikuwa hana doa lolote na CCM badala ya kumchagua huyo na kuuambia umma wa Watanzania na wanachama wake kuwa sasa tunaanza kusafisha chama kiukweli na si porojo na unafiki, CCM ikachagua vinginevyo, ikachagua mlinzi wa mfumo mchafu wa ubabe na kulinda maslahi ya Chama (wachache ndani ya chama) kutafuna hazina ya Taifa!
 
Maswali mazuri sana haya Mchambuzi.

  • Nafikiri CCM hawamwoni EL kama "individual" bali wanamwona EL kama "organization" mpya ndani ya chama chao.
  • Hivyo naona CCM strategist wana-contain EL waves kama wanavyocontain waves zingine zinazotishia usalama wa taifa.

Tofauti na fikra za wengi kuwa EL ni tishio kwa CCM wao CCM wanamwona EL kuwa ni tishio LA usalama wa taifa.

Kama kweli Lowassa ni tishio la Usalama wa Taifa kama walivyokuwa Makaburu, Nduli, Walanguzi na vitu vingine, Lowassa angekuwa Segerea au Ukonga siku nyingi sana, tangu 1995.

Kwanini kama Lowassa alikuwa ni mhuni na mwivi, pale Nyerere alipomtukana 1995 kuwa ananuka harufu ya rushwa, hakuchukuliwa hatua bali Mkapa alimpa uwaziri na mbaya zaidi alipitishwa na chama kuwalikisha jimbo la Monduli?

Kwa nini kama tuhuma za Richmond (ukiondoa matumizi mabaya ya madaraka) zinalenga rushwa na ufisadi, kwa nini CCM na Serikali yake ziliachia akachaguliwa 2010 Monduli na Rais Kikwete alikwenda mpigia kampeni?

Kwa nini Lowassa kama aliendelea na uhuni akakiuka kanuni za chama, alifutiwa kifungo cha kuanza kampeni mapema na kuruhusiwa kuchukua fomu?

Je huko mikoani Lowassa alipokusanya kura karibu 20% ya wanachama wa CCM, iweje tuendelee kuamini ana uwezo wa kuhonga watu milioni moja, na tuna vyombo vya usalama wa taifa na sheria (TISS, PCCB, Polisi, DPP) ambao wangeweza kuleta ushahidi na mashitaka ya ukiukwaji wa kanuni na rushwa dhidi yake?

CCM na uongozi wake inataka kutuaminisha kuwa sasa wameinamisha mtungi na wamekamata panya au wamechinja kope kwa utaratibu, hilo ni changa la macho, tena ni dhihaka kubwa sana kwa Watanzania.

CCM ndi ililelea na kumruhusu LOwassa akawa jinamizi, mzoga, shombo, zimwi na walimfurahia na walinogewa na yote aliyofanya, kwa maana yeye ni kama wao. Tofauti kubwa ni kuwa Lowassa yeye tumbo lake lilikuwa kubwa zaidi na njaa yake na kupenda nguvu zaidi haikuwapendeza wao.

Hapo nitakubali yeye kama mfumo ni hatari kwa usalama wa Taifa kwa mtaji a hatari ndani ya CCM na kuepusha machafuko ndani ya CCM na CCM kupoteza madaraka, hivyo basi ni kuhatarisha usalama wa Taifa.

Kama CCM inataka haki, imfukuze uanachama, Serikali ya CCM imfungullie mashitaka ya tuhuma walzozipata kwenye kikao cha maadili kilichimchuja jina lake, ili ukweli ujidhihiri, mfumo na organization unayoisema kuwa ni hatari kwa usalama wa Taifa ukamatwe na ufutwe kabisa bila kuruhusu chembe moja wa upuuzi huu kujirudia au kujitutumua na kugangamala kama Lowassa alivyofanya.

Kuna viji-Lowassa vingi sana ndani ya CCM, walichofanya ni kumpa sumu nyangumi, Papa, Kasa, Taa, kambale, na dagaa bado wako wengi sana kutokana na mfumo ambao unakumbatiwa na kupewa baraka na uongozi wa juu wa CCm.
 
1. Kashfa ya Richmond ndo imemponza Lowassa - regardless of namna alivyohusika. Na lawama anastahili yeye mwenyewe kwa hili. Richmond ulikuwa ni mchezo wa hatari kwake hata kama na wenzake waliwahi kucheza michezo kama hiyo na wakasitiriwa. He has only himself to blame on this one.

2. Ametoswa na serikali nzima ya sasa na iliyostaafu. Bado ana marafiki wengi lakini hawakuwa na "power" ya kumwezesha kutimiza career aspirations zake. Sasa ajifunze tu hata kwa umri huu alionao sasa kwamba binadamu hawaaminiki; hata marafiki zake ambao hakukutana nao "barabarani" wamethibitisha hilo kwa matendo yao. Alipaswa tu kuwa makini yeye mwenyewe badala ya kuwekeza kwa marafiki.

By the way, yaliyomtokea Lowassa liwe somo lenye manufaa kwa wengine.
Kula like👍 mkuu
 
Nafikiri Lowassa aliwahi ku declare openly kwamba yeye hatoki kamwe CCM, asiyemtaka atoke yeye.
Japo aliwahi kusema hakuna wa kumkata na sasa amekatwa basi lolote laweza kutokea ila naona zama zake zimefika kikomo!
 
Mkuu Nguruvi3,

Umechambua Vyema Sana. Naomba nikuulize maswali matatu:

1. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwake kisiasa?

2. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama atakachohamia?

3. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama chama cha mapinduzi?
Kabla sijapitia hoja naomba nichangie hoja inayosema haiwezekani mtu kuhonga watu milioni moja.

Tunasema inawezakana, kina matter ni definition ya hongo. Imesemwa hongo inaweza kuwa ya pesa, nafasi au upendeleo

Haiwezekani kutoa hongo kwa watu milioni 1. Inawezekana kuhonga watu milioni 1 kwa njia za ahadi, upendeleo, mafao n.k.

Katika kutekeleza hilo mtu hahitaji watu 100.
Wanahitajika watu 50 wenye ushawishi katika jamii.

Hawawanaweza kuitwa influencial leaders au ‘KOL' ikimaanisha key opinion leader.
Ndivyo lobbying ya taasisi inavyofanyika

Kuchukua wenyeviti wa mikoa, wajumbe wa NEC na CC wenye command katika maeneo yao inatosha kuhonga watu M1 .Ukiwawezesha kwa pesa, nao watawezesha wenyeviti wa Wilaya, tarafa had ikata.

Huko ni ahadi tu, mzee akifanikiwa utapanda na kuwa DC, mkuu wa mkoa, au waziri.
Hivyo hongo ipo katika mfumo huo

Hoja za maswali ya Mchambuzi

1 Akiamua kwenda upinzani, Edo atafungua milango ya kuanikwa.Kumbuka, atakuwa ‘Rai' na CM ikiwana dola.
Mwisho wa siku atachafuka kisiasa na kijamii. Anaweza kujikuta Kisutu kama walivyofanyiwa wawili walioko magereza

2 Akihama CCM kwenda upinzani, chama kitakacho mpokea kitaingia katika mgogoro mkubwa na umma.
‘Nembo' yake inahusishwa na udanganyifu , ufisadi n.k Chama husika kitapoteza uhalali wa kusimamia maadili ya nchi.

Chama hicho hakitakuwa na platform ya kukemea achilia mbali kuzungumzia uovu kitanasibishwa na uovu.
Unawezaje kuoga maji safi ukajifuta na taulo chafu na kusema umetakata?

3 Akihama CCM, athari itakuwa chanya. CCM itakuwa imejitakasa kwa kuvua gamba bila mawaa.

Hata leo inajifaragua kuvua gamba,seuse akiondoka. Hakuna athari ya kisiasa au wanachama.

Ataondoka na kundi dogo lenye waaminifu, si kama inavyodhaniwa. Ni kundi la ‘KOL' ambalo halina muda wakujipanga.

Kwa hofu hiyo, tayari tumeona wajumbe wa CCM walioku wakaribu wengine walibaki kumshangilia Mzee Pombe.

CCM inaomba aondoke na watu wake wachache ili iweze kujijenga kupitia yeye na wenzake
 
Rev. Kishoka

Security threat is never managed through "cause-effect framework" but rather through "wicked problem framework". It has happened to EL and the team as you've clearly observed.

Best wishes
 
Mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM umeshakamilika, na mgombea aliyepatikana ni John Pombe Magufuli. Pamoja na hayo, ukweli unabakia kwamba katika mchakato wa kutafuta wadhamini, ni Edward Lowassa ndiye aliyeungwa mkono na wanachama na makada wengi wa CCM kuliko mgombea mwingine yoyote.

Edward Lowassa aliungwa mkono na wanachama karibia milioni moja wa Chama Cha Mapinduzi. Pamoja na jina la Edward Lowassa kutorudishwa na vikao vya ngazi za juu ya CCM, kuelekea uchaguzi mkuu, suala la Lowassa kupata wadhamini karibia milioni moja ni suala ambalo halitakiwi kuchukuliwa kimasihara au kubezwa, kote - ndani na nje ya CCM. Kwanini tunasema hivyo:

1. Wadhamini hawa karibia milioni moja ni mchanganyiko wa wanachama na viongozi wa ngazi mbali mbali wa CCM. Wanatoka katika kona mbalimbali za Tanzania. Ni hawa ambao kwa kawaida, ndio wanaochukuaga jukumu la kumbeba na kumnadi mgombea urais (CCM) baada ya jina la mgombea kupatikana.

2. Kwa kuzingatia historia inavyotueleza, upinzani umeweza kunyakua makada wengi wa CCM baada ya makada hao kuenguliwa majina yao na vikao vya juu vya chama, licha ya makada husika kukubalika na kuwa chaguo la wanachama na makada wengi wa ngazi za chini. Kilichofuatia ni kwamba, CCM ilikuja kupoteza majimbo kadhaa kwa upinzani.

Kama ilivyotokea huko nyuma kwa makada kadhaa kuenguliwa katika vinyang’anyiro cha ubunge hivyo safari yao ya matumaini kuzimishwa na vikao vya juu vya CCM licha ya kukubalika na makada wengi wa ngazi za chini za CCM, hali hii imejitokeza kwa mara ya kwanza katika kinyang’anyiro cha kutafuta mgombea urais (CCM) ambapo, Safari ya matumaini ya Edward Lowassa kubeba bendera ya CCM (urais) 2015, Safari hiyo imezimwa rasmi na vikao vya juu vya chama cha mapinduzi. Je:

· Edward Lowassa alikosea wapi katika safari yake ya matumaini ndani ya CCM?

Na iwapo itatokea akashawishika kuendelea na safari yake ya matumaini kupitia chama kingine cha siasa kama ilivyotokea kwa makada wengine walioenguliwa kwenye vinyang’anyiro vya ubunge (CCM), ili kutimiza safari yake ya matumaini nje ya CCM, je:

· Edward Lowassa arekebishe wapi ili kufika safari yake ya matumaini nje ya CCM?

1. Lowassa ni Muoga na pengine tuseme ni mnafiki, kama alikuwa anaona ameonewa na kusingiziwa kwenye issue ya Richmond kwa nini asingekuwa wazi kusema ukweli ili umsafishie njia? Amini usiamini ile issue pia imemdhoofisha sana kisiasa, kwa sababu mpaka sasa hajasema ukweli, alipokuwa Dodoma kwenye mkutano na wandishi wa habari aliahidi kuwa akifika Arusha kwenye mkutano wake mkubwa atalisemea hilo, lakini wapi

3. Alikuwa na team yenye pesa iliyokosa mipango na mbinu za kumwingiza Ikulu, mimi niliidharau team yake baada ya Lowassa kuwa ni miongoni mwa watu wa mwanzo kutangaza nia, yeye ilipaswa kuwa wa mwisho baada ya kuona upepo wote, Judge Ramadhani aliingia mwisho na akabadirisha upepo wa wagombea wote, kama ingekuwa Lowassa na support aliyonayo ingekuwaje?

2. Nadhani pia Lowassa ana matatizo ya kujieleza, hana mtiririko mzuri kabisa wa kuelezea kitu, hivyo ni vigumu sana kumwelewa Lowassa, hotba yake moja tu ile ya pale bungeni alipokuwa anaachia ngazi ndio ilieleweka, zingine zote hata wakati wa Kampeni ikikuwa ni vigumu kumwelewa Lowassa

4. Cha kufanya kwa sasa ni ile ya "kumkoma nyani giladi" kama mbwai mbwai tu, kama wamemwaga mboga yeye amwage Ugali, inampasa atumie nguvu zake zote, pesa zake zote kuhakikisha CCM haitoi Raisi, sio kwa yeye kugombea upinzani, bali kwa kusupport mgombea wa upinzani, so anaweza kwenda opposition na kuwa ni mtu wa kawaida tu na atumie nguvu zake kutengeneza raisi wa upinzani
 
Wakuu salam
Mchambuzi asante kwa maswali mazuri. Naomba nami kuongezea maswali mawili

1. Je huu ndo mwisho wa EL kwenye majukwaa ya siasa?

2. Endapo EL atabaki ndani ya CCM na akafanikiwa kuingia kwenye vikao, Ni madhara gani yataendelea ndani ya chama?

Wapi EL atapeleka mchango chamani kusaidia mgombea wa CCM

SP
 
Je:

· Edward Lowassa alikosea wapi katika safari yake ya matumaini ndani ya CCM?

Na iwapo itatokea akashawishika kuendelea na safari yake ya matumaini kupitia chama kingine cha siasa kama ilivyotokea kwa makada wengine walioenguliwa kwenye vinyang’anyiro vya ubunge (CCM), ili kutimiza safari yake ya matumaini nje ya CCM, je:

· Edward Lowassa arekebishe wapi ili kufika safari yake ya matumaini nje ya CCM?
1. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwake kisiasa?

2. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama atakachohamia?

3. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama chama cha mapinduzi?

Mkuu Mchambuzi, kwanza asante kwa uzi huu, pia asante kwa mchango kutoka kwa Mkuu Nguruvi3.

Baada tuu ya jina la Lowassa kukatwa kwenye 5 bora, nilipandisha uzi huu, Kukatwa Kwa Lowassa, Jee Ndio Mwisho wa Ile Safari, Au..., nikishauri ahame CCM safari iendelee, huku nikitaraji atakayepita ni Membe!.

Lakini baada ya kupitishwa Magufuli, nilifanya about turn na kumshauri sasa atulie tuu, kwa sababu Magufuli ni jembe zaidi ya Lowassa!. Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali yaishe, vunja kambi na kujisalimisha!.

Katika uzi wangu wa posibility ya kupitishwa kwa Magufuli nilioupandisha humu Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, nilitoa angalizo kuwa jina la Magufuli limetajwa for a reason!. Mpaka sasa kuna watu wanaamini kupitishwa kwa Magufuli kumetokea tuu by chance na sio plan or pre meditated move!.

Nikirudi kwenye hoja hizi
1. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwake kisiasa?-mpaka hapo tuu baada ya kukwa, Lowassa sasa kwisha!, baada ya kupita kwa Magufuli, hata akihamia upinzani bado atakwisha tuu!.

2. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama atakachohamia?, athari zitakuwa kama zile za Mrema tuu, atahama na wafuasinwake wawili watatu, chama atakachojiunga kitainuka kwa nguvu ya soda tuu, then atajifia na kitajifia zake!.

3. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama chama cha mapinduzi?- mgombea angekuwa Membe kisha Lowassa akahama, CCM kingeathirika sana kwa sababu angekata pande kubwa la Kanda ya Ziwa, na CCM ingepigwa chini jumla!.

Tukubali tukatae, kwenye siasa zetu kuna karata mbili za turufu ambazo huwa zinatembea, hatuzikubali lakini zipo!.
Hii ni turufu ya Udini na Ukanda. Katika kumchagua Magufuli, hizi zote mbili zimezingatiwa. Ukinisoma hapa utanielewa
[h=3]Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote?.
[/h][h=3]Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real?
[/h]Kuna uzi niliwahi kuupandisha humu kuuliza "Rais wa Tanzania akiwa Mkristu "Jee ni lazima awe Mkatoliki?!", mode waliifuta fasta na mimi kunyooshewa kidole cha "mdini mkuu!". Nilipopandisha huu uzi Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, based on sababu nilizozisikia, na hili likaja kutokea, hivyo nime confirm kile nilichokisikia, lakini sio lazima kukisema kila unachokisikia, haswa ikitokea unaposikia jamba ambalo una disbelief halafu linatokea!.

Tuna siasa za Ukanda, niliwahi kusema humu, kuna Kanda fulani ndizo determinant ya nani anakuwa rais wa Tanzania!. Nikasema humu kuwa lakini hata Kaskazini yote wawachague wapinzani, bila kuishika Kanda ya Ziwa, mtu wao hawezi kuwa rais!. Kanda ya Ziwa ndio determinant. Kama ulinote hata Lowassa aliweka msisitizo Kanda ya Ziwa, mtu kama Mgeja ndizo zilikuwa nguzo zake!, siku ile akitangaza nia pele Sheikh Amri Abeid, Lowassa aliinuka kitini kuja kumpokea M/Kiti wa CCM Geita, Joseph Msukuma!. Hata kama umefuatilia kwa karibu nyendo za Kinana kwenye Kanda ya Ziwa, utanielewa!. Kanda hii ndio yenye the biggest chunk ya population kubwa Tanzania. Wazukuma ndilo kabila kubwa kuliko kabila jingine lolote nchini Tanzania na ndilo kabila pekee linalomiliki mkoa mmoja mzima wenye kabila moja bila kuchanganya na kabila jingine lolote!.

Baada ya kuchaguliwa Magufuli kutoka kanda ya Ziwa, damu ni nzito kuliko maji, hivyo ile support yote ya Kanda ya Ziwa ambayo Lowassa angeitumia kama mtaji, sasa imerudi nyumbani!.

Ila Chadema/Ukawa, kama ndio bado itamtegemea kwa Lowassa kwa 2020, watakuwa watu wa ajabu sana, kwa sababu by 2020, Lawassa atakuwa by passed by events, he will be too old to cop. Chadema watafute damu change ambaye ni charismatic, kwa ajili ya kujipanga tuu kwa 2025, kwa upande wangu, uchaguzi wa 2020 kwenye urais, ni igizo tuu la uchaguzi!. Hivyo the best thing kwa sasa Lowassa to do, ni kutulia, kukubali matokeo na kustaafu kwa amani, akajichungie ngombe wake kwenye zile ranchi zake, na kwenda akajipumzikie kwenye kasri lake kule London maisha yake yaliyobakia!.

Paskali

KOSA KUBWA alilolifanya ni pale alipoamua kuzira/kukubari kujiuzuru u-PM kwa sakata la Richmond, wakati lilikuwa dili lake na Mkulu.

Wewe unamawazo km Yangu!!
Bora angekataa kabisa!!!
Alifanya kosa kukubali kuachia ngazi
 
Uchu wa kupitiliza wa Madaraka + Namna mbaya ya kukabiliana na Changamoto + Fikra Potofu ya Pesa ni kila kitu + Kiburi kwa Viongozi Serikalini na Chamani + Wafuasi waliolewa mapesa na matumaini ya madaraka = Kuanguka Kwake.

Na kama akiyaendeleza hayo anaenda kuanguka zaidi ya hapa.

Hii equation nimeikubali.
 
Mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM umeshakamilika, na mgombea aliyepatikana ni John Pombe Magufuli. Pamoja na hayo, ukweli unabakia kwamba katika mchakato wa kutafuta wadhamini, ni Edward Lowassa ndiye aliyeungwa mkono na wanachama na makada wengi wa CCM kuliko mgombea mwingine yoyote.

Edward Lowassa aliungwa mkono na wanachama karibia milioni moja wa Chama Cha Mapinduzi. Pamoja na jina la Edward Lowassa kutorudishwa na vikao vya ngazi za juu ya CCM, kuelekea uchaguzi mkuu, suala la Lowassa kupata wadhamini karibia milioni moja ni suala ambalo halitakiwi kuchukuliwa kimasihara au kubezwa, kote - ndani na nje ya CCM. Kwanini tunasema hivyo:

1. Wadhamini hawa karibia milioni moja ni mchanganyiko wa wanachama na viongozi wa ngazi mbali mbali wa CCM. Wanatoka katika kona mbalimbali za Tanzania. Ni hawa ambao kwa kawaida, ndio wanaochukuaga jukumu la kumbeba na kumnadi mgombea urais (CCM) baada ya jina la mgombea kupatikana.

Lowassa ameanza campaign ya urais tangu mwaka 1995, na alipofanikiwa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu ndio alizidisha campaign, kwa kupanga safu ya watendaji anaowataka yeye kupitia TAMISENI. Na kama kumbukumbu yangu ni sahihi mara baada ya kuwa Waziri Mkuu ulipelekwa muswada bungeni ambao ulimfanya Waziri Mkuu kukaimu madaraka in the absence ya Rais! = POWER MONGERING.

Baada ya kujiuzulu Uwaziri Mkuu alikuja na mbinu ya Harambee kuandaa mtandao wa hicho unachosema "wanachama karibia milioni moja". Hata mlala hoi wa nchi hii anajua kuwa wadhamini wa Lowassa walipatikana kwa njia ya pesa zaidi kuliko hoja! Yes, wanaCCM wenzake nao wametumia hela lakini hela ya Lowassa ni ndefu.

Pili, Kanuni zinamtaka mgombea kupata wadhamini 450 kutoka mikoa isiyopungua 15; kati yake 12 toka Bara na 3 toka Zanzibar. Yeye Lowassa kwa kuonesha jeuri ya pesa, alichukuwa wadhamini MIKOA YOTE. = CAMPAIGN

Tatu, Mkakati wa kupata wadhamini kwa MALAKI (870,000) ulilenga kuleta msukumo (pressure) kwa CCM kwamba yeye anakubalika zaidi (regardless kwamba alihonga), hivyo hawana jinsi zaidi ya kukubali kauli ya 'wananchi wengi'. = BLACMAIL

Nne, Kamati ya Bunge ili-implicate 'Waziri Mkuu' Lowassa kwenye sakata la kampuni hewa ya Richmond, hivyo kusababisha Lowassa kujiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu. Hadi leo hii Lowassa hajawaambia wana-CCM na Watanzania kwa ujumla wao uhusika wake (au kutohusika kwake) na sakata hilo la Richmond! Kimya chake, na kujiuzulu kwake vinatoa tafsiri moja tu - UONGOZI MBOVU

Sasa, maswali yako kwamba Lowassa alikwama wapi na afanye nini kama anataka kuendelea mbele ni hivi:
- Lowassa amekwama kwenye utii wa kanuni na taratibu zinazoongoza Taasisi ambayo naamini alijiunga nayo kwa hiari. Ametumia fedha nyingi ili kushinikiza matwaka yake binafsi jambo. Na hii inaweza kuunganishwa na hoja kwamba Lowassa hana historia ya kufanya mikutano ya kuimirisha Chama chake cha CCM. Mara nyingi huonekana na mikutano ya kunadi watu ambao ana maslahi nayo, au yeye binafsi!

Afanye nini? Lowassa ana imani na CCM? Anaamini kuna mwana CCM yeyote mwenye uwezo wa kukiongoza hicho chama zaidi yake?

Lakini swali muhimu zaidi, kwanini Lowassa amezungukwa na watu ambao wamehusika na kashfa kubwa hapa nchini? Iweje kundi linamuunga mkono lisheheni wafanyabiashara waliotajwa kwenye kashfa nzito nzito au mawaziri waliofukuzwa kazi kutokana na uongozi mbovu?
 
Lowassa atafaa sana kuwa ama literature figure study or political science study. Na silisemi hili kwa masihara, bali nikiwa very serious kuwa tunavyoendelea mbele, kuna watu katika jamii yetu na vizazi mbali mbali watatokea kuwa wa pekee na ni wasifu tosha wa kusoma na kujifunza kwa wigo mkubwa sana: Lowassa kama binaadamu, Lowassa kama mzazi, Lowassa kama mume, Lowassa kama mwanasiasa.

Labda na sisi tutaacha kusoma ya Socrates, Marx na Adam Smith, tumwongeze Lowassa pamoja na kina Kinjekitile, Nyerere na Mkwawa!
 
Kwa umri na alipofikia kisiasa Lowasa has nothing to lose in politics akiamua kuingia opposition, aingie upinzani akajaribu karata yake ya mwisho,kubakia CCM haitamsaidia chochote na wala hatakuwa na legacy yeyote zaidi ya ufisadi na KUKATWA,na nina uhakika akienda upinzani CCM itayumba ingawaje not necessarily will lose na anaweza kushinda vilevile who knows,aache kuwa soft apigane kiume mpaka mwisho na ajue siasa ngumu na kila mtu anataka

ushauri huu naona aliufanyia kazi kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa,
 
Mkuu Mchambuzi, kwanza asante kwa uzi huu, pia asante kwa mchango kutoka kwa Mkuu Nguruvi3.

Baada tuu ya jina la Lowassa kukatwa kwenye 5 bora, nilipandisha uzi huu, Kukatwa Kwa Lowassa, Jee Ndio Mwisho wa Ile Safari, Au..., nikishauri ahame CCM safari iendelee, huku nikitaraji atakayepita ni Membe!.

Lakini baada ya kupitishwa Magufuli, nilifanya about turn na kumshauri sasa atulie tuu, kwa sababu Magufuli ni jembe zaidi ya Lowassa!. Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali yaishe, vunja kambi na kujisalimisha!.

Katika uzi wangu wa posibility ya kupitishwa kwa Magufuli nilioupandisha humu Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, nilitoa angalizo kuwa jina la Magufuli limetajwa for a reason!. Mpaka sasa kuna watu wanaamini kupitishwa kwa Magufuli kumetokea tuu by chance na sio plan or pre meditated move!.

Nikirudi kwenye hoja hizi
1. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwake kisiasa?-mpaka hapo tuu baada ya kukwa, Lowassa sasa kwisha!, baada ya kupita kwa Magufuli, hata akihamia upinzani bado atakwisha tuu!.

2. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama atakachohamia?, athari zitakuwa kama zile za Mrema tuu, atahama na wafuasinwake wawili watatu, chama atakachojiunga kitainuka kwa nguvu ya soda tuu, then atajifia na kitajifia zake!.

3. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama chama cha mapinduzi?- mgombea angekuwa Membe kisha Lowassa akahama, CCM kingeathirika sana kwa sababu angekata pande kubwa la Kanda ya Ziwa, na CCM ingepigwa chini jumla!.

Tukubali tukatae, kwenye siasa zetu kuna karata mbili za turufu ambazo huwa zinatembea, hatuzikubali lakini zipo!.
Hii ni turufu ya Udini na Ukanda. Katika kumchagua Magufuli, hizi zote mbili zimezingatiwa. Ukinisoma hapa utanielewa

[h=3]Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote?.
[/h][h=3]Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real?
[/h]Kuna uzi niliwahi kuupandisha humu kuuliza "Rais wa Tanzania akiwa Mkristu "Jee ni lazima awe Mkatoliki?!", mode waliifuta fasta na mimi kunyooshewa kidole cha "mdini mkuu!". Nilipopandisha huu uzi Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, based on sababu nilizozisikia, na hili likaja kutokea, hivyo nime confirm kile nilichokisikia, lakini sio lazima kukisema kila unachokisikia, haswa ikitokea unaposikia jamba ambalo una disbelief halafu linatokea!.

Tuna siasa za Ukanda, niliwahi kusema humu, kuna Kanda fulani ndizo determinant ya nani anakuwa rais wa Tanzania!. Nikasema humu kuwa lakini hata Kaskazini yote wawachague wapinzani, bila kuishika Kanda ya Ziwa, mtu wao hawezi kuwa rais!. Kanda ya Ziwa ndio determinant. Kama ulinote hata Lowassa aliweka msisitizo Kanda ya Ziwa, mtu kama Mgeja ndizo zilikuwa nguzo zake!, siku ile akitangaza nia pele Sheikh Amri Abeid, Lowassa aliinuka kitini kuja kumpokea M/Kiti wa CCM Geita, Joseph Msukuma!. Hata kama umefuatilia kwa karibu nyendo za Kinana kwenye Kanda ya Ziwa, utanielewa!. Kanda hii ndio yenye the biggest chunk ya population kubwa Tanzania. Wazukuma ndilo kabila kubwa kuliko kabila jingine lolote nchini Tanzania na ndilo kabila pekee linalomiliki mkoa mmoja mzima wenye kabila moja bila kuchanganya na kabila jingine lolote!.

Baada ya kuchaguliwa Magufuli kutoka kanda ya Ziwa, damu ni nzito kuliko maji, hivyo ile support yote ya Kanda ya Ziwa ambayo Lowassa angeitumia kama mtaji, sasa imerudi nyumbani!. Hivyo the best thing kwa sasa Lowassa to do, ni kutulia, kukubali matokeo na kustaafu kwa amani, akajipumzikie kwenye kasri lake kule London maisha yake yaliyobakia!.

Pasco

Mkuu Pasco

Uko vizuri sana kuchambua na kubashiri mwelekeo wa siasa zetu. Hongera tena kwa kuwa na kiburi cha kuamini kwamba 'it is not over till it's over'.

Karama yako ya kuchambua na kubashiri ni karama adimu. Hongera mno kwa karama hii. Mwenyezi Mungu akujalie ujasiri ili utumie karama hii kwa faida ya nchi yetu hasa hasa kwenye kupigania ustawi wa watu masikini na wanaotengwa na jamii (socially excluded) kwa sababu mbalimbali.

Nikutakie heri na fanaka kwa mwaka 2016.

Inshallah.
 
Back
Top Bottom