Dr. Slaa nakushauri pumzika, Urais sahau

Dr. Slaa nakushauri pumzika, Urais sahau

mchuzi ushatiwa mguu hapo Amkawewe jiulize nani alie utia mguu haunywiki tena.
 
km ishu ni sura mpya mbona hata magufuli ni sura ile ile ktk serikali yenu.mnge msimamisha sepetwo tungesema mmeleta sura mpya kwe siasa.
 
WATANZANIA ni watu wa ajabu sana.Kuchaguliwa Magufuli mnaanza kuona kama upinzani hauna maana.
Tuelewe ya kuwa mfumo ndio mbovu na hata kama Magufuli angekuwa vipi lakini CCM ina walakini mkubwa ambao itabidi ajitoe fahamu kuweza kukabiliana nao.
Kwa CCM suala ni ushindi lakini katika kubadili mfumo hilo halipo kwani ndani yake kuna King Makers ambao hawaonekani.
Magufuli ni mtendaji na si mwanasiasa na muda mfupi atajutia kiti kwani mambo yatakuwa kinyume na dhamira yake.
Upinzani ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na litakuwa jambo la ajabu kupungukiwa na idadi ya wabunge wa upinzani.

Kwani mifumo haibadiliki? CCM ilizaliwa na mifumo ya kifisadi? Tumewatengenezea mazingira, leo mafisadi wote wa ccm wanahamia either ACT au UKAWA na kutuachia CCM safi...hapo ndo mtaanza kuona mchakamchaka
 
no stone will be left unturned, na wahame wote wakiache chama safi katika misingi ya waanzilishi
 
stroke,
What does you signature imply, has punctuation in those words has anything to do with it?

Anyway, can you tell me if you know the name of the piper who calls the tune for 'puppets' to dance or swing? If you don't, I'd be good enough to lighten you on this: THESE ARE MALICIOUS KINGPINS bent to drain dry our abundant natural resources leaving us with nothing. They're using any dirty methods available to make sure Tanzania get president who'd be more softer than the outgoing one for them to come in and go out without hindrance.

Dr. Slaa or anybody from UKAWA is the only solution to combat corruption, rampant theft in government institution and every vices in the system.
 
bwana stroke, kama bado unasumbuliwa na stroke basi ninaomba ukatibiwe. Ila kumbuka wakati wa uchagunzi wa marekani hasa mwanzoni ilionekana kati ya vyama viwili kimoja kinaongoza, lkn kuja kumaliza kampeni kile kingine kikaja juu! Hivyo swala la slaa liache lilivyo wewe endelea na kudumaa mpaka mwisho wa maisha yako!

wabuyaga kwa nini hamtaki ukweli mbona siasa zenu hazina tofauti na sisim heri hata sisim kuna demokrasi. Mtabugia vumbi tu la kampeni lakini ikulu hataikaribia
 
WATANZANIA ni watu wa ajabu sana.Kuchaguliwa Magufuli mnaanza kuona kama upinzani hauna maana.
Tuelewe ya kuwa mfumo ndio mbovu na hata kama Magufuli angekuwa vipi lakini CCM ina walakini mkubwa ambao itabidi ajitoe fahamu kuweza kukabiliana nao.
Kwa CCM suala ni ushindi lakini katika kubadili mfumo hilo halipo kwani ndani yake kuna King Makers ambao hawaonekani.
Magufuli ni mtendaji na si mwanasiasa na muda mfupi atajutia kiti kwani mambo yatakuwa kinyume na dhamira yake.
Upinzani ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na litakuwa jambo la ajabu kupungukiwa na idadi ya wabunge wa upinzani.

Well thought well said
 
Kwa Mtanzania Mwenye Akili Timamu Ambae Hajatekwa Na Mgando Wa Mawazo Na Kumezwa Na Ulimbukeni Wa Ushabiki.Anaweza Akapingana Na Huu Ukweli Kwamba Dr.Slaa Wa Leo Sio Yule Wa Miaka Mitano Iliyopita.Dr.Slaa Wa Leo Amepoteza Mvuto Na Hana Ushawishi Wa Kisiasa Kama Aliokuanao Miaka Mitano Iliyopita.Dr.Slaa Wa Leo Hata Akiamua Aende Akagombee Ubunge Wa Jimbo Lolote(Achilia Mbali Uraisi)Ushindi Wake Bado Ni Kitendawili.

UKAWA Watakua Wamefanya Kosa Kubwa Sana Kumteua Dr.Slaa Kama Mgombea Wao Wa Kiti Cha Uraisi.Na Matokeo Yake Ni Anguko La Aibu Kwa UKAWA.

Kila MwanaUKAWA Mwenye Akili Timamu.Sasa Anajua Kama CCM Wamekisimamisha Kisiki.Na Zinahitajika Nguvu Za Ziada Kuweza Kuking'oa.Kwa Mtu Dhaifu Kama Dr.Slaa Wa Leo Hana Ubavu Hata Wa Kukitikisa.

Ushauri:UKAWA Waweke Nguvu Zao Nyingi Katika Nafasi Za Ubunge Ili Waweze Kukusanya Viti Vingi.Ila Kwa Habari Ya Uraisi Wajipange Upya Katika Miaka10 Ijayo.Lakini Kwasasa Wameshachelewa Hawana Mtu Imara Anaeweza Kucheza "Muziki Munene" Wa Dk.John Pombe Magufuli.

You really are scared of this man from the tone of your voice, you shouldn't!
 
Tokea Dr. Slaa, aje na ile list ya mafisadi papa, hakuna jipya tena alilowahi kulileta.

Dr. Slaa kabakia jina tu, siasa za Tanzania zimemkataa, kuendelea kugombea hiyo nafasi ni kupoteza muda na rasilimali.

Nakushauri upumzike katika nafasi yako ya ukatibu mkuu, muda wako umekwisha kuwika katika siasa za ushindani.

Siasa za kishindani zinahitaji ubunifu na uibuaji hoja zinazolengea kuleta changamoto ya maendeleo, Dr. slaa hajawahi kuibua hoja yoyote kuanzia nyakati zile, na amekua tu akiishi katikamiale ya mwanga wa nyota iliyozaliwa karne zile alizoibuka katika siasa za taifa hili.

Hakuna jipya toka kwa Slaa, Chadema wala Ukawa. Wagombea wa Ukawa ni wale wale, Kama sio slaa, basi ni Lipumba au Mbatia.

Watanzania wanahitaji kuona sura mpya katika majukwaa, sidhani kama nafasi ya urais, lazima iende kwa Slaa, lipumba au Mbatia, kwenye vyama vyao, kuna maelfu wa wanachama wengine wenye sifa za kugombea.

Ubinafsi wa watu hawa ni viashiria vya kidikteta, ambavyo kwa utaratibu wetu kama watanzania, hatuna ubinafsi wa viwango vya slaa, Lipumba na mbatia.

Tuwalazimishe Ukawa kuleta sura mpya kwa kuwakataa wagombea wake katika masanduku ya kura.

CCM all the way till 2025.

Sura mpya? Mimi nilidhani anahitajika mgombea mwenye uwezo?

Ndio maana CCM mlichagua Kikwete, sura mpya yenye mvuto. Nchi hii ni ya kuhurumiwa tu, kama wachambuzi wenyewe ndio akina situroki.
 
Tokea Dr. Slaa, aje na ile list ya mafisadi papa, hakuna jipya tena alilowahi kulileta.

Dr. Slaa kabakia jina tu, siasa za Tanzania zimemkataa, kuendelea kugombea hiyo nafasi ni kupoteza muda na rasilimali.

Nakushauri upumzike katika nafasi yako ya ukatibu mkuu, muda wako umekwisha kuwika katika siasa za ushindani.

Siasa za kishindani zinahitaji ubunifu na uibuaji hoja zinazolengea kuleta changamoto ya maendeleo, Dr. slaa hajawahi kuibua hoja yoyote kuanzia nyakati zile, na amekua tu akiishi katikamiale ya mwanga wa nyota iliyozaliwa karne zile alizoibuka katika siasa za taifa hili.

Hakuna jipya toka kwa Slaa, Chadema wala Ukawa. Wagombea wa Ukawa ni wale wale, Kama sio slaa, basi ni Lipumba au Mbatia.

Watanzania wanahitaji kuona sura mpya katika majukwaa, sidhani kama nafasi ya urais, lazima iende kwa Slaa, lipumba au Mbatia, kwenye vyama vyao, kuna maelfu wa wanachama wengine wenye sifa za kugombea.

Ubinafsi wa watu hawa ni viashiria vya kidikteta, ambavyo kwa utaratibu wetu kama watanzania, hatuna ubinafsi wa viwango vya slaa, Lipumba na mbatia.

Tuwalazimishe Ukawa kuleta sura mpya kwa kuwakataa wagombea wake katika masanduku ya kura.

CCM all the way till 2025.

Unaonaje ungewashauri UKAWA wamuweke Dr. Slaa ili iwe raisi kwetu CCM kushinda? Mbona unawastua mapema hivyo au na wewe ni CDM?
 
1. Nyumba za Serikali
Kwa hakika hili ni doa kubwa sana kwa Magufuli. Ni katika kipindi alichokuwa Waziri wa Ujenzi (awamu ya 3) alishawishi kwa nguvu na msukumo mkubwa sana mpaka kufanikiwa uuzaji wa nyumba za serikali.

Hii hatua ya Magufuli halina tofauti na kile alichokiita CAG Professor Assad “Political Entrepreneurship”. Professor Assad mara baada ya kuingia madarakani alisema wazi kwamba mradi wa Magufuli wa kuuza nyumba za serikali ni ufisadi mkubwa sana. Professor Assad alizidi kusema ya kwamba alichokifanya Magufuli yalikuwa kwa manufaa yake binafsi na ilikuwa ni “personal political entrepreneurship”.

Katika uamuzi huo, Magufuli alienda mbali zaidi mpaka kugawa bure baadhi ya nyumba kwa ndugu zake na mahawara zake. Kwa mfano Dada Kabula ambaye ni mmiliki hewa wa Kebby’s Hotel iliyopo Mwenge/Bamaga jijini Dar es Salaam. Dada Kabula ambaye hajawai kuwa mtumishi wa umma tokea awamu ya kwanza mpaka leo hii Ocampo ninaposhusha huu uzi alifanikiwa kuhongwa nyumba mbili zenye Plot No. MSM/201 na Plot No. MK/521 (Mikocheni na Msasani).

Kwa hatua hiyo Magufuli aliliingiza serikali hasara kubwa sana, na hayo machungu mpaka leo hayajaisha na serikali bado linaendelea kubeba mzigo. Katika kipindi hiki tumeshuhudia watumishi wengi (Majaji, na watendaji wakuu, makatibu wakuu) wamekuwa wakiishi hotelini, huku gharama za vyumba zikiwa za hali ya juu sana almost dola 1200-1500 kwa mwezi ambayo ni sawa na Millioni 27 kwa mwezi; kwa mwaka ni Millioni 324 kwa mtumishi moja.

2. Ujenzi wa Barabara
Eneo hili ni sehemu nyingine ambayo Magufuli amekuwa akijipatia fedha haramu. Baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakijaribu kusema kwamba ni TANROADS ndiyo wahusika wakuu katika barabara na siyo Magufuli. Ingawa hoja yao siyo ya kweli na haina mashiko.

Kiutaratibu na sheria barabara utakiwa kuwa na upana (width) wa 6.5m ila imegundulika barabara nyingi kipindi hichi cha Magufuli zimekuwa zikijengwa kwa 5.7m to 6m na siyo 6.5m, je fedha za hizo baki 0.5m to 0.8m zinakwenda wapi, ni wazi fedha hizo uingia mifukoni mwa Magufuli na washirika wake wa Tanroads. Vile vile ni kipindi kirefu sasa Highway Economic Assessment ya miradi ya barabara imekuwa hazifanyiki kitu ambacho kinapelekea barabara zetu nyingi kuwa chini ya viwango. Utafiti wa Ocampo unaonyesha kwamba barabara kuwa chini ya viwango ni swala la makusudi ambapo waziri na wasimamizi wa miradi husika wanakula na kugawana fedha za miradi….

3. Sakata La Bomoa Bomoa
Ni jambo la wazi ya kwamba sheria zimetumgwa ili zifuatwe, lakini kuwa na ubinadamu au utu ni zaidi ya sheria. Ni Magufuli huyu huyu alipigwa stop na Mh. Rais pale alipoona Magufuli anakiuka wazi haki za binadamu. Ubomoaji wa nyumba zilizopo pembezoni mwa barabara umekuwa hauzingatii “UTU”. Ni jambo la wazi wanaanchi wengi waliobomolewa nyumba zao mpaka sasa wako katika hali ngumu ya maisha na hawana uelekeo baada ya kufanyiwa unyama usiyothimilika na Magufuli.

Either wataalamu wengi pale wizarani katika mahojiano wanasema Magufuli hana tabia ya kufata sheria na utaratibu, wakitolea mfano swala la kuvunjwa kwa jengo la TANESCO (Ubungo) na jengo la Millenium Towers. Kwa hakika ni jambo jema sana kuwa na Rias kama JK aliyediriki kumpiga stop Magufuli, hivyo basi ni wazi anapaswa apate mtu wa juu yake katika kufanya maamuzi, ila yeye ndiyo akiwa mtoa maamuzi walai nchi tutaipoteza (Tafakari kwa kina).

4. Shelly Ya Mwanza
Tukizidi kukumbuka sakata la Shelly ya Mwanza ndipo tunazidi kujua jinsi gani Magufuli ni mtu wa kukurupuka na mtu mwenye chuki. Kwa chuki zake binafsi kipindi cha awamu ya 3 akiwa waziri wa ujenzi aliamuru kuvunjwa kwa Shelly ya bwana Mansoor (mbunge wa Kwimba) iliyopo maeneo ya madaraka misheni jijini Mwanza. Baada ya ukiukwaji huo wa sheria bwana Mansoor alienda mahakamani na kisha kushinda kesi na hukumu kutolewa kwamba serikali imlipe Mansoor mabillioni ya fedha, sababu kubwa zikiwa ni chuki na kisasi cha Magufuli……

5. Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki
Sifa zingine pekee za Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa. Hayo mambo yamepelekea hata utendaji kazi wa watumishi wa chini kuwa mgumu sana. Watumishi chini ya wizara yake wanasema Magufuli ni mtu mwenye majivuno sana, ni mtu mwenye chuki na ni mtu asiyepokea ushauri wa mtu yeyote yule zaidi ya mke wake na Kabula…

6. Umiliki wa Kebby’s Hotel
Kebby’s Hotel ni hoteli iliyopo Mwenge/Bamaga upande wa kulia kama unaenda posta/mjini. Kwa muda mrefu mmiliki wa hoteli hiyo amekuwa akijificha katika mgongo wa mtu mwingine ila ukweli ni kwamba mmiliki halali wa hoteli hiyo ni John Pombe Magufuli na siyo Dada Kabula.

Umiliki wa Hoteli kubwa kama Kebby’s ambayo kulala ni zaidi ya dola 60-90 inaonyesha wazi kwamba Magufuli ni fisadi wa kimya kimya kama yule jamaa mwingine aliyepiga za Escrow na vibali vya sukari au yule aliyechimbia fedha za Ghadafi kwenye mahandaki.

7. Kuvunja Ndoa
Katika maandiko Matakatifu, Kumbukumbu la Torati 27: 14 imeandikwa alaaniwe yule amtamaniye mke wa nduguye au jirani yake. Ila kinyume na hayo maandiko Matakatifu Magufuli amediriki kumtamani mke wa jirani yake mpaka kupelekea kuvunja ndoa ya mtu.

Dada Kabula ambaye ni mmiliki hewa wa Kebby’s Hotel, awali alikuwa mke wa Januarius Maganga ambaye ni mtumishi mwandamizi katika makampuni ya IPP Media. Swali la kujiuliza kama Magufuli kadiriki kuvunja ndoa ya mtu angali ni waziri wa kawaida tu, je akiwa Rias itakuwaje? Jibu nafkiri unalo…. Na sitaki unipe jibu.

Nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi kutolea mfano sakata la waziri mdogo wa Uingereza aliye onekana na kimada barabarani. Kwa tamaduni za hao wenzetu huo ulikuwa ukosefu mkubwa wa maadili mpaka ikapelekea kufukuzwa kazi na waziri mkuu wa wakati huo.

8. Magufuli Hakifahamu Chama Vizuri
Ni jambo la wazi na ukweli usiopingika kwamba Taifa linatafuta Rais bora na kwa upande mwingine CCM kinatafuta mtu mwenye uwezo wa kushika kofia mbili kwa pamoja.

Magufuli ana utamaduni wa kutumia chama pale anapoitaji madaraka, ila pale tu anapoyapata hayo madaraka anakuwa ajiusishi na mkakati wowote wa kujenga chama. Historia inaonyesha Magufuli hajawahi kushika wadhifa au nafasi yoyote ile ndani ya chama, wanachama wa CCM wanauliza kwamba watamkabidhi vipi mtu asiye na background nzuri kwenye chama? Vile vile historia inaonyesha hajawahi kuchangia hata senti tano katika shughuli zozote zile zenye lengo la kujenga chama.

9. Sakata La Samaki
Katika muendelezo wa kukurupuka katika maamuzi, Waziri Magufuli mwaka jana tena aliliingiza Taifa na serikali kwa ujumla katika hasara nyingine. Ambapo serikali iliamuriwa na mahakama ilipe kiasi cha shilling Billioni 2.8 na kurudiha meli husika baada ya kukiuka sheria za kimataifa pale alipokamata Meli yenye vibali halali na iliyokuwa inafanya shughuli zake kihalali.

Sasa kama ni waziri wa kawaida anadiriki kuvunja sheria za kimataifa, Je akiwa Rais si ni wazi anaweza kulipelekea Nchi ikatengwa na jumuiya za kimataifa….. we need to think kwa umakini sana wakuu…..

10. Sakata La Kivuko
Dhana ya ubinadamu siyo kuvaa nguo au kulala kwenye nyumba bali ubinadamu ni pamoja na kuwa na hekima, busara na kauli nzuri kwa binadamu wenzako; cha kushangaza Magufuli alidiriki kutumia lugha iliyotafsiriwa kama tusi kubwa sana na wananchi wa Dar es Salaam, pale alipoowambia wapige mbizi wakitaka kwenda Kigamboni. Ni jambo jema kwa kiongozi kuwa na msimamo ila msimamo wake uendane na lugha nzuri, ya uungwana na ya ubinadamu. Ni wazi kauli hiyo iliwauzinisha sana na kukasirisha wananchi wengi Dar es Salaam. Ubinadamu na utu ni kitu cha bure na siyo cha ulazima, hivyo ilitegemewa Magufuli awe na kauli nzuri na yenye hekina na busara kwa wananchi husika.

11. Magufuli ni Mtu wa Visasi vya Hatari
Magufuli siyo mtu wa kawaida kabisa, ndani yake amejaa chuki na visasi. Ni mtu wa visasi vya ajabu, hii inanikumbusha alipogombea ubunge 1995 na bwana Ernest Nyororo. Baada ya kushindwa katika kura za maoni ila baadaye alipoteuliwa bila uwoga alianza kumshughulikia Nyororo mpaka ikampelekea Nyororo akapata shinikizo la moyo. Kumbuka Nyororo ni ndugu yake wa damu sasa sisi wengine itakuwaje, ni wazi hili jambo linaitaji tafakari ya kina. Kama ndugu yake anaweza kumshambulia kiasi hicho iweje watu wa kawaida….. Leo Ocampo nikiwa naandika huu uzi sisiti kusema ya kwamba hata hao viongozi wanaotaka Magufuli apitishwe naomba niwaambie kwa chuki na kisasi cha Magufuli kuna siku atawabadilikia tena sana sana. Huko mbeleni naomba msije mkasema Ocampo hakutuambia….. Nina hakika asilimia zaidi ya 100 Magufuli ana chuki na viongozi waandamizi wa sasa, chuki hiyo anasubiri kuilipiza muda ukifika….

NB: Je kuna Magufuli Mwingine au ni huyu huyu?...............

Asanteni
Ocampo four

nimekupenda bure✔✔✔✔✔✔
 
wabuyaga kwa nini hamtaki ukweli mbona siasa zenu hazina tofauti na sisim heri hata sisim kuna demokrasi. Mtabugia vumbi tu la kampeni lakini ikulu hataikaribia

Hivi marikiti kuhamia ACT ndiyo inakufanya usahau aliekuzaa! Jamani kumbe viumbe ndo mlivyo?
 
Tangu lini chama cha siasa kikachagua yule anayestahili kugombea toka upinzani? Mnaogopa nini kwa kutotaka Dr Slaa asimame kama mgombea wa UKAWA? Kama hana mvuto si ndiyo mtapata ushindi wa kirahisi na wa kishindo? Naona mmeanza kuweweseka mapema katika juhudi zenu za kumpiga vita Dr Slaa kwa kumuogopa. Mambo ya Ngoswe mwachieni Ngoswe, ya UKAWA kumsimamisha mgombea yupi hayawahusu hata chembe.

Tokea Dr. Slaa, aje na ile list ya mafisadi papa, hakuna jipya tena alilowahi kulileta.

Dr. Slaa kabakia jina tu, siasa za Tanzania zimemkataa, kuendelea kugombea hiyo nafasi ni kupoteza muda na rasilimali.

Nakushauri upumzike katika nafasi yako ya ukatibu mkuu, muda wako umekwisha kuwika katika siasa za ushindani.

Siasa za kishindani zinahitaji ubunifu na uibuaji hoja zinazolengea kuleta changamoto ya maendeleo, Dr. slaa hajawahi kuibua hoja yoyote kuanzia nyakati zile, na amekua tu akiishi katikamiale ya mwanga wa nyota iliyozaliwa karne zile alizoibuka katika siasa za taifa hili.

Hakuna jipya toka kwa Slaa, Chadema wala Ukawa. Wagombea wa Ukawa ni wale wale, Kama sio slaa, basi ni Lipumba au Mbatia.

Watanzania wanahitaji kuona sura mpya katika majukwaa, sidhani kama nafasi ya urais, lazima iende kwa Slaa, lipumba au Mbatia, kwenye vyama vyao, kuna maelfu wa wanachama wengine wenye sifa za kugombea.

Ubinafsi wa watu hawa ni viashiria vya kidikteta, ambavyo kwa utaratibu wetu kama watanzania, hatuna ubinafsi wa viwango vya slaa, Lipumba na mbatia.

Tuwalazimishe Ukawa kuleta sura mpya kwa kuwakataa wagombea wake katika masanduku ya kura.

CCM all the way till 2025.
 
Aliemuua kisiasa Babu slaa ni Mbowe kwaku mwambia agombee Urais mwaka 2010 haliyakuwa alijua atashindwa!Mbowe alisahau kuwa kilichomng'arisha kisiasa babu Slaa lilikuwa ni bunge!
Tokea Dr. Slaa, aje na ile list ya mafisadi papa, hakuna jipya tena alilowahi kulileta.

Dr. Slaa kabakia jina tu, siasa za Tanzania zimemkataa, kuendelea kugombea hiyo nafasi ni kupoteza muda na rasilimali.

Nakushauri upumzike katika nafasi yako ya ukatibu mkuu, muda wako umekwisha kuwika katika siasa za ushindani.

Siasa za kishindani zinahitaji ubunifu na uibuaji hoja zinazolengea kuleta changamoto ya maendeleo, Dr. slaa hajawahi kuibua hoja yoyote kuanzia nyakati zile, na amekua tu akiishi katikamiale ya mwanga wa nyota iliyozaliwa karne zile alizoibuka katika siasa za taifa hili.

Hakuna jipya toka kwa Slaa, Chadema wala Ukawa. Wagombea wa Ukawa ni wale wale, Kama sio slaa, basi ni Lipumba au Mbatia.

Watanzania wanahitaji kuona sura mpya katika majukwaa, sidhani kama nafasi ya urais, lazima iende kwa Slaa, lipumba au Mbatia, kwenye vyama vyao, kuna maelfu wa wanachama wengine wenye sifa za kugombea.

Ubinafsi wa watu hawa ni viashiria vya kidikteta, ambavyo kwa utaratibu wetu kama watanzania, hatuna ubinafsi wa viwango vya slaa, Lipumba na mbatia.

Tuwalazimishe Ukawa kuleta sura mpya kwa kuwakataa wagombea wake katika masanduku ya kura.

CCM all the way till 2025.
 
Mtakusanya habr kutoka kila sehem ila mwisho mtajua tu.... Ndoa, kutokujua chama yanakuhusu nn? We unayekijua nawe tangaza nia tukuone
 
Back
Top Bottom