Rais Magufuli tunaomba mulika TAZARA Mbeya, ni ubabaishaji mtupu, ukitaka kukata tiketi ya kesho wanakataa, ukiuliza sababu hawana, na hakuna muda rasmi wa kukata tiketi, kwa mfano jumamosi wanatakiwa kuanza kukata tiketi saa nne kamili asubuhi lakini mpaka muda bado hawajafika watu wanazidi...
Nipo Mbeya hapa aisee Mh Sugu anakubalika kupita maelezo yaani yuko close na wananchi anapiga kazi kimya kimya hataki promo kama za magambaz, hapa Sugu tu, nyingine kelele tu, heko MHESHIMIWA SUGU.
Waliowahi kuwa wanasali pale Msimbazi miaka ya 1980 watamkumbuka Fr Novartus Kaverlas, jamaa alikuwa mholanzi, alijua kiswahili na alikuwa mwandishi wa habari baadae akawa mhariri wa gazeti la kiongozi, huyu jamaa alieneza ukristu mbagala, mkuranga, kilimahewa na kibiti alikuwa anajichanganya...
Mmoja wana JF mwenye heshima kubwa M M Mwanakijiji amebadili gia angani, kwa maneno yake anasema Magufuli SAFI, naomba nijitokeze kumuunga mkono ndugu Mwanakijiji, bila shaka baraza la mawaziri la Magufuli limetusisimua wengi, na imani Mwanakijiji pia amelifurahia.
Huwezi kuwa kiongozi bora kwa kuponda watangulizi wako bali kutekeleza ahadi zako, ona mpaka sasa wiki ya tatu hata mashine za muhimbili bado hazijatengemaa, tabia ya kuponda inakunyima fursa muhimu ya kujikosoa wewe mwenyewe, unapoteza mwelekea kwa kuona madhaifu ya wenzako badala ya kusonga...
Nimepitia kitabu cha kanisa katoliki kinachoelezea historia za watakatifu, kwa nchi za Afrika Mashariki nimeona mashahidi wa uganda pekee kama karoli lwanga, mathias mulumba n.k, na kwa majirani zetu wa sudan nimemwona sista josephine bakhita ambaye baadaye aliishi italia, kongo nimemwona isdore...
Niseme wazi kuwa sifurahishwi na tabia ya baadhi ya viongozi wapya kuwaponda watangulizi wako, siamini kama unaweza kuwa kiongozi bora bila kuponda watangulizi wako, fanya utendaji wako bila kupondaponda wenzako, kuna tuliofurahishwa na uongozi wa huyo mstaafu, tuna imani amefanya makubwa ya...
"tuwavumilie watoto" JPM, "nimewaalika viongozi wa upinzani kujadili kuhusu katiba mpya" JK, uvumilivu wa kisiasa ni muhimu katika kuliunganisha taifa na kuleta maendeleo, Magufuli anapaswa kujifunza kwa JK
Tangu CCM ilivyompitisha Magufuli na CDM kumpokea Lowassa ndugu M M Mwanakijiji amekuwa na imani kubwa na CCM.
Sasa kwa vile Magufuli ameshinda (kama Mwanakijiji alivyobashiri) na kwa vile Mwanakijiji ni mchambuzi na mwanahabari wa viwango vya kimataifa, naomba ikimpendeza mh Magufuli amteue...
Wiki ya tatu sasa nchi tunajadili utawala, mara pm mara spika yaani mpaka sasa hakuna ishu ya national development, who cares? nani anafatilia kama michango hakuna mashuleni? nani anajua kama hakuna dawa hospitalini? yaani ni mwendo wa matamko na uteuzi, tunacheza na maendeleo nchi za kiafrika...
Lowassa ndiye atakayekuwa rais wa tano wa Tanzania, hali ndiyo ilivyo, mnaompenda Magufuli mfanyeni mwenyekiti wa CCM(opposition party to be), forget about Ikulu.
Wadau,
Itakumbukwa kuwa Mhe. Rais Kikwete amewahi kutunukiwa PHD na uprofesa na vyuo kadha wa kadha. Jambo la kusikitisha wanahabari hawataki kumu-address kama professor? wameshikilia Dr tu?
Ikumbukwe kuwa na Rais Profesa inatujengea heshima kimataifa..
Waliobahatika Kumsikia Lowassa Watakubali Kuwa Huyu Jamaa Ni Mwanamapinduzi, Hana Blahblah Nyingi Kama Washindani Wake, Anajiamini Sana, Aki Team Up Na Sumaye Inakuwa Kama Che-Guavara na Mao Tse Tung
Gazeti la Raia Mwema limewahi kuchapa makala ya MAYAGE iliyobeba kichwa cha habari NINGEMWONA LOWASSA JASIRI KAMA ANGEINGIA MSITUNI, mpaka leo sijasikia onyo lolote, tena mwandishi kakoleza Lowassa akifanya hivyo hatokuwa wa kwanza hata Nkuruzinza, Kabila na Kagame walifanya ivyo na kufanikiwa...
CCM leteni maji mtaani, nipeni ajira na Bachelor ya uchumi, ondoeni msongamano wa magari, mpeni mwanangu elimu bure, mpo hapo? kinyume na hapo kura yangu itakwenda kwa mzee wa mabadiliko Lowassa!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.