Hivi bado kuna watu wanasoma Education?

Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
11,045
15,380
Habari wanazuoni wa jukwaa la elimu
Najaribu kujiuliza tuu.......
Hivi bado kuna wanafunzi wameomba udahili wa Course za Education tena Arts?????

Na changamoto zote hizi kwenye Tasnia ya Ualimu tena ajira zilivyokuwa ngumu hasa kwa walimu wa sanaa na Sayansi ya jamiii bado kuna watu wanenda kupoteza muda na pesa kusomea ualimu???

Nikifikiria kuwa kuna watu ni mwaka wa 4 sasa ajira za ualimu hazieleweki, watu wamejiajiri katika ualimu lakini Holaaaaaa. Tusheni zenyewe ndo zimefutwa.

Bado kuna mtu anenda kweli kusoma mika mitatu BAED?????

Hivi kweli unataka uniambie hawaoni Course kama, IT, Procurement, BA, Marketing na nyingine za kawaida mapaka wakasome ualimu??

Mimi binafsi nawasikitikia sana. Japo hata hizo course nilizozitaja zina changamoto lakini sio kama za ualimu.

Najaribu kufikiria tuu. Naomba nisihukumiwe. Ila kama na wewe una fikra zako ni bora kutashirikishana
 
Hivi bado kuna wanafunzi wameomba udahili wa Course za Education tena Arts?????

Na changamoto zote hizi kwenye Tasnia ya Ualimu tena ajira zilivyokuwa ngumu hasa kwa walimu wa sanaa na Sayansi ya jamiii bado kuna watu wanenda kupoteza muda na pesa kusomea ualimu???
Mimi nawapongeza wanaokwenda ualimu. Kuna magumu lakini tukumbuke bado tunafyatua watoto, na watoto hawa watahitaji elimu. Au wenzangu kuna njia nyingine ya kupata elimu bila mwalimu.
 
Ualimu ingekuwa ni fani mbaya na hailipi wizara na vyuo husika wangeshaifuta lakini ipo kwa kuwa ina maslahi mapana kwa maendeleo ya taifa lolote duniani, think out of box.......Mabadiliko hayo ni ya muda tu lakin amini ipo siku ajira za walimu zitafunguliwa utataman ungesoma ualimu waache wakasome waje kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii .Kusubir ajira za serikal ni utumwa usiokifani .Elimu Elimu Elimu.
 
. infact kusoma ualimu wa arts kwa sasa hailipi labda baadae huko itatokea Trap yaan walimu wa arts watakosekana kabisa
 
Ualimu Sio tatizo Ila tatizo ni hii awamu ya jiwe Ila ikipita mambo yatakuwa powa acha madogo wakomae na ualimu
 
Kuna jamaa alimaliza pcm akapata division one , wazazi wake wakamtia chumvi kwamba ukienda ualimu unapata mkopo asilimia zote , akakubali msomi kushauriwa na wazaz ambao hata darasa la saba hawajafika , akawa yeye ndio muhubiri pale mtaani akiwaambia wenzake kwanini mnaenda masomo ya engineering hajira hakuna huko ,eti mkopo mtakosa ualimu ndio kila kitu , unaweza kujiendeleza ukiwa unasoma and all of nonsense , baada ya miaka kadhaa kumaliza akapangiwa huko mwisho wa nchi kijijini kabisa kabisa nyumba za walimu hakuna mtaa mzima msomi yeye , muda wote anajiona yuko targeted anahangaika kurudi dar es salaam huku amewaacha wazazi wanalia hali ngumu , wenzake aliomaliza nao sasa hivi wana drive anapishana nao barabarani wanampa lift sasa wenzake wametoka kinaisha anawa brainwash waache kazi private waombe serikalini eti kuna ajila ya kudumu hata ukiumwa mshaara bado unapata , nikasema jamaa huyu wazazi wake wamemharibu kupenda vitu rahisi , mwanaume pambana tengeneza maisha tafuta pesa weka akiba ukijua maisha yanabadilika usipende kua na hakika ya maisha , matajiri wa leo walianza kwa kuweka rehani pesa ndogo aliyonayo iliapate kubwa , maisga yaendelee angetaka kubweteka kufikilia future angeifukia chini pesa yake
 
interesting
 
Ajira za ualimu zipo nyingi sana tena za art maana serikali imeajiri walimu wa.literature.Labda ungefuatilia vizuri ungeeleza kuwa hata ukipata fursa private bado mshahara utakuwa mdogo labda ungeeleweka.Pia hii itaathiri walimu wote wa art kwa kuwa walimu wakiwa wengi ni rahisi kupunguziwa mshahara,ukigoma unafukuzwa kazi.Ila bado shule mpya ni nyingi na zinaendelea kujengwa mpya
 
Back
Top Bottom