Ugonjwa wa Masundosundo mwilini na sehemu za siri (Genital & Skin Warts)

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,025
1599131498745.png

Wengi wamekuwa wakiuliza juu ya ugonjwa huu; mjadala huu tunajadili kwa undani juu ya maradhi haya:

=========

UFAFANUZI WA KINA WA UGONJWA HUU
Ugonjwa kwa kitaalamu vinaitwa human papillom virus HPV,

Vinaambukizwa kwa mgusano wa damu au wa majimaji kutoka kwa mtu mwenye navyo hadi mwingine, hivyo kupelekea sababu mojawapo ya kuambukiza hivi vinyama kuwa ni ngono zembe.

Nasikia hakuna dawa ila mwili wenyewe unaweza kuviondoa vyenyewe na kupotea vyenyewe kabisa au huweza kusambaa sehemu mbali mbali za mwili na kuwa tatizo kubwa.

Hatari yake zaidi huweza leta kansa za aina mbalimbali kwa wanawake na wanaume, sababu hukwenda kubadilisha seli za mwili embu fikiria vikiota ndani ya mwili kwa ndani, basi tena ndio kansa tayari .

Chanjo ipo kwa ambao hajapata ugonjwa huo na kwa watoto wenye umri wa miaka 10 hadi 12, sijui hiyo chanjo kwa hapa TANZANIA au Afrika mashariki ipo?!

Kuhusu Tiba ya hivi vidude kwa njia ya asilia au namna nyingine yoyote; fuatilia mjadala huu...

Masundosundo au vigwaru au Genital warts ni vinyama laini vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya siri. Vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo [urethra], vulva, shingo ya kizazi [cervix], au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake.
Huu ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana [sexually transmitted infection(STI)].

Visababishi
Ugonjwa wa masundosundo husababishwa na jamii ya virusi wanaoitwa Human papilloma virus (HPV). Kuna zaidi ya aina 70 tofauti za virusi wa HPV ingawa si wote wanaosababisha masundosundo kwenye maeneo ya siri [genital warts]. Baadhi ya aina nyingine za HPV husababisha masundosundo kwenye ngozi inayozunguka sehemu nyngine za mwili kama vile kwenye mikono au miguu.

Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa baadhi ya aina za virusi wa HPV pia husababisha saratani ya shingo ya kizazi [carcinoma of the cervix] kwa wanawake au saratani ya njia ya haja kubwa [anal cancer] kwa jinsia zote mbili. Aina hii ya virusi hujulikana pia kama high-risk HPV.

Pamoja na kwamba ugonjwa wa masundosundo kwenye maeneo ya siri umejitokeza kwa kasi kubwa hasa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI, watu wengi waliopatwa na ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote zile. Kwa mfano, kwa wanawake, virusi wa HPV wana uwezo wa kusambaa mpaka maeneo ya ndani kabisa ya kuta za uke au shingo ya kizazi [cervix] bila kuonekana wala kuhisiwa kwa urahisi.

Kama tulivyotangulia kueleza hapo awali, maambukizi ya HPV husambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni. Mara baada ya kuambukizwa, huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi miezi 6 kwa masundosundo kuwa dhahiri, ingawa baadhi ya wagonjwa wanaweza kukaa hata miaka kadhaa bila kuwa na dalili yeyote ile. Aidha imeonekana pia kuwa si kila mtu anayejamiina na aliye na maambukizi ya HPV au mwenye masundosundo anaweza naye kupata ugonjwa huu.

Vihatarishi
Watu walio katika makundi haya wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupatwa na masundosundo kwenye maeneo ya siri
• Wenye wapenzi wengi
• Kufanya ngono isiyo salama/ ngono zembe
• Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo
• Watumiaji wakubwa wa sigara pamoja na pombe
• Kupatwa na maambukizi ya virusi wa herpes na wakati huo huo kuwa na msongo mkali wa mawazo
• wajawazito
• kuwa na upungufu katika mfumo wa kinga mwilini kwa sababu ya magonjwa mbalimbali au kwa sababu ya matumizi ya dawa fulani fulani kwa watoto wadogo, ukiona mtoto amepata masundosundo basi ni vema kufanya uchunguzi ikiwa amewahi kubakwa au kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.

Dalili za masundosundo [genital warts]
Masundosundo [genital warts] huonekana kama vioteo laini vinavyojitokeza juu ya ngozi ingawa wakati mwingine vinaweza kuwa vidogo mno kiasi cha kutoweza kuonekana vizuri kwa macho ya kawaida.

Kwa wanaume, vioteo hivi hutokea zaidi kwenye uume, ngozi ya pumbu, eneo la mitoki, mapajani pamoja na maeneo ya kuzunguka nje ya njia ya haja kubwa au ndani yake; wakati kwa wanawake hutokea ndani ya uke au njia ya haja kubwa, nje ya uke au ngozi ya nje kuzunguka njia ya haja kubwa, au ndani ya uke kuzunguka eneo la shingo ya kizazi.

Kwa wale wanaopenda kufanya ngono ya mdomoni [oral sex], wanaweza kupatwa na masundosundo/genital warts kwenye maeneo ya kuzunguka mdomo, lips, kwenye ulimi na hata kwenye utando unaozunguka koo.

Dalili nyingine ni kama vile mgonjwa kujihisi kukosekana kwa hisia [kufa ganzi] maeneo yaliyozungukwa na masundosundo, kwa wanawake kuongezeka kwa utoko/ uchafu sehemu za siri, kuwashwa sana maeneo ya siri na wakati mwingine kutokwa na damu ukeni mara baada ya tendo la ngono. Hata hivyo dalili hizi hutokea mara chache sana.

Wanawake wengi vijana wanaojihusisha na vitendo vya ngono [sexually active] huambukizwa sana ugonjwa huu lakini wengi wao hupona bila hata kuhitaji matibabu, wakati wanaume wanaoambukizwa, wengi wao huwa hawaoneshi dalili zozote za ugonjwa ingawa wanaweza kuwaambukiza wenzi wao bila ya wao kujua.

Uchunguzi na vipimo
Kwa wanawake, uchunguzi wa ugonjwa wa masundosundo/genital warts hujumuisha uchunguzi wa maeneo ya nyonga [pelvic examination] ambapo daktari huchunguza eneo hilo kwa kutumia vifaa maalum vinavyomuwezesha kuona uwepo wa masundosundo na wapi vilipo. Wakati fulani, kunyunyizia dawa yenye tindikali ya acetic acidhusaidia kufanya masundosundo kuonekana kwa urahisi zaidi. Wakati mwingine daktari anaweza pia kufanya kipimo cha pap smearkwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi [kwa vile kama tulivyoona hapo awali, zipo aina fulani fulani za HPV ambazo husababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake].
Kwa wanaume, uchunguzi wa maeneo ya siri ni muhimu sana ili kufahamu kama kuna masundosundo au la.

Matibabu
Ni vema genital warts zitibiwe hospitali na daktari; haishauriwi kutumia dawa za kununua kujitibu mwenyewe kwa vile kuna uwezekano mkubwa wa kuchanganya aina ya dawa zinazotumika maalum kutibu aina nyingine za warts kwa ajili ya kujitibu genital warts.

Matibabu ya genital warts hufanyika hospitali kwa mganga kuondoa vioteo juu ya ngozi iliyoathirika au kwa kutumia dawa utakazoandikiwa na daktari na kuelekezwa namna ya kuzitumia mwenyewe nyumbani kwa siku kadhaa mpaka majuma kadhaa. Dawa zinazotumika ni pamoja na Podophyllin na podofilox, Trichloroacetic acid (TCA) au Imiquimod

Ukiachilia mbali matumizi ya dawa, masundosundo yanaweza pia kutibiwa kwa njia ya upasuaji mdogo kama vile kwa kuvikata, au kuvimaliza kwa kutumia njia ya baridi/barafu [cryosurgeryLaser therapy].

Matibabu ya masundosundo, kama yalivyo matibabu ya magonjwa mengine yanayosambaa kwa njia ya ngono, ni lazima yahusishe pia tiba kwa mwenza wa mgonjwa. Wakati mwingine hata kama utajihisi huna dalili za waziwazi, ni vema kumuona daktari ili uchunguzwe na kutibiwa kuepusha kusambaza ugonjwa kwa watu wengine au kuachia ugonjwa mpaka ukakuletea madhara zaidi. Aidha matibabu yanaweza kuhitaji kurudiwa rudiwa mara kadhaa mpaka masundosundo yatakapokuwa yametoweka kabisa.

Kwa wanawake ambao wametibiwa genital warts na kupona au wale ambao wamewahi kuwa na wenza waliowahi kuugua ugonjwa huu, wanashauriwa sana kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa shingo za kizazi [pap smear ni vema kufanya pap smearwalau kila baada ya miezi 3 mpaka 6 tangu kupata matibabu ya awali ya genital warts. Na kwa wale watakaonekana kuwa na dalili za awali za saratani ya shingo ya kizazi, hawana budi kufanyiwa uchunguzi na tiba zaidi li kuepusha uwezekano wa kupata saratani kamili ya shingo ya kizazi.

Baadhi ya nchi zilizoendelea zina utaratibu wa kuwapatia chanjo ya kuwakinga wanawake vijana au wasichana wadogo wenye umri kati ya miaka 10 mpaka 25 dhidi ya maambukizi ya HPV. Chanjo hii hutolewa hata kwa wale ambao wamewahi kuugua genital warts ingawa imeonekana kuwa ufanisi wa chanjo ya HPV dhidi ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kwa wale waliowahi kupatwa na genital wartszilivyosababishwa na high risk HPV huwa ni mdogo ukilinganisha na wale ambao hawajawahi kuugua lakini wapo katika hatari ya kupatwa na ugonjwa huo.

Hata hivyo, pamoja na kuwa umetibiwa, bado unaweza kuwaambukiza wengine virusi hawa wa HPV hivyo ni muhimu kuchukua hatua za kujikinga wakati wa kujamiiana.

Madhara ya masundosundo
Kama tulivyoeleza hapo awali, baadhi ya aina fulani za HPV wameonekana kusababisha saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya vulva. Kiujumla, HPV ndiyo kisababishi kikuu cha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wengi. Tofauti na wanawake, ifahamike pia kuwa aina za HPV zinazoweza kusababisha genital warts kwa wanaume ni tofauti kabisa na zile zinazoweza kusababisha saratani ya uume [cancer of the penis] au saratani ya njia ya haja kubwa [anal cancer].

Kwa baadhi ya wagonjwa, masundosundo yanaweza kuwa mengi na makubwa sana kiasi cha kuhitaji matibabu ya muda mrefu na ghali zaidi pamoja na ufuatiliaji wa kina.

Kinga dhidi ya genital warts
Njia mojawapo ya uhakika kabisa ya kujiepusha na ugonjwa wa genital wartspamoja na magonjwa mengine ya ngono/zinaa ni kujiepusha na matendo ya ngono na zinaa kabisa. Lakini kwa wale ambao ni ngumu kufanya hivyo, wanaweza kupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa huu kwa kujihusisha kingono na mwenza mmoja tu ambaye una uhakika kuwa hajaambukizwa wala hayupo katika hatari ya kuambukizwa magonjwa haya.

Tofauti na magonjwa mengine ya zinaa, matumizi ya condom hayana uhakika wa asilimia mia moja katika kukukinga dhidi ya HPV kwa sababu virusi wa HPV au hata masundosundo yanaweza kuwa nje nje kwenye ngozi ambayo uwezekano wa kugusana ni mkubwa. Pamoja na hayo, bado condom inaweza sana kupunguza hatari ya kuambukizwa masundosundo ikiwa tu itatumika vema na inashauriwa kuitumia mara zote unapokutana kingono na mwenza usiye na uhakika naye.

Tukumbuke kila wakati kuwa HPV inaweza bado kuambukizwa kwa mtu hata kama mwenza hana masundosundo yanavyoonekana au hana dalili zozote zile.

Ikiwa kuna uwezekano, ni vema kwa wanawake wote wenye umri wa miaka kati ya 9 mpaka 26 kupata chanjo dhidi ya virusi wa HPV ili kuzuia uwezekano wa kuambukizwa virusi hao ambao hatimaye husababishasaratani ya shingo ya kizazi.

hpv1.gif
6056155_f260.jpg

read more ;

http://www.medicalnewstoday.com/articles/246670.php

Human Papilloma Virus Natural Cure Herbal Treatment for HPV Genital Warts Herbs

The deadliest silent killer, Human Papilloma Virus aka HPV(papillomavirus)

americanhealthjournal.com

Magazine_20130503_200210_01.jpg

---
Habari rafiki, natumaini mnaendelea vizuri leo napenda nizungumzie tatizo la kutokewa vinyama katika sehemu za siri na sehemu mbalimbali za mwili, (Masundosundo /vigwaru /genital warts & skin)
~MASUNDOSUNDO /VIGWARU /GENITAL WARTS & SKIN NI NINI?

~NI vinyama Laini vidogovidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando Laini unaozunguka maeneo ya sehemu za siri, vinyama hivyo vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo (urethra), maeneo yanayozunguka haja kubwa na sehemu mbalimbali za mwili,
~Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia ya kujamiiana (SEXUAL TRANSMITTED INFECTION) STI)

CHANZO CHA TATIZO HILI
~Ugonjwa wa Masundosundo husababishwa na virus waitwao HUMAN PAPILLOMA VIRUS ( HPV) hata hivyo Kuna Aina tofauti za virus wa HPV hivyo sio wote wanaosababisha tatizo hili kwani Kuna ambao wanaosababisha Masundosundo katika sehemu tofauti kama vile mkono, mgongoni, mguuni nk pia HPV huweza kasababisha saratani ya shingo ya kizazi(CARCINOMA OF THE CERVIX) kwa wanawake, na pia huweza kusababisha saratani ya sehemu ya haja kubwa (ANAL CANCER) kwa jinsia zote mbili
~Ugonjwa huu wa Masundosundo umejitokeza kwa kiasi kikubwa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI hivyo watu wenye wapenzi wengi, wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo na haja kubwa, wajawazito, watumiaji wakubwa wa sigara na pombe, watu wenye upungufu wa kinga mwilini wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu.

DALILI ZA MASUNDOSUNDO
~mgonjwa wa tatizo hili hutokewa na vinyama Laini vidogovidogo vinavyoota kwenye katika maeneo tofauti (MFANO HALISI TIZAMA KATIKA PICHA) ingawa wakati mwingine huwa ni vidogo kiasi cha kutoweza kuonekana kwa njia ya kawaida.
~mgonjwa kupata ganzi maeneo yaliyozungukwa na Masundosundo
~kutokwa na uchafu mzito sehem za siri na kuwashwa kupita maelezo
~kutokwa damu ukeni mara baada ya kufanya tendo la ndoa
NOTED :mwanaume huwa anachelewa kupata dalili na huwa na uwezekano mkubwa wa kuambikiza wenza wao

MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA UGONJWA HUU
~matibabu ya tatizo hili hupatikana kirahisi iwapo tatizo halijachelewa kupatiwa tiba, matibabu hutolewa kwa kufuata utaratibu wa Majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali, matibabu hayo huweza kuwa ya kuviondoa vinyama kwa kufanya operations au kutumia dawa, hata hivyo njia ya operation sio nzuri sana kwasababu huweza kutengeneza madhara zaidi na uwezekano mkubwa wa kupata kansa hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa ambazo zitatibu na kuondoa tatizo hilo na mgonjwa kupona kabisa ila cha kuzingatia ni kwamba ugonjwa huu ni wa kuambikiza hivyo inashauriwa wenza wote kupata matibabu hata kama atajihisi hana dalili yoyote ni vyema akafanya vipimo ili kujihadhari kabla ugonjwa haujaleta madhara zaidi.

~Waswahili wanasema bora kinga kuliko matibabu hivyo ni vyema ukajiepusha na ugonjwa huu kwa kuepuka yafuatayo
EPUKA KUWA NA WAPENZI WENGI
EPUKA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
ACHA ORAL SEX UKISHINDWA BASI KUWA NA MPENZI MMOJA TU AMBAYE NDIO UNAWEZA KUMNYONYA SEHEMU ZAKE ZA SIRI ZINGATIA MAPENZI UJUZI LAKINI AFYA YAKO NI MALI ZAIDI WADADA/WAKAKA WENGI MMEKUA MKITAKA KUWARIDHISHA KILA MNAOKUTANA NAO KIMWIL KWA KUWANYONYA SEHEMU ZA SIRI KITU AMBACHO KINAKUWEKA KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU NA KANSA YA KOO.

EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA, SIGARA NA POMBE KUPITA KIASI
NOTED :NDUGU RAFIKI ugonjwa huu una madhara makubwa unaweza kusababisha kansa ya kizazi, kansa ya uume, kansa sehemu ya haja kubwa NK hivyo hakikisha unapata matibabu ya uhakika iwapo una tatizo hili au ikiwa hauna jitahid kujiepusha na vihatarishi vya ugonjwa huu

Kwa maoni na ushauri Niandikie whatsapp/sms
+255 714 206 306
Blog: Tovuti ya Uelimishaji na Ushauri wa magonjwa sugu, kisukari, shinikizo la damu, kansa, ugumba, upungufu wa nguvu za kiume n.k.
Email : khalidgugu@gmail.com
Makala hii imeandaliwa na
Khalid Gugu
USISAHAU KUSHARE, KUCOMENT, KULIKE
---
Masundosundo ni ugonjwa gani?

Masundosundo ni ugonjwa wa ngozi unaosababisha uoto mgumu kwenye ngozi wenye umbo mithili ya mboga iitwayo koliflawa (cauliflower). Ugonjwa huu husababishwa na kirusi kiitwacho HPV-Human Papilloma Virus.
phototake_rm_hand_warts.jpg

Nini husababisha masundosundo kwenye ngozi?

Chanzo cha ugonjwa huu ni kirusi kiitwacho HPV-Human Papilloma Virus. Kuna aina zaidi ya 100 ya kirusi HPV, aina nyingi ya HPV huwa na madhara madogo kwa binadamu. Baadhi ya aina za kirusi hichi huweza kusababisha kansa mfano kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake.(type 6,11,16,18)

Kirusi hichi humwingia mwanadamu kupitia sehemu za ngozi zenye mikato (broken skin).

Aina za masundosundo:

Kuna aina nyingi za ugonjwa huu ila kwa urahisi tunaweza kuzigawanya katika aina mbili kuu; masundosundo ya ngozi(skin warts) na masundosundo ya sehemu za siri(genital warts).

Masundosundo ya ngozi huwa na dalili kwenye ngozi ya kawaida na masundosundo ya sehemu za siri huambatana na uoto sehemu za siri.

916058-16464641-a72d-4abf-ad8c-d5dcd90162ae.jpg

Tiba ya misundosundo:

Ukiachana na mwonekano wa ngozi, ugonjwa wa misundosundo hauna madhara kwa binadamu. Baadhi ya aina ya kirusi HPV husababisha kansa ila uoto wa misundosundo hauna madhara.

Tiba yake ni kuondoa uoto huu kwa njia mbalimbali. Dawa aina ya Salicylic acid husaidia kuondoa masundosundo kwenye ngozi. Pia tiba ya cryotherapy ambayo uoto wa masundosundo hugandishwa kwa gesi yenye joto dogo.

Kinga ya misundosundo:

Chanjo ya kirusi HPV itwayo Gardasil imetengenezwa kwa ajiri ya kinga ya kansa isababishwayo na baadhi ya aina ya kirusi HPV.

Pia ethanol 90% husaidia kupunguza maambukizi ya kirusi HPV kwenye ngozi.

Dr Luhaja Nginila,MD
 
Symptoms

In females, genital warts appear in and around the vagina or anus or on the cervix. In males, they appear on the penis, scrotum, groin, or thigh. Genital warts can be raised or flat, small or large. Sometimes they're clustered together in a cauliflower-like shape. Most of the time, they're flesh-colored and painless. Sometimes, the warts are so small and flat that they may not be noticed right away.

It may take several months or years after infection for symptoms to appear - if there are symptoms at all.

In females, the virus can lead to changes in the cervix that may lead to cancer, so it's important that it is diagnosed and treated as soon as possible. Males infected with HPV can also be at risk for cancer of the penis and the anus.

Genital warts are transmitted through sexual contact (anal, oral, and vaginal) with an infected person, and warts can appear within several weeks or months afterwards.

The virus is passed through skin-to-skin contact, but not everyone who's been exposed to the virus will develop genital warts.

Prevention
A vaccine for females 9 to 26 years old is approved to prevent HPV infection, which causes most cervical cancers and genital warts. The vaccine, called Gardasil, is given as three injections over a 6-month period. It doesn't protect females who've already been infected with HPV, and doesn't protect against all types of HPV, so be sure your daughter gets routine checkups and gynecologic exams. If you have questions about the vaccine, talk with your doctor.

Because genital warts are spread through sexual contact, the best way to prevent them is to abstain from having sex. Sexual contact with more than one partner or with someone who has more than one partner increases the risk of contracting any STD.

When properly and consistently used, condoms decrease the risk of STDs. Latex condoms provide greater protection than natural-membrane condoms. The female condom, made of polyurethane, is also considered effective against STDs.

Using douche can actually increase a female's risk of contracting STDs because it can change the natural flora of the vagina and may flush bacteria higher into the genital tract.

A teen who is being treated for genital warts also should be tested for other STDs, and should have time alone with the doctor to openly discuss issues like sexual activity. Not all teens will be comfortable talking with parents about these issues. But it's important to encourage them to talk to a trusted adult who can provide the facts.

Treatment
Though there's no cure for an HPV infection, the genital warts can be treated and removed with prescription medication or other medical procedures, such as freezing or laser treatments.

Because the HPV remains dormant in the body, genital warts may reappear at any time after treatment. Those who have had one outbreak of genital warts still carry the virus and can infect others. Someone who has had HPV can also get a new HPV infection from another partner.

Getting Help
If your teen is thinking of becoming sexually active or already has started having sex, it's important to talk with him or her about it. Make sure your teen knows how STDs can be spread (during anal, oral, or vaginal sex) and that these infections often don't have symptoms, so a partner might have an STD without knowing it.

It can be difficult to talk about STDs, but just as with any other medical issue, teens need this information to stay safe and healthy. Provide the facts, and let your child know where you stand.

It's also important that all teens have regular full physical exams - which can include screening for STDs. Your teen may want to see a gynecologist or a specialist in adolescent medicine to talk about sexual health issues. Community health organizations and sexual counseling centers in your local area also may be able to offer some guidance.
 
HPV has more than 130 serotypes/clades, can be grouped into 2 categories based on their oncogenicities:

1. Highly oncogenic-responsible for cervical CA (type 16,18,32,33,35,43,55 etc)
2. Low oncogenic-responsible for all forms of warts (type 6 & 9)

Haven't seen any literature that points any ability of the low oncogenic subtype transforming to high oncogenic and ultimately to malignancy but who knows anything can happen in medicine.

WARTS-hyperkeratinization AgNO3 can also be used if the d'se hasn't yet advanced (applicable to oral warts as well). I have looked for podophylin but it seems not to be found in any of the pharmacies in town.

PREVENTION can also be through the use of cervarix (50-75,000/=) vaccine now available in Tanzania but this targets only the high oncogenic subtypes. Vaccine works mostly to those who havent yet engaged in sexual activities tho' havent heard of the efficacy of it to those who are already sexually active.

The body has capabilities of fighting the disease within two years of clinical period. There is no 100% cure to warts, as the disease goes into episodes of remission even after surgical procedures.
 
Hivyo "vinyama" ni more serious kuliko jinsi watu wengi wanavyovichukulia.

Userious wake unatokana na fact kwamba uwepo wake huashiria uwezekano wa kutokea kansa baadae.

Matibabu yake ni ya aina tatu.
1. Dawa za kupaka kuua virusi vinavyosababisha

2. Kuziunguza kwa umeme (surgical)

3. Kufuatilia iwapo kuna kansa inayojitokeza.

Iwapo vinajitokeza kwa mwanamke, ni MUHIMU mwanamke huyo afanyiwe vipimo vya kansa ya shingo ya uzazi.
 
Majipu au uvimbe na chunjua.

Saga vitunguu saumu vibichi na funga vilivyopondwa kwenye sehemu ya jipu, uvimbe au
Chunjua mara mbili kwa siku na gandamiza. Anza matibabu haya mapema iwezekanavyo.

Dawa ingine ya Tiba Mbadala jaribu hii
Nunua kitunguu swaumu Kimoja kizima.Menya

chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikisha sagika changanya na maji ya uvuguvugu kidogo

kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu na uvimeze.

Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza tapika.
(Mara chache

sana hutokea kutapika)
Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida. Jaribu kutumia kila siku Asubuhi kabla ya kula

kitu tumia hii dawa mpaka hapo utakapo pona maradhi yako kisha uje hapa unipe Feedback.@
Android
 
Wakuu nilishawahi pata hilo tatizo zamani sana wakati niko highschool.

Sasa nilikua nakaa kwa mjomba huko nchi za watu. Nikaenda kwa daktari (nilikua miaka 17 nafkiri) akaniambia the only treatment ni laser, amabyo bila health insurance ni kama 1000 dolars back then. Dah nitamwambieje uncle au mshua. Nikakaa kitu ikawa inakua mpaka inataka kuanza kuziba mrija wa mkojo.

Bahati nzuri akaja mtanzania mmoja na design akagongea malazi kwa mjomba kwa kama mwezi hivi akisoma mazingira, nikamfungukia bwana. Maana nilishaanza kukonda na mawazo na hata shule kitabu hakipandi. Nilivyomwonyesha aisee kitu ilikua tayari inaspread akaniambia katafute papai bichi halafu upakae utomvu wake na uchome chome na pini!!

Sasa mtoni unapata wapi papai bichi? Bahati nzuri nyumba kama ya 5 hivi kwa street palikua na mti wa mipapai sikumbuki niliuoneje. Nikaenda kuwaomba kuwa nafanya scientific study. Wakanigee nikaanza tumia kama nilivyoelekezwa. Maajabu siku ya tatu kitu ilipote yoooote mpaka leo many years have passed.

Story yote hio ni ili mniamini tu! Utomvu wa papai bichi ulinitibu mimi HPV! Halafu hivi kweli si niifanyie research hii kitu!!
 
kuna dawa nyingi on line ya kuviondoa ziko katika cream form au solutions lakini hospital nyingi za Bongo wanatumia pencil za kuchoma ambazo zina usumbufu kuapply mimi niliagiza India kwa Ebay na ilifika dawa ya kupaka within 7 days na ilicost kama TZS15,000 na imesaidia kufuta usoni.Lakini vinasababishwa na virus walioko katika damu kwa hiyo vinaweza ota sehemu nyingine ya mwili
 
kama wewe ni jasiri kikate mapema kikiwa hakijakua, yaani kikiwa hakijtapakaa, tumia kiwembe kipya na kikali, kikate kwenye shina kabisaa. kisha futa damu na kitambaa kisafi au tissu , utupe mbali hiyo tissue au kitambaa, sehemu iliyobaki na kidonda paka asali au kitunguu saumu au paka chochote cha asili ambacho ni strong acid.

Ushauri wa kutumia dawa ya kunywa vilevile ni mzuri yaani kama ipo kwenye damu ijitibie kabisaa, hivyo kunywa vitunguu saumu au asali plus mdalasini kama alivyoshauri FaizaFoxy na MziziMkavu.

huu ugonjwa ni serious sana kuliko watu wanavyochukulia, ni mojawapo ya visababish vya kansa nyingi kwa binadamu, kansa ya kizazi hadi throat kansa. tiba ya mapema ni bora kuliko kuchelewa.
 
Last edited by a moderator:
kuna dawa nyingi on line ya kuviondoa ziko katika cream form au solutions lakini hospital nyingi za Bongo wanatumia pencil za kuchoma ambazo zina usumbufu kuapply mimi niliagiza India kwa Ebay na ilifika dawa ya kupaka within 7 days na ilicost kama TZS15,000 na imesaidia kufuta usoni.Lakini vinasababishwa na virus walioko katika damu kwa hiyo vinaweza ota sehemu nyingine ya mwili

Kituga, inaitwaje hiyo dawa?
 
Mkuu pole sana.

Tiba mbadala ninayoifahamu mimi na iliniponya nilipokuwa secondari ni utomvu wa ile miti (vines) inayopandwa kama hedge na ukikata kitawi kinatoa utonvu mweupe. Huu mti siujui jina lake lakini nadhani wakuu MziziMkavu , FaizaFoxy et al. wanaweza kutusaidia. Hii tiba inafanana na tiba ya utomvu wa papai bichi aliotoa mkuu Nyamgluu

Hivi karibuni swahiba wangu nae aliathiriwa na haya maradhi. Daktari akamuelekeza kununua Dr. Scholl's Wart Remover. (Hii sio dawa ya prescription ni off-the-counter). Aliweka hizi plasta na katika kipindi cha wiki moja zile warts zilidondoka mpaka mizizi. Active ingredient ya hii wart remover ni Salicylic Acid (40%). Sasa kama huwezi kuipapata hii Dr. Scholl's Wart Remover nadhani unaweza kusaga asprin ambayo ina hii Salicylic Acid.

Hapa pa kusaga asprin naomba tuwaulize madaktari ushauri wao.
Riwa watu8 georgeallen AshaDii ZeMarcopolo Mupirocin, et al.
 
kiongozi unakunywa dozi hiyo mara ngapi kwa siku? na inatakiwa unywe kwa siku ngapi?
Kula kila siku Asubuhi unapo amka kabla ya kula kitu kisha ukae baada ya saa moja ndio waweza kula chakula fanya hivyo kwamuda wa siku 15 au mpaka upone kisha uje hapa ulete maendeleo yako.Na pia unaweza kukisaga kitunguu saumu kingine ukakiweka hapo penye ugonjwa pia inasaidia kuondowa hayo maradhi fanya kila siku asaubuhi na jioni mpaka upone.
 
nimevutiwa na hii topic...mim nilishawah pata genital warts nikatumia dawa inaitwa podosal paint vikaisha..je ninaweza nikawa kwenye hatar ya kupata kansa ya kizaz?
 
Mada nzuri mimi nimewahi kupata kwenye vidole vya mikono na nilitumia dawa iitwayo SILVER NITRATE Ni kama penseli unapaka tu baas na ukishapaka usiguse maji hii ilinisaidia tena kwa haraka kwani ndani ya nwez 1 vilikua.vimeisha kabisa na havijanirudia tena! sijui hata nilivipata vip jaman ila nakushauri uitafute hii dawa ni kiboko ndugu...kichaga tunaita Nzindo ambapo nliona waliokua navyo walikua wanapaka mti fulani hivi unatoa maziwa...
 
Kwanza nashukuru kwa kutambua mchango wangu, pili samahani kwa kuchelewa kujibu coz muda mwingi natumia simu ambayo ni ngumu kuona notification.

katika maitbau ya kisasa tunatumia SILVER NITRATE pencil ambayo unachovya kwenye maji kile kichwa cha kuandika na kugusisha au kupaka kwenye kiwart ulichonacho. kumbuka hii inaunguza sasa basi kabla ya kupaka kwanye kiwarts chako paka mafuta ya mgando kuzunguka kile kiwart nipo upake maji ya silver nitrate ili kuzuia ngozi nyingine isiungue. baada ya kupaka subiri mpaka msaa sita ndipo uoshe na maji, baada ya hapo utaona kiwart chako kinyeyuka haraka iwezekanavyo. kama hakitoki rudi tena siku ya pili hadi kiishe. lakini mara nyingi huondoka ndani ya siku moja.

Pia waweza tumia podophylline ambayo nayo matumizi yanafanan kama silver nitrate lakini hii hairuhusiwi kwa wanawake wajawazito.
All the best mkuu
 
Naomba kujua vinyama hivi ni sawa na uvimbe unaotokea nyuma ya sikio baada ya kutoga? naomba kufaham tafadhali
 
Back
Top Bottom