Fangasi sugu sehemu za siri

sanga misuka

Member
Aug 24, 2017
38
42
Habari great minds,
Nina tatizo la fangasi sugu sehemu za siri kwa miaka zaidi ya 4, huwa linanisumbua miwasho japo kuna muda linapungua na kupotea.

Nimeshatumia kila aina ya dawa zikiwemo za kupaka na kumeza, na kufuata maelekezo yote lakini tatizo bado lipo.

Kwa mikoa niliyokuwa naishi Mwanza tatizo lilikuwa la kuja kwa muda na kupungua hadi kupotea kwa mda kutokana na msimu.

Lakini kwa sasa nipo Dar tatizo limekuwa kubwa sana hadi kuleta michubuko ya ngozi sehemu za siri hii kutokana na joto kali,

Naombeni kwa aliyewahi kupatwa na fangasi sugu na akapona kwa dawa zingine tofauti na za kumeza na kupata za hospitalini maana nimeenda hospitali nyingi zikiwemo za binafsi.

Naomba anisaidie niweze kupona maana kuna muda inanipa shida hadi kutembea.

Nashukuru sana.
 
Fua boxer & badilisha walau mara mbili kwa siku

Ukishaoga kausha maji kwa kutumia taulo safi kwenye sehemu zako za siri (pumbunyo & kwenye pachupachu baina ya mapaja)

Tumia anti-fungal creams zenye clotrimazole kwa muda wa siku kumi na nne mfululizo (asubuhi na jioni)
 
Tunaomba picha picha picha tukukague vizuri Madaktari hizo fangasi zinaonekanaje tukusaidie km unaona aibu hapa tuma PM
 
Ni kwamba unaingiza kwenye shimo lilelile linalokusababishia fangasi.
Tibu kwanza shimo kisha jitibu
Badilisha mtindo wa maisha. Tofauti na hapo utasumbuka na huo ugonjwa milele
 
Ni kwamba unaingiza kwenye shimo lilelile linalokusababishia fangasi.
Tibu kwanza shimo kisha jitibu
Badilisha mtindo wa maisha. Tofauti na hapo utasumbuka na huo ugonjwa milele
Shimo lipi unazongumzia?
 
Pima na HIV kwanza ndo uendelee kutafuta tiba ....hiv na fungus ni mtu na mdogo wake pima kwanza ukiona huna......ndo endelea kutafuta dawa bila hofu......
 
Dawa ya kwanza ni maji

Je! Unaogea maji gani?
Je! Boxer unazovaa unafua baada ya mda gani?
Je! Unanyoa msitu baada ya mda gani?
Je! Unatumia mafuta gani kujipakaa?
Je! Unatumia chemikali yoyote kujipakaa?
Je! Unaoga kila baada ya mda gani kwa siku?
Je! Unaoga mara ngapi kwa siku?
Je! Unaoga maji gani ya bomba, ya MTO au ya mvua?
Je! Unatumia sabuni gani kuogea?
Je! Unavaliana nguo za ndani km boxer na mtu mwingine?

Maswali ni mengi hayo ni baadhi tu
 
Hivi unaujua mziki wa Dettol wewe? Ile inachoma sasa unataka umfanye nini mwenzio aongezee tatizo?
Hiyo ndio dawa zingine atamaliza pesa muhimu awe amehakikisha kuvumilia kwa sekunde 3-5 baada ya hapo Kuna upepo mzuri utampuliza na muwasho utapotea kabisa baada ya masaa ataanza kubandua ngoz ambayo n useless iliokuwa inasababisha muwasho.

Muhimu ajikaze na ahakikishe amefunga mlango kama nyumba haina bord juu aangalie asije akarukia kenchi.

Muhimu ajikaze Dettol ya maji n msaada mkubwa wengi imewaokoa fast and clear na gharama nafuu matumizi siku chache
 
Dettol bila kidonda inaunguza sasa sipati picha kwenye kidonda tena Ile ya maji ni balaa atalia kikwao
 
Pole mazingira ya joto fangasi huwa wanastawi,hakikisha unafika ospital wakupe za kupaka na kunywa,ukianza dozi usiache mpaka iishe,badili boxa kila siku.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom