Shajara ya mhunzi: Tusifukue makaburi ya zamani huku tukisakafia mapya

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,640
697,940
Mhunzi hakosi kuwa na Shajara... Anaweka kumbukumbu zake vyema! Vifaa vyake vikiwa ni nyundo koleo na fuawe daima mhunzi mahiri atakumbuka kwa hakika kabisa mwaka juzi alifua nini na kumpa nani... Ukitaka ulinganisho ukitaka mfanano atakutolea Shajara lake ujichagulie ujipimie....!!!

Daima hakosi cha jana kuwa cha juzi na cha majuzi kukifanya cha mtondogoo... Ni umahiri wa hesabu wa kumbukumbu jadidi

Kuna wakati nami nataka nitangaze nia ya kuacha kibarua changu cha kuagua ili niunge mkono juhudi!!! Lakini nikichungulia kwenye Shajara la mhunzi nasita.. Nashindwa kutamalaki... Kufanya mafunuo yangu yajulikane kwa wana kaya watukuka sana...

Hizi ni sawa na porojo tu za wanamageuko lakini kumbe zina ujumbe! Kwamba niambie nani kamdhulumu kamanda mafikra pumzi yake!? kaiachia kaya yake jinamizi la sononeko sononi na upweke wa milele... Lakini si afadhali huyu imejukana wazi mustkabali wake? Vp kuhusu mdogo wetu, mtoto wetu rafiki yetu mJF jamaa yetu Ben? Peke yake na .. Huyu anaweza kuwa ni kiwakilishi wa ile mizoga kwenye sandarusi.... God is watching...!!! Kaka mtukutu Tundu kaponea shimo la tewa..... Wengi wameikosa hiyo bahati ya kipekee na nadra kabisa

Basi acha tu niunge juhudi hapa hapa nimeona ya bandari (japo kuna fiksi zake) nimeona ya makinia ( nimehuzunishwa na ujenzi wa ukuta mirerani.. Tunapiga hatua kurudi nyuma), nimeshuhudia yasiyowezekana yakiwezekana (japo kuna makengeza! Yule mupe yule muruke) na kadhalika wa kadhalika kama TTCL NA AIRTEL, ya NHC.... Kwa ujumla wake mkuu ukitumia MAGAZIJUTO ni makaburi ya zamani

Taharuki yangu hii hapa...! Ni simanzi pia... Manunuzi yasiyozingatia kanuni na taratibu tulizojiwekea.... Maamuzi yasiyofuata katiba na utawala wa sheria... Makosa kwenye miradi ya maendeleo na taratibu zilizovunjwa.... Usalama wetu! Wapiga mbiu... Nk nk.... Nikiyaangalia haya kwa jicho kodo naona wazi na bila kificho ni makaburi mapya tunayoyasakafia kwa ufundi uliokosa viwango...

Nimeshindwa kuacha ugaguzi kuunga mkono juhudi....!!!

Salam toka Msata kilingeni
 
Huyu bwana ataacha madudu mengi na akirithiwa na wa chama chake nae atalindwa kama anavyolinda waliomtangulia.

Lengo la kukwepa taratibu na sheria ni iliwa wapate mwanya wa kupiga madili huku wakituzuga kwa kuibua ya wengine alafu wanayamaliza kisanii kwa style ya kulindana huku mazwazwa yanashangilia.
 
Mmmmh!!!!"naam,naam!tafakari tunduizi kutoka kwa gwiji wa kilinge kisicho na inda wala tashtiti huko Msata.Yataka akili fumbuzi kuchimbuwa mifuniko ya mashimo tele yaliyotegwa njiani mwa ubongo wakati ukitiririka kwa mseleleko kuchambua nahau na methali zilizo beba dhima na dhamira ya muhenga huyu.Heko manju.
 
Mmmmh!!!!"naam,naam!tafakari tunduizi kutoka kwa gwiji wa kilinge kisicho na inda wala tashtiti huko Msata.Yataka akili fumbuzi kuchimbuwa mifuniko ya mashimo tele yaliyotegwa njiani mwa ubongo wakati ukitiririka kwa mseleleko kuchambua nahau na methali zilizo beba dhima na dhamira ya muhenga huyu.Heko manju.
Asante... Shukraani kwa fasihi jadidi
 
Back
Top Bottom