JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Kwa mujibu wa mdau mmoja, Disemba 12, 2019 aliona kwenye taarifa ya habari ya chombo kimoja wakitangaza kuwa familia moja imepoteza watoto wao wanne kwa kile kinachodaiwa kuwa walikula mihogo yenye sumu. Aidha, mada hii imekuwa inazungumzwa sana mitaani, huku ikiacha mashaka makubwa kwa kuwa mihogo ni chakula kinachotumika kwa kiasi kikubwa, kama kingekuwa na sumu basi watu wengi wangekuwa wamepoteza maisha. Tuelewe nini kuhusu madai haya? Ni kweli kuwa mihogo huwa na sumu, au ni uzushi tu unaopaswa kupuuzwa?
UVUMI Hivi karibuni baada ya Elon Musk kuununua mtandao wa Twitter kuliibuka uvumi kwamba bilionea huyo amepanga kurejesha akaunti zote za Twitter zilizofungiwa, kasoro ile ya aliyekuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 2017 hadi 2021, Donald Trump. Kichwa cha habari cha taarifa hiyo kinasomeka kwa Kiingereza: “Elon Musk States Intention to Restore Every Banned Twitter Account, ‘Except For Donald Trump’, huku ikifuatiwa na maandishi yasomekayo kwa Kiingereza: "It may seem petty but I just don’t like him"- ikimaanisha kuwa ni jambo linaweza kuoneka dogo, ila yeye (Elon Musk) hampendi tu Donald Trump. Picha (screenshot) hiyo inayodaiwa kutoka ukurasa wa gazeti maarufu la Marekani, New York Times, imekuwa ikizunguka kwenye mitandao ya...
Siku chache baada ya kufariki nywele za mtu pamoja na kucha zake huonekana zikiwa zimeongezeka urefu. Jambo hili huonekana mara nyingi sana, linaweza pia kuthibitika kwa kutazama masalia ya binadamu yanayoibuliwa kila kukicha. Baada ya kufariki, sayansi inasema kuwa ukuaji wa kiumbehai kupitia seli hai zake hufikia mwisho, mifumo yote tendaji hukoma na hakuna jambo lolote ambalo huendelea. Kwanini ukuaji wa sehemu hizi unapingana na sayansi?
Tovuti moja inadai kutangaza nafasi za ufadhili wa masomo katika chuo kikuu nchini Norway na kusambaa katika mitandao ya kijamii. Tovuti hiyo ina ujumbe wa Kiingereza ulioandikwa vibaya unaotafsirika: "Kasome Nchini Norway Kozi Yoyote Uliyochagua Bila Malipo kwa Muda wote wa programu" "Programu ya Scholarship ya Chuo Kikuu cha Bergen Huwawezesha Wanafunzi wa Kimataifa Kusoma nchini Norway kwa Raha na Bure. Waombaji wajaze fomu hapa chini na kubofya Omba,” Tovuti hiyo ambayo ina muonekano wa kutilia shaka (norway.visa2abroad.online) imechapisha “nafasi” hizo kwenye makundi ya mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, na katika nchi kadhaa ikiwemo Tanzania. Tovuti hiyo pia inaonesha "fomu ya maombi" ambayo inataka muombaji kujaza...
Kuna tetesi zimeibuka leo 25/10/2022 zinadai kuwa Yanga imeachana na kocha wake Mkuu Nasreddin Nabi. Tetesi hizi zimeshika kasi baada ya kuchapishwa na Gazeti la Mwanaspoti pamoja na kutumwa kwenye mitandao ya kijamii. Mpaka kufikia saa saba mchana Uongozi wa Yanga, umeendelea kuwa kimya na kutokuwa tayari kulizungumzia suala hilo, hata walipotafutwa wamesema Nabi bado ni kocha wa timu hiyo hadi hapo itakaptangazwa kivingine.
Madai Shirika la utangazaji la BBC liliripoti kuwa nchi ya China ina mpango wa kufungua vituo vya polisi nchini Nigeria, Lesotho na Tanzania ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na raia wake wanaoishi katika nchi hizo tatu za Afrika, tovuti inayomilikiwa na mtu binafsi ya Nigeria ya Vanguard imeripoti. Wakiwanukuu watetezi wa Usalama, Vanguard amesema mpangilio wa China unaweza kuonekana kama shambulio dhidi ya uhuru wa eneo husika. Aidha inaelezwa kuwa, [China] imeamua… kushirikiana na United Front linked, mashirika ambayo yako nje ya nchi katika mabara matano, kuanzisha mfumo mbadala wa polisi na mahakama ndani ya nchi tatu, na kuhusisha moja kwa moja mashirika hayo katika mbinu zisizo halali zinazotumiwa kuwasaka...
Back
Top Bottom