UZUSHI Video inasambaa ikionesha Mwanajeshi wa Marekani (Texas) akiwavusha Wahamiaji haramu

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Salaam Ndugu zangu,

Nimekutana na video kupitia mtandao wa Tiktok ikimuonesha Mwanajeshi wa Texas akiwavusha Wakimbizi kimagendo.

Je, kuna ukweli wowote kwenye hili?

picha border.jpeg

Picha haihusiani na habari. Credit: AP News


 
Tunachokijua
Tangu Mei 17 kupitia mtandao wa TikTok kuliibuka taharuki sehemu mbalimbali baada ya kuanza kusambaa video ambayo ikionesha mtu aliye katika sare za kijeshi za Marekeani akiwafungulia Wakimbizi geti kimagendo. Video hiyo (Tazama hapo juu) iliambatana na ujumbe huu:

"Askari wa Marekani waliovaa sare wamenaswa kwenye video wakifungua lango la mpaka na kuwaruhusu Wahamiaji Haramu ambapo wanachukuliwa haraka na kupelekwa mbali.. Nani alitoa Amri hii?"

Katika video hiyo ya sekunde 45 hivi, watu wanaonekana wakitembea kando ya ukingo wa mto na kupita kupitia lango ambalo ni sehemu ya uzio mrefu wa waya wa chuma. Mtu mwenye mavazi ya kijeshi anaonekana akisimamia zoezi hilo. Mwishoni linaonekana basi jeupe llinakuja na kisha watu hao wakiingia kwenye basi hilo.

Je, ni upi ukweli wa jambo hili?
JamiiForums imefatilia taarifa hii katika vyanzo mbalimbali vinavyoaminika ili kujua uhalisia wa taarifa hii inayosambaa ambapo taarifa zinaeleza yafuatayo

Kwa mujibu wa taasisi ya PolitiFact na EP News wanaeleza kuwa Mwanajeshi huyo aliyeonekana katika video hiyo ni Mwanachama wa Kikosi cha Kitaifa cha Missouri ambaye alikuwa akisaidia wafanyakazi wa Ulinzi na Uhamiaji wa Marekani karibu na eneo linaloitwa Eagle Pass, Texas tukio hili lilitokea mnamo tarehe 15 Mei 2023.

Zaidi ya hayo, Msemaji wa Jeshi la Uhamiaji na Ulinzi wa Mpaka nchi Marekani ameeleza kuwa Wahamiaji wanaoonekana kwenye Video hiyo tayari walikuwa wameshaingia katika ardhi ya Marekani, baada ya awali kuvuka Mto Rio Grande kutoka Mexico, na kwamba Idara ya Ulinzi wa Mpaka ilikuwa na wajibu wa kuwaweka mikononi mwao.

Hivyo, kutokana na ufafanuzi huo si kweli kwamba Wanajeshi wa Marekani walikuwa wanavusha Wahamiaji haramu kimagendo isipokuwa watu hao walikuwa tayari ndani ya Ardhi ya Marekani na watu wa usalama walikuwa wanatekeleza wajibu wao.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom