JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Nimekuwa nikisikia kuwa wabunge wetu hawalipi kodi kwenye mshahara mnono wanaopata. Kuwa walimu wanalipwa Tsh 400,000 lakini kamshahara hako kanaliwa na PAYE. Wabunge wetu wakiwa kwenye vikao, sitting allowance na Perdiem wanakunja 470,000 kwa siku, Mshahara wa mwisho wa mwezi nao mnono hatari. Je, hakuna sababu ya wabunge kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi? Tena napendekeza hata yale marupurupu wanayopata nayo yakatwe kodi.
Hatua za ukuaji wa mtoto huambatana na mabadiliko mengi ya kimwili. Mojawapo ya mabadiliko hayo ni kung’oka kwa meno ya awali na kuota kwa meno ya kudumu. Mdau wa JamiiForums ametoa hoja kuwa meno ya mtoto mwenye umri kati ya miaka 6-7 yanapotingishika kisha yakaendelea kukaa pasipo kung’olewa husababisha meno mengine kuota kwa pembeni, hivyo ni lazima yang'olewe ili kuepusha kutokea kwa tatizo hili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?
Kuna kijiwe huku Bonyokwa tunapiga stori za kawaida kuhusu nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Sasa kuna jamaa kasema kuwa Rais wa awamu ya pili nchini Kenya, Hayati Daniel Arap Moi wakati anaingia madarakani hakuwa na mahusiano kabisa na hakutaka kujihusisha nayo kabisa. Nguvu kubwa alielekeza katika malezi ya watoto. Jambo hili lilimfanya ahudumu miaka 24 ya urais bila kuwa na mke (First Lady) jambo ambalo halijazoeleka ulimwenguni, kwamba kuwe na mtawala asiye na mwenza. Daniel Toroitich Arap Moi (Google)
Bado nipo njiapanda, nimesikia kuwa mwanamke mjamzito akinywa pombe kwa kiwango kikubwa wakati wa ujauzito basi huweza kusababisha changamoto kubwa sana kwa mtoto. Kuna wajawazito kadhaa nimepata kuwaona wakinywa pombe tena kali sana lakini hizo changamoto kwa watoto wao sijaziona. Baadhi ya changamoto nilizoambiwa ni kuwa na kichwa kidogo isivyo kawaida, uso bapa, macho madogo, pua ndogo nk Naomba kujua hili ili nimkanye mama kijacho kufakamia mipombe asijeleta balaa ndani.
Kuna mwanamama aliwahi nipa ushuhuda kuwa matiti yake yalianza kuanguka akiwa na miaka 23 kutokana na mitomaso aliyokuwa anafanyiwa na mpenzi wake wa kwanza. Aliendelea kwa kusema kuwa, kabla ya kuanza michezo na wanaume alikuwa na chuchu dodo zilizosimama na kuchoma. Hivi ni kweli kuwa matiti ya mwanamke yanapopapaswa na viganja vya mwanaume hupelekea kuanguka na kuwa ndala?
MADAI Mdau wa JamiiForums ametoa mkasa mmoja unaomhusisha mume wa rafiki yake wa kike aliyeanza kuonesha dalili za ujauzito kwenye ujauzito mchanga wa mkewe. Mdau anaeleza kwamba shemeji yake huyu ilikuwa kila asubuhi anatapika njano, na homa za hapa na pale na kila alipoenda hospital Ugonjwa haukuonekana, ilifikia wakati mwanamme akawa hawezi kufanya shughuli zake kwa sababu ya kutapika sana. Baada ya kupima ilikuja kugundulika kuwa mkewe alikuwa na ujauzito. Ikasemekena kwamba kuna nyakati fulani ujauzito anabeba mwanamke Ila mabadiliko na dalili za ujauzito anakuwa nazo mwanaume. Jambo hili ni kweli au uzushi?
Back
Top Bottom