Kama ilivyo kwa watu wengi, nimekuwa nikisikia hadithi na imani mbalimbali za mitaani kuhusu matumizi ya limau. Hivi karibuni, niliamua kunywa maji ya limau kwa wingi. Lengo langu halikuwa kufanya majaribio ya kitabibu, bali ilikuwa ni sehemu ya utaratibu wangu tu wa kawaida.
Huwa nimewahi kusikia kuwa ukitaka kusogeza siku zako ziende mbele unatakiwa kunywa juisi ya malimao. Nikajaribu baada ya kunywa hedhi ikakakta ghafla kwa siku kadhaa ikarudi tena na inasemekana pia kuwa ukinywa limau nyingi kabla ya hedhi kuanza, utapata siku chache sana (kwa mfano siku mbili badala ya tano).
Je, huu ni ukweli wa kisayansi au ni sadfa (coincidence) tu?