Wahaya wote inawahusu!!!

Wasalaam wana Jamvi.
Kama wewe ni muhaya au ulizaliwa katika mkoa wa Kagera au una ndugu yako
aliyefanikiwa kujiunga na chuo kikuu mwaka 2012/13 basi hii inakuhusu.
Binafsi nimeona ni busara kuwakutanisha wahaya wote tulioko vyuoni na
tuliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu au taasisi za elimu ya juu,ili.:
1.Tuweze kupanga mikakati ya kuendeleza wenzetu(wahaya) walioko chini
yetu.
2. Tuweze kupanga mikakati ya kuendeleza na kuwasaidia wahaya wenzetu
kielimu walioko vijijini na waweze kuwa kama sisi.
3. Kupitisha sheria ndogo kwa wahaya itakayokuwa inawaamuru kila Muhaya
kufikia kiwango cha elimu cha angalau shahada ya kwanza.(atleast 1st
degree)
4. Kupanga mikakati ya kuiendeleza Kagera kiuchumi na kielimu , na
ifikapo 2020 kila kijiji kiwe na graduates wasiopungua 20.
"WAHAYA ELIMU KWANZA"
NB: KAMA WEWE UNA JAMBO LOLOTE LA KUCHANGIA JINSI YA KUFANIKISHA HAYA
BASI KARIBU LAKINI KAMA UNATAKA KUTUKANA NA WEWE KARIBU.

hii mada inachefua kweli. Vp rais akiwa mhaya!!!! dah, masifa camp jamani!!
 
Hii mada ni ya mwaka jana lakini naona imerudishwa tena baada ya kitambo kirefu.

Kwa taarifa tu ni kwamba, mchakato wa kufahamiana umeenda vizuri na sasa tuko kwenye hatua za mwisho za kuform vikundi mbalimbali vya wahaya hapa chuoni(UDSM) vitakavyojihusha na uhamasishaji wa wenzao huko mitaani pindi semister itakapo isha.

Napenda kutoa shukrani kwa wahaya wote walio nipa ushirikiano wa hali na mali katika kufanikisha hili. Ni matumaini yetu sote kuwa lengo tuliloweka lazima litimie ili tuondokane na ujing
 
1. Kwa takwimu za siku za Karibuni (Household Budget Survey 2010/2011).. Kagera is the economically 2nd poorest region in Tanzania only bitting Singida! Dar is the richest, followed by Mwanza, Arusha, Kilimanjaro!!

Watu wa Kagera acheni kutamba!!! Wekezeni Kagera kama watu wengine wanavyowekeza katika Mikoa yao!

2. Why? Kagera is fertile region, it has learned population (some who in fact stay in Oysterbay), it is bordering many countries (Uganda, Rwanda and Burundi), plenty of fish! n.k, n.k

Sasa mimi sijui kwa nini mkoa huu uanzidi kuwa nyuma wakati kuna raslimali zote hapo juu!

Natoa hoja

kwa masifa haya, kweli wewe ni mhaya...ajabu yake sasa huna hata kitu unatembelea ndala tu hapo, mawazo yako yote yapo chini kuwaza wanawake wakati huohuo hujakata govi, kati ya makabila ya kutojisifia ni kabila la wahaya, ndo maana kama wewe mhaya bora ukifika mbele za watu ujitambulishe kama wewe ni mtz tu na si mhaya specifikally, ....lakini tusipoteze muda na huyu kinyangarika, yeye ndo anaanza mwaka wa kwanza chuo kikuu, ....na ndo anaanza kuwaza leo, siku zote alikuwa amelala na hajui kinachoendelea katika karne hii ya 21....sisi wengine huko kwenye vyuo tulishaacha miaka mingi sana na tuna watoto kama yeye...unahitaji maombi na msaada mkubwa sana.

uhayani nimeishi, na juzi nilipita kule kikazi, bora hata umasaini, unakuta mtu amechokaaa kavaa suti na kandambili lakini kiburi sasaaaa, anajiona yeye emetoka new york leo...hahaha. sifuri hizi bwana bora hata ya oooooo, kwa ukabila huu nakutabiria sup nyingi sana chuo, na utatoka na failure mbaya sana, ila nakuombe usidisco kwasababu pamoja na weuzi na govi lako hilo ndo na madem utakosa wote na utakufa kwa presha.
 
Duh hasira na wivu tu. Wahaya ni wahaya. Hata. Ukienda Musoma lazima nao wana watu wao, kuishi mkoani kwao sio lazima wakuhusishe na mambo yao ya esp vijijini.

Sio mkoani kwao wewe,mkoa ni wetu sote.Hili la kuendeleza kabila lao ndo shida,angeweka heading kwamba WANA KAGERA WOTE HILI LINAWAHUSU.Tofauti na hapo,na akiendelea ivo,ndo yale yale ya Wahutu.
 
Hapa sijaona ukabila, anataka wahaya wasaidiane kwenye elimu na kwa fursa hii na nyie wasukuma, wachaga, wanyakyusa, wahehe makabila yote itaneni msaidiane katika elimu ili mwisho wa yote makabila yote yawe yamesoma. Nani ataumizwa na huu utaratibu huu.
Angesema wahaya wote msio na kazi njooni kwenye wizara fulani au kitengo fulani cha serikali muulizie fulani. Huo ndiyo ukabila. kuwanyiama au kuwapa watu fursa kwasababu ya kabila lao. Tungemuwashia moto

Hapa anaitisha kitu ambacho wenzetu wakenya wanakiita Harambee na sio ukabila. Hilo la kutaja course yake ni ile wakale walisema jasiri haachi asili.
 
watanzania kawaida yetu ni maselfish sana ndio maana hata kazi watu wanapeana kimtindo mtindo......kwahiyo network mnayotaka kuitengeneza nayo itakuwa na madhumuni ya kibinafsi kama yakupena job!
 
Samehe bure,ukabila utakwisha taratibu kadiri miaka inavyokwenda.mbona tunaoleana kwa sana siku hizi, ipo siku tutakuwa kabila moja la watanzania.
 
Wasalaam wana Jamvi.Kama wewe ni muhaya au ulizaliwa katika mkoa wa Kagera au una ndugu yako aliyefanikiwa kujiunga na chuo kikuu mwaka 2012/13 basi hii inakuhusu.Binafsi nimeona ni busara kuwakutanisha wahaya wote tulioko vyuoni na tuliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu au taasisi za elimu ya juu,ili.:1.Tuweze kupanga mikakati ya kuendeleza wenzetu(wahaya) walioko chini yetu.2. Tuweze kupanga mikakati ya kuendeleza na kuwasaidia wahaya wenzetu kielimu walioko vijijini na waweze kuwa kama sisi.3. UPDATES:Napenda kutoa taarifa ya hatua tulizo zifikia katika uhamasishaji. Mwaka jana September nilileta mada ya uhamasishaji wa wahaya waliopo vyuoni kuungana na kuweka mikakati ya kuendeleza wenzao walioko vijijini. Nilipata majibu mbalimbali, yakiwa ni yakutia moyo lakini pia ya kukatisha tamaa. Wengi walio nijibu hovyo hawakunielewa nia yangu, ila walinishutumu kuwa mimi ni mkabila.Lahasha mimi sio mkabila, ila sina uwezo wakuhamasisha vikundi vyote katika nchi hii. Nilichagua kuhamasisha watu wa nyumbani(WAHAYA) na mchakato umeenda vizuri sana, kwani nimepewa ushirikiano mkubwa sana hapa chuoni.(UDSM).Napenda kutoa shukrani za dhati kwa wahaya wote walio onesha ushirikiano na kunipa nguvu ki hali na mali. Hakika umoja ni nguvu.Mpaka sasa tumesha unda vikundi kazi vy uhamasishaji, na lengo kuu ni kwamba tunataka ifikapo 2020, angalau kila kaya iwe na kichwa kimoja chenye elimu ya chuo kikuu.Pia malengo mapya ni kuendeleza mkoa wetu wa Kagera na tuna malengo ya kufanya mji wa Bukoba kuwa jiji ndani ya miaka michache ijayo. Hii itatokana na sisi wana chuo kuwekeza zaidi kwetu pindi tunapomaliza elimu yetu ya juu.Kuna minong'ono inayoendelea mitaani kuwa rais wa nchi hii haawezi kuwa Muhaya. Basi sisi kama wana Kagera tunataka kuwaondolea mawazo hayo watanzania hasa kizazi cha sasa. Hata ikitokea tukapata mgombea urais kutoka Kagera basi ukabila isiwe kikwazo.Tuna panga kufanya mkutano mkuu mwishoni mwa semister hii hapa chuoni ili kuona ni vipi tunaweza kufanikisha mipango yetu.Nitaendelea kuwapa taarifa kwa yale yote tutakayo afikiana.NATOA WITO KWA MAKABILA MENGINE KUIGA MFANO HUU, KWANI NI NJIA RAHISI KUFIKIA MAENDELEO.
Mimi sitoke bukoba ila jitihada zako mali kwelikweli. Badala ya kuitwa mkabila mikoa yote hasa pwani lindi na mtwara walioko vyuoni igeni badala ya kuwasikiliza waongo eti kuna mfumo kristo.
 
Wazo zuri ila rekebisha sema wana kagera woote, wazo zuri sana, saidianeni masuala ya elimu na kiuchumi achaneni na mambo ya urais mtaonekana wakabila.
 
Mkuu wazo lako ni zuri ila ungetumia wanaKAGERA,CIO WAHAYA!!sababu hata nyie ndani ya hao Wahaya Mnabaguana!!!
 
1. Kwa takwimu za siku za Karibuni (Household Budget Survey 2010/2011).. Kagera is the economically 2nd poorest region in Tanzania only bitting Singida! Dar is the richest, followed by Mwanza, Arusha, Kilimanjaro!!

Watu wa Kagera acheni kutamba!!! Wekezeni Kagera kama watu wengine wanavyowekeza katika Mikoa yao!

2. Why? Kagera is fertile region, it has learned population (some who in fact stay in Oysterbay), it is bordering many countries (Uganda, Rwanda and Burundi), plenty of fish! n.k, n.k

Sasa mimi sijui kwa nini mkoa huu uanzidi kuwa nyuma wakati kuna raslimali zote hapo juu!

Natoa hoja
Kusema kweli takwimu hizo huwa zinanishangaza sana!kwani nikiangalia umasikini wa Dodoma sidhani kama umaskini huo upo Kagera!Inafika mahali nalazimika kuamini huenda takwimu hizi hupikwa tu kwa malengo yasiyoeleweka!Mikoa inayopiga kelele sana kuwa imetelekezwa kimaendeleo mf Lindi,Mtwara na Kigoma ni ya ngapi?Ila nawapa Hongera Nshomire kwa kuweka mikakati ya kimaendeleo.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ni muhimu sana kukumbuka nyumbani. naunga mkono

Wasalaam wana Jamvi.Kama wewe ni muhaya au ulizaliwa katika mkoa wa Kagera au una ndugu yako aliyefanikiwa kujiunga na chuo kikuu mwaka 2012/13 basi hii inakuhusu.Binafsi nimeona ni busara kuwakutanisha wahaya wote tulioko vyuoni na tuliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu au taasisi za elimu ya juu,ili.:1.Tuweze kupanga mikakati ya kuendeleza wenzetu(wahaya) walioko chini yetu.2. Tuweze kupanga mikakati ya kuendeleza na kuwasaidia wahaya wenzetu kielimu walioko vijijini na waweze kuwa kama sisi.3. UPDATES:Napenda kutoa taarifa ya hatua tulizo zifikia katika uhamasishaji. Mwaka jana September nilileta mada ya uhamasishaji wa wahaya waliopo vyuoni kuungana na kuweka mikakati ya kuendeleza wenzao walioko vijijini. Nilipata majibu mbalimbali, yakiwa ni yakutia moyo lakini pia ya kukatisha tamaa. Wengi walio nijibu hovyo hawakunielewa nia yangu, ila walinishutumu kuwa mimi ni mkabila.Lahasha mimi sio mkabila, ila sina uwezo wakuhamasisha vikundi vyote katika nchi hii. Nilichagua kuhamasisha watu wa nyumbani(WAHAYA) na mchakato umeenda vizuri sana, kwani nimepewa ushirikiano mkubwa sana hapa chuoni.(UDSM).Napenda kutoa shukrani za dhati kwa wahaya wote walio onesha ushirikiano na kunipa nguvu ki hali na mali. Hakika umoja ni nguvu.Mpaka sasa tumesha unda vikundi kazi vy uhamasishaji, na lengo kuu ni kwamba tunataka ifikapo 2020, angalau kila kaya iwe na kichwa kimoja chenye elimu ya chuo kikuu.Pia malengo mapya ni kuendeleza mkoa wetu wa Kagera na tuna malengo ya kufanya mji wa Bukoba kuwa jiji ndani ya miaka michache ijayo. Hii itatokana na sisi wana chuo kuwekeza zaidi kwetu pindi tunapomaliza elimu yetu ya juu.Kuna minong'ono inayoendelea mitaani kuwa rais wa nchi hii haawezi kuwa Muhaya. Basi sisi kama wana Kagera tunataka kuwaondolea mawazo hayo watanzania hasa kizazi cha sasa. Hata ikitokea tukapata mgombea urais kutoka Kagera basi ukabila isiwe kikwazo.Tuna panga kufanya mkutano mkuu mwishoni mwa semister hii hapa chuoni ili kuona ni vipi tunaweza kufanikisha mipango yetu.Nitaendelea kuwapa taarifa kwa yale yote tutakayo afikiana.NATOA WITO KWA MAKABILA MENGINE KUIGA MFANO HUU, KWANI NI NJIA RAHISI KUFIKIA MAENDELEO.
 
Naunga mkono kabisa, suala la kuendeleza sehemu yako ya asili si ukabila. Lazima watu waelewe tafsiri halisi ya ukabila nini? Huwezi kusaidia watoto wajirani wakati wa kwako wanalia njaa. Hata misaada tunayopata kutoka ulaya, marekani na mabara mengine ni masazo tu.

Ndiyo maana maeneo mengi ya vijijini hayaendelee kwa sababu ya dhana ya Ukabila. Nyie vijana mimi binafsi nawaunga mkono. Endapo nitakuwa na uwezo wa kusaidia nitasaidia.

Aluta Kontinua.
 
ukabila bado upo ,, na hawa wahaya ndo wenyewe.... pale mlimani wamejazana kama uchafu ,,, kila depertment imejaa wahaya ,,,,, sehemu ambayo wameshindwa kupenya ni UDBS tu peke yake....

Tueleze ni kitu gani kimewashinda kupenya UDBS?
 
Nachokiona ni hatred kwa watu ila kama ulivyosema maendeleo ni watu,kaeni pamoja msaidie nyumbani nami niko nanyi pa1
 
Ni vizuri kuhamasisha madanguro ya wahaya waach... Mana naskia ata buku 2 unamaliza shughuli yako kwao
 
Back
Top Bottom