Nchi ambazo hazina Viwanja vya Ndege

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Sisi wahaya ni watu ambao ndio makabila ya mwanzo kuanza kuvuka border, ni watu tuliwahi kupata exposure mapema, ukibisha basi nenda Vatican umuulize Pope ni kabila gani kutoka Tanzania ambalo kila siku makadinali wake wanaongoza kuongia Vatican utaambiwa ni wahaya, Juzi kati tu Papa kamuapisha Rugambwa huyo ni muhaya.

Sasa kwenye kusafiri safiri kwetu, nataka nikwambie wewe Msukuma au mzaramo kuwa Si kila nchi ina uwanja wa ndege bro, kuna nchi nyingine huwa hazina hata viwanja vya ndege, sasa unafikaje huko ukitaka kwenda? Ni rahisi sana, unatumia usafiri wa treni ama basi kuingia katika nchi hizo.

Hizi ni baadhi ya nchi zisizokuwa na viwanja va ndege.

1. Andorra: Hii nchi haijawahi kuwa na uwanja wa ndege. Ni nchi ndogo kule Ulaya, wao wanatumia viwanja vya nchi mbili, yaani Ufaransa na Hispania ambazo zimepakana nazo. So ukitaka kwenda huko, utakwenda mpaka Hispania ama Ufaransa, hapo utachukua treni ama basi kuingia nchini Andorra. Japo pia unaweza kutumia barabara za magari kufika katika nchi hiyo.

2. Liechtenstein: Kama ilivyo kwa Andorra, hi nchi nayo haina uwanja wa ndege. Ukitaka kuingia nchini humo, utakwenda nchini Uswisi ama Ujerumani ambapo huko sasa utachukua basi ama treni kuingia nchini humo.

3. Monaco: Hapa kuna watu watajiuliza kwa nini Monaco ni nchi na si moja ya miji nchini Ufaransa? Majibu yake ni marefu na kuna siku nitakuja kukwambia kwa nini Monaco hujulikana kama nchi na si mji. Hapo Monaco napo hakuna uwanja wa ndege. Ukitaka kwenda nchini humo, kwanza utatakiwa kutumia uwanja wa ndege wa nchini Ufaransa ndipo utaweza kuingia Monaco kwa treni ama basi.

4. San Marino: Hawa washikaji nao hawana uwanja wa ndege, wanautumia uwanja wa nchini Italia. Ukitaka kwenda kwao, cha kwanza nenda Italia, hapo utachukua treni ama basi kwenda huko.

5. Vatican: Hapa tunakutana na ile ishu ya Monaco. Vatican ilikuwa nchini Italia lakini baadaye nao wakajulikana kama nchi. Vatican ina serikali yake inayoongozwa na Papa. Wana jeshi lao, wana utajiri mkubwa mno. Pamoja na nguvu yao kubwa duniani, nao hawana uwanja wa ndege, ukitaka kwenda Vatican, ni lazima utue nchini Italia na utakwenda huko kwa usafiri mwingine. Hapa wahaya ni kama nyumbani kwao.
 
Muhaya hujambo kwa kujisifia! Labda nikuambie tu hizo si nchi ni miji tu yenye utawala wake ndani ya nchi kubwa, afadhali ya zanzibar yetu. Ni viinchi vidogo sana kuliko hata mikoa yetu. Hata dar es salaam inaweza kujiita nchi. Hizo nchi ziko chini ya ufaransa, hispania, ujerumani, italia
 
Bukoba pia hamna uwanja wa maana hadi ufike mwanza kwa wasukuma na dar kwa wazaramo ndio unaweza panda ndege uende ulaya
 
Back
Top Bottom