Ni aibu kubwa mwanafunzi awe na first class GPA chuoni abaki mtaani, hawa watu wabakizwe vyuoni, mtaani bila mitaji wanateseka sana

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Imagine mtu ana gpa ya 4.5 hadi 4.9 sijawai ona 5.0) , anamaliza chuo anarudi kitaa na kwao hawapo njema kiuchumi hawezi pata mtaji kirahisi, umaarufu wa kupata gpa nzuri unageuka kumuaibisha.

Na mara nyingi aina hii ya watu ni wale tuliokuwa tunawaita kina john kisomo, Sehemu wanayoiwezea zaidi ni masomo na taaluma walizosomea vyuoni, nje ya hapo mambo mengi ni mapya, ni heri wawe wanabakizwa vyuoni wawe hata tutorial assistants, pia huwa wanakuwa wachache unakuta kozi nzima yupo moja ama wawili na si ajabu baadhi ya miaka hawapo kabisa.

Watu hawa wana stress sana, oili waliyochoma chuoni inakuwa imeenda bure,
 
Imagine mtu ana gpa ya 4.5 hadi 4.9 huko, anamaliza chuo anarudi kitaa na kwao hawapo njema kiuchumi hawezi pata mtaji kirahisi, inakuwa ni aibu sana, umaarufu wa kupata gpa nzuri unageuka kumuaibisha.

Watu hawa wana stress sana, oili waliyochoma chuoni inakuwa imeenda bure,
"Life is not fair" alisema nani hii kauli?

NB:

Maisha ni zaidi ya kupata first class GPA, Wahenga husema "Maisha ni fumbo".
 
Watu wanaosota na hizo gpa ni wale waliosoma vyuo vya kufaulishwa na wamesoma kozi ambazo hazitumii calculator sana.

Ni ngumu sana mtu aliesoma public university na kupata first class ya accounting ama ya STEM degree yoyote halafu akose mchongo.

Big four Auditing firms zinawapenda sana hao vipanga. Na zina programe za kuwaajiri kila mwaka.

Hapo hujaweka na kampuni ndogo ndogo za proffessional services nazo zinategea ambao hawaendi big four
 
Imagine mtu ana gpa ya 4.5 hadi 4.9 sijawai ona 5.0) , anamaliza chuo anarudi kitaa na kwao hawapo njema kiuchumi hawezi pata mtaji kirahisi, umaarufu wa kupata gpa nzuri unageuka kumuaibisha.

Na mara nyingi aina hii ya watu ni wale tuliokuwa tunawaita kina john kisomo, Sehemu wanayoiwezea zaidi ni masomo na taaluma walizosomea vyuoni, nje ya hapo mambo mengi ni mapya, ni heri wawe wanabakizwa vyuoni wawe hata tutorial assistants.

Watu hawa wana stress sana, oili waliyochoma chuoni inakuwa imeenda bure,
Sifa ya mtu mwenye digrii ya kwanza kuajiriwa kufundisha chuo lazima awe na kuanzia 3.8GPA.

Huyu mtu huajiriwa kwenye ngazi ya mkufunzi (tutorial assistant). Hiyo huwa ni nafasi ya mafunzo kazini, huku akitakiwa kwenda kusoma digrii ya umahiri (master's degree).

Ila sasa, kuwa na 'first class' haimaanishi huyo mtu yuko vizuri kwenye kufundisha. Hivyo, kinachofanyika, nafasi zinatangazwa ili wote wenye sifa stahiki waweze kupambania 'kombe'.

Iliwahi kutokea kwenye chuo kikubwa hapa nchini. Walikuwa wanawabakiza hao wenye first class. Ila baadhi walikuwa wanachemka kwenye master's degree, na pia kwenye utendaji.

Hivyo, maamuzi yakabadilishwa. Nafasi za kazi zitangazwe, wenye sifa washindanishwe kwenye written na oral interviews, ili wenye uwezo wapatikane. Utashangaa mwenye first class kachemka ila mwenye upper second class kafanya vizuri. Haya yametokea sana tu.
 
Imagine mtu ana gpa ya 4.5 hadi 4.9 sijawai ona 5.0) , anamaliza chuo anarudi kitaa na kwao hawapo njema kiuchumi hawezi pata mtaji kirahisi, umaarufu wa kupata gpa nzuri unageuka kumuaibisha.

Na mara nyingi aina hii ya watu ni wale tuliokuwa tunawaita kina john kisomo, Sehemu wanayoiwezea zaidi ni masomo na taaluma walizosomea vyuoni, nje ya hapo mambo mengi ni mapya, ni heri wawe wanabakizwa vyuoni wawe hata tutorial assistants.

Watu hawa wana stress sana, oili waliyochoma chuoni inakuwa imeenda bure,
Kila mwaka wabakishwe vyuoni si chuo kitakua na wakufunzi wengi kuliko wanafunzi,halafu watalipwa na nani!?
 
Labda kwenye course tofauti na sayansi. Kufundishwa sayansi na ICT na ma lecturer ambao hawakuwahi kupata ujuzi wa kufanyia kazi fani wanazofundisha kumeua ndoto za vijana wengi na pia imekua nichimbuko la watu wanaokaririshwa theories ila practical 0.
 
Imagine mtu ana gpa ya 4.5 hadi 4.9 sijawai ona 5.0) , anamaliza chuo anarudi kitaa na kwao hawapo njema kiuchumi hawezi pata mtaji kirahisi, umaarufu wa kupata gpa nzuri unageuka kumuaibisha.

Na mara nyingi aina hii ya watu ni wale tuliokuwa tunawaita kina john kisomo, Sehemu wanayoiwezea zaidi ni masomo na taaluma walizosomea vyuoni, nje ya hapo mambo mengi ni mapya, ni heri wawe wanabakizwa vyuoni wawe hata tutorial assistants.

Watu hawa wana stress sana, oili waliyochoma chuoni inakuwa imeenda bure,

Hizi GPA za kupata hadi 4.9 siku hizi zinatoka wapi? Ina maana hata chuo kikuu alichosoma huyo mwanafunzi wameshindwa kumuajiri?
Nina mashaka makubwa na Grade Point Averages (GPA) za miaka hii kwa kweli! Maana yake hapo kwa miaka yote aliyosoma mwanachuo iwe mitano, minne au mitatu alikuwa akipata almost A kila somo kwa kila mwaka. Basi mitaala ya miaka hii ni ya ubabaishaji kabisa!
Zamani ilikuwa kazi mnoo kupata GPA ya aina hiyo, na ikitokea hivyo mwanachuo alikuwa anagombaniwa kama mpira wa kona na idara alizosoma ili abaki pale kuwa tutorial assistant!
Hao wenye hizo GPA ukimwajiri utashangaa vioja sehemu ya kazi!
Anyway, maisha si lazima ajira, kama amekosa ajira aingie kwenye plan B ya maisha! Tatizo la ajira ni dunia nzima, ukisubiri kuajiriwa basi jiandae siku moja kupiga mkasi hicho cheti.
Ni ushauri tu!
 
zamani elimu ilikuwa chini sana na ngumu, sikuhizi elimu imerahisishwa waweza download kitabu sio kama zamani, kuna online discussions, past papers rahisi sana kuzipata, mejenereta yanawashwa umeme ukikatika, n.k. lakini bado first clasa kuipata ni mziki sio shughuli nyepesi
 
zamani elimu ilikuwa chini sana na ngumu, sikuhizi elimu imerahisishwa waweza download kitabu sio kama zamani, kuna online discussions, past papers rahisi sana kuzipata, mejenereta yanawashwa umeme ukikatika, n.k.

Sawa, mitihani inayotungwa ipoje standard yake? Na siyo kweli kuwa zamani elimu ilikuwa chini dhidi ya sasa kwa taarifa yako !
 
Elimu ya zamani kitabu kimoja cha library unamsubiria mwenzako amalize ili usome utalinganisha na sasa kila mwanafunzi ana kitabu kwenye simu ??

Mitihani ipo standard nzuri tu, usipojiandaa unafeli kama kawaida
 
Imagine mtu ana gpa ya 4.5 hadi 4.9 sijawai ona 5.0) , anamaliza chuo anarudi kitaa na kwao hawapo njema kiuchumi hawezi pata mtaji kirahisi, umaarufu wa kupata gpa nzuri unageuka kumuaibisha.

Na mara nyingi aina hii ya watu ni wale tuliokuwa tunawaita kina john kisomo, Sehemu wanayoiwezea zaidi ni masomo na taaluma walizosomea vyuoni, nje ya hapo mambo mengi ni mapya, ni heri wawe wanabakizwa vyuoni wawe hata tutorial assistants, pia huwa wanakuwa wachache unakuta kozi nzima yupo moja ama wawili na si ajabu baadhi ya miaka hawapo kabisa.

Watu hawa wana stress sana, oili waliyochoma chuoni inakuwa imeenda bure,
Your so naive! Reading bible is source of knowledge
 
Back
Top Bottom